Biblia: Kitabu cha Mkanganyiko au Neno la Mungu?

Biblia: Kitabu cha Mkanganyiko au Neno la Mungu?

Ndiyo maana mimi nimekomaa na Korani tu. Yenyewe imenyoka bila mikanganyiko yo yote. Na imeshushwa kutoka mbinguni na kupokelewa na mtu mmoja tu tena asiyejua kusoma wala kuandika. Kitabu cha maajabu sana. Kitabu cha kweli. Kitabu cha Allah!
 
Kwani mtoa mada haupendi mafundisho mazuri ya kwenye Biblia ?
Kama hili

Mathayo (Mat) 19:19

Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Honour thy father and thy mother: and, Thou shalt love thy neighbour as thyself.
 
Hivi kweli akili zenu zimefungwa na kufuli la Wazungu mpaka mmeshindwa kuona ukweli ulio wazi? Yaani hapa duniani hakuna kitu kinachochanganya na kuvuruga akili za watu kama hiki kitabu cha Wazungu!,
Yaani Biblia!.

Inakuwaje Mungu aliyeumba mbingu na ardhi, mwenye akili na mamlaka, aandike kitabu halafu ATUCHANGANYE kiasi hiki? Hivi mnamfanya Mungu ni mwandishi wa hadithi za abunuasi au ni nini? Mnataka kutuambia Mungu ni mbabaishaji kiasi hicho?

Angalia huu upuuzi! Wasabato wamekomalia kuishika siku ya Jumamosi, wanakuambia ukigusa kazi siku hiyo wewe ni dhambi! Dakika hiyo hiyo, wengine wanakuambia, "Acheni ushamba, Jumamosi ilikuwa ya Wayahudi, sasa hivi ni Jumapili, siku ya kufufuka!" Halafu wanakuja wengine wajuaji zaidi wanakuambia, "Ah, Sabato haihitaji siku, Sabato iko moyoni!"

Hivi mnatufanya sisi ni watoto wadogo? Mungu gani huyo anayetoa maelekezo ya siku ya kuabudu halafu kila mtu anaelewa chake? Hiki kitabu cha Wazungu kimejaa mkanganyiko kiasi kwamba hata mkipewa miaka elfu moja, hamtakaa muelewane! Ni machafuko matupu!...

Hapa ndipo kichekesho kikubwa na cha kusikitisha kilipo! Ili uelewe hiki kitabu kinachojichanganya, unaambiwa mpaka umuite ROHO MTAKATIFU aje akueleweshe!....
Yaani Mungu atupe mwongozo wa maisha, halafu wakati huo huo tumuite Roho atueleweshe? Kwani hicho kitabu kimeandikwa kwa lugha ya majini?..

Huyo Roho anayewaambia Wasabato wasile nguruwe, ndiye huyo huyo anayewaambia wa Jumapili wale nguruwe. Huyo ni Roho Mtakatifu? au ni roho ya kuchanganyikiwa iliyopandikizwa na Wazungu ili kutuvuruga akili..

Biblia hiyo hiyo inatumika na watu wanaopiga marufuku kucheza kanisani, wakisema ni fujo.
Halafu Biblia hiyo hiyo ndiyo inayotumiwa na wengine kuruka sarakasi, kupiga ngoma na mayowe utadhani wako disko, wakisingizia Daudi alicheza mpaka nguo zikaanguka!.......

Hivi huu si ni uwendawazimu? Kitabu gani hicho ambacho hakina msimamo? Leo kinaruhusu, kesho kinakataza! Huu ni mtego wa Wazungu wa kutuvuruga akili ili tu.

Utasikia mchungaji anasema, Roho ameniambia ukitumia maji haya ya baraka, unakanyaga mapepo! Biblia hiyo hiyo inatumika kuhalalisha biashara ya maji, mafuta, na vitambaa vya upako utadhani mko sokoni! Hivi Mungu amekuwa muuza maduka ya jumla?..

Mwingine anakuja na mstari wake, anasema "Roho anasema panda mbegu ya milioni moja ndiyo ufunguliwe! Maskini anatoa mpaka senti ya mwisho akitegemea muujiza, huku mchungaji akinunua gari la kifahari kwa kutumia Biblia hiyo hiyo!

Huu ni uhuni! Inakuwaje Mungu aandike kitabu ambacho kinampa nafasi tapeli yeyote kujiita Mtumishi wa Mungu halafu anatumia ujanja wa maneno kuwapokonya watu haki zao? Huu mkanganyiko ndio unazalisha hawa manabii wa uongo wanaochipuka kila kona....

Hebu niulizeni Inakuwaje Mungu aliye mmoja, mwenye akili timamu, aandike kitabu ambacho kinashindwa kutoa msimamo mmoja kuhusu mambo ya msingi?
Huyu anasema kusuka nywele ni chukizo, yule anasema ni urembo wa uumbaji..

Hivi huyo ni Mungu au ni mchezo wa kuigiza wa Wazungu? Huwezi kuwa na kitabu ambacho kinasema NDIYO na HAPANA kwa wakati mmoja! Huku ni kutuona sisi kama hatuna akili!..

Geukia upande wa pili uone wenzenu walivyojipanga. Kurani haina hizi sarakasi za kijinga!.
Kwenye kitabu cha Waarabu, sheria ni msumeno inakata pande zote! Hakuna cha tajiri, hakuna cha maskini, hakuna cha nabii wa uongo wa kujitungia tafsiri.
Kimepangika, kimeeleweka, na hakihitaji upako wa ziada kuelewa kuwa dhambi ni dhambi!..

Kama kitabu chako kinakufanya ubishane na jirani yako kila siku badala ya kukuleta kwenye toba ya kweli, basi hicho ni kitabu cha kuvuruga watu! Amkeni! Mungu hawezi kuwa mwandishi wa machafuko. Acheni kufuata hadithi za Wazungu zinazohitaji sarakasi za kiroho kueleweka.

Tafuteni neno lililonyooka ambalo halitupi nafasi ya kutoroka dhambi kwa kutumia visingizio vya kijinga!

Hebu tuchambue huu upuuzi mliolishwa, mnaambiwa ni "Neno la Mungu" wakati limejaa sarakasi ambazo hata mtoto wa chekechea anaziona.

Kule Mambo ya Walawi 11:7, Biblia hiyo hiyo inasema: "Na nguruwe... huyu ni najisi kwenu." Msimamo uko wazi, sivyo?

Lakini ruka mpaka Matendo 10:15, utamsikia huyo huyo "Mungu" wa Wazungu akimwambia Petro: "Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi!" Sasa hapa ndipo mnapopigwa changa la macho! Wasabato wanashikilia Mambo ya Walawi, Walokole wanashikilia Matendo. Hivi Mungu alisahau alichokiandika mwanzo au alibadilisha gia angani? Hii ni vurugu!

Mithali 20:1 inasema: "Mvinyo ni mshihaki, kileo ni fujo!" Inakemea ulevi mazima.
Lakini nenda 1 Timotheo 5:23, Paulo anakuambia "Usinywe maji tu, bali tumia mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lako!"..

Yaani hapa ndipo mtego wa Wazungu uliponasa akili zenu mazima. Mungu anageuka kuwa kinyonga asubuhi anasema hivi, jioni anageuka kule, halafu ninyi mnasimama madhabahuni na kusema Bwana asifiwe! Asifiwe kwa lipi? Kwa kuwavuruga akili?...

Hebu tazameni huu usanii mwingine Biblia inakuambia kwenye Wagalatia 2:16 kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali ni kwa imani tu.
Yaani, hata uwe jambazi vipi, ukiamini tu basi milango ya mbinguni iko wazi!.....

Lakini kabla hujakaa sawa, mwandishi mwingine anakuja juu kwenye Yakobo 2:24 anasema, "Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa haki kwa matendo, wala si kwa imani peke yake."

Sasa mnataka kutuambia nini? Huyo Mungu wenu ana matatizo ya kusahau au alikuwa anajikata kauli mwenyewe? Huku mnaambiwa "fanya kazi upate thawabu," huku mnaambiwa "kazi ni bure, amini tu.

Mtu anajiishi anavyotaka akitegemea "neema," huku mwingine anajitesa kwa sheria akitegemea "matendo," na wote wanatumia kitabu kimoja! Huu ni uwendawazimu wa hali ya juu! Yani hapa Wazungu walipokuwa wakiandika hiki kitabu walituvuruga sana, hawakwenda direct kama Waarabu..

Wazungu wanawaimbisha kila siku "Mungu ni upendo," "Mungu ni mwema." Haya, fungueni hiyo Biblia yenu muone ukatili uliopindukia!

Kwenye 1 Samweli 15:3, huyo anayeitwa Mungu anatoa amri ya kikatili: "Nenda ukawapige Waamaleki... uwaue mwanamume na mwanamke, mtoto mchanga na anyoyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda."

Hivi huyu ndiye Mungu mnavyotuaminisha ana huruma? Mtoto mchanga anayeuawa ana kosa gani? Halafu dakika mbili mbele, anawaambia "Usiue." Huu ni ulingo wa machafuko! Leo anasema penda adui yako, kesho anasema fyeka hata watoto wachanga. Kama huu siyo mkanganyiko wa akili, basi ni nini?...

Mababu zetu walijua kuna Muumba mmoja, na huyo Muumba hakuleta vitabu vya kuwafanya watu wapigane mapanga eti kwa sababu huyu amekula nguruwe au yule amesali Jumamosi.

Kwetu, Mungu alionekana kwenye matendo, kwenye mvua, kwenye ardhi, na kwenye uhai hakuwa mungu wa nadharia zinazopingana!....
Mungu ambaye Mo29 watu walichinjwa akiwa anaona ni Mungu wa ajabu sana
 
Mi ninachojua MUNGU yupo.

Amri kumi zipo na zinajidhihirisha zenyewe.

Katika zote amri kuu ni UPENDO.

hayo mambo mengine yoooooooooooteee yapo hapo kwenye herufi kubwa hiii ya mwisho baaasi.
 
Kuna mwandish mzungu kwenye biblia? au mm nashndwa kuelewa mzungu ni nani na jews ni nani
 
Been learning about Islam lately
:2Head:

1) Jesus is just a Messenger 😂

View: https://youtube.com/shorts/7YYzgMQj3OM?si=5sQsZ2Yqy-07mTq4


2) Jesus spoke of Muhammad 😂


View: https://youtube.com/shorts/A7F3_AytauI?si=I5CQfxBtYMrtm_cb


3) Islam is a religion on peace 😂


View: https://youtube.com/shorts/5yVfDAn5hlE?si=EGImSQ_Q8LRZi_17


4) Muhammad is the first Muslim 😂

View: https://youtube.com/shorts/sWlP1X78b3w?si=9s3QoAINUDcCP07c


5) The Quran is a clear book 😂


View: https://youtube.com/shorts/cswsidQf9vY?si=fD1b87xExQuV1_4f


6) The Quran is Confirming the scriptures 😂

View: https://youtube.com/shorts/4pHRYWZviAc?si=wehIdCNlg8O9ivHU


7) Islam respects women the most 😂


View: https://youtube.com/shorts/HcIDNzfX4sY?si=1ZGnNqPoa3zSL


8) The Quran came to correct the Torah and the Bible 😂


View: https://youtube.com/shorts/51YXg0F91I0?si=dnBwHL2OXGLd2Xol


9) The Heavens and Earth were created in how many days? 😂


View: https://youtube.com/shorts/7JvVVxg5wG0?si=5Up3wcZWLRS3JB5w


10) Is JESUS the Truth, The First and The Last? 😂


View: https://youtube.com/shorts/B3nwkIRXY3k?si=RUX_knmOGTNwStl7


11) Who is coming with angels on Judgment Day? 😂


View: https://youtube.com/shorts/VOPfYgKY90I?si=Dwq66s1JUu7rACLA


12) Are we mistakenly comparing the Bible to the Quran? Who is going to raise the dead? 😂


View: https://youtube.com/shorts/emybUPY7994?si=U5ophOG1WlsBd_6E

Hapa mtoa mada ameongelea Biblia sidhani kama ametaja Qur’an
 
Geukia upande wa pili uone wenzenu walivyojipanga. Kurani haina hizi sarakasi za kijinga!.
Kwenye kitabu cha Waarabu, sheria ni msumeno inakata pande zote! Hakuna cha tajiri, hakuna cha maskini, hakuna cha nabii wa uongo wa kujitungia tafsiri.
Kimepangika, kimeeleweka, na hakihitaji upako wa ziada kuelewa kuwa dhambi ni dhambi!..
Al-mukheef
 
BIBLIA ni Kitabu cha Historia ya Ulimwengu huu.

Ukweli wa ulimwengu huu.

1000055548.jpg



Vitabu 66. Waandishi 40. Miaka 1,500.

Lakini ni simulizi moja, sauti moja, ujumbe mmoja!

Hakuna kitabu kingine duniani kinachofanana na hiki! HAKUNA!

Miunganiko hii 63,779 si jambo la ustadi wa kawaida tu! Haiwezekani kuratibiwa kwa usahihi huo wote! ! ! !

Isipokuwa kama Mwandishi wake ni Mungu Mwenyewe.
1000055546.jpg




Hii si sanaa! ! Ni ramani ya kuona ya Biblia.

Kila mstari ulio chini unawakilisha sura moja.

Kadiri mstari unavyokuwa mrefu, ndivyo sura hiyo inavyounganishwa na mistari mingi zaidi!

Mikunjo iliyo juu inaunganisha mistari ya Biblia kupitia unabii, ishara, au mada zinazofanana.

Rangi zinaonyesha umbali kati ya mistari inayounganishwa: Rangi za baridi zinaonyesha mistari iliyo karibu, Rangi za joto zinaonyesha mistari iliyo mbali zaidi.


Unachokiona si jambo la bahati nasibu.

Ni alama ya kipekee ya Mwandishi wa Kimungu.

1000055547.jpg
 
Je Hayo yote yanabadilisha kuwa mwanamume aitwaye YESU:

aliishi karne ya kwanza,
alifanya miujiza,
aliteswa,
akauawa na wasiomuamini,
akafufuka siku ya tatu,
akatokea mamia kwa siku 40?

Bila kusahau kulikuwa na unabii wa matukio zaidi ya 300 ambayo angefanya kwenye maisha yake, ambayo yaliandikwa mamia ya miaka kabla hajazaliwa?

Post in thread 'Hivi Kuna ushahidi wowote Yesu alikuja duniani or it's just a conspiracy theory ya watunga stori?' Hivi Kuna ushahidi wowote Yesu alikuja duniani or it's just a conspiracy theory ya watunga stori?

Je, si jambo la busara kuuliza ni nani hasa aliyerekodi si tu mojawapo ya sala za mwisho za huyo mtu-mungu, bali pia tukio la mwisho ambapo huyo shujaa mkuu aliyehai alikuwa pamoja na wafuasi wake?

Mashahidi pekee walikuwa wamelala.‘Naye akasema, “Aba, Baba, yote yanawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; lakini si nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.”

Akaja akawakuta wamelala, akamwambia Petro, “Simoni, umelala?

Hukuweza kukesha saa moja?

Kesheni na kuomba msije mkaingia majaribuni. Roho iko tayari, lakini mwili ni dhaifu.

”Akaenda tena akaomba, akisema maneno yaleyale.

Aliporudi, akawakuta tena wamelala, kwa maana macho yao yalikuwa mazito; wala hawakujua la kumjibu.

Akaja mara ya tatu, akawaambia, “Endeleeni kulala na kupumzika; imetosha. Saa imefika; tazama, Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwa wenye dhambi.”– Marko 14:36-41 (toleo la Mathayo linafanana karibu kabisa; Luka amelifupisha, na Yohana ameacha kabisa tukio hili.)

Lakini bila shaka, kama tamthilia takatifu – fabula praetexta – mizunguko hiyo ya kwenda na kurudi pamoja na hotuba za kishairi kwa hadhira ni hasa kile tunachotarajia.

Kinakufanya ufikiri.

Vipengele vingi vya simulizi la “Mateso” (Passion) havina mantiki kihistoria.

Kwa nini Yesu afanyiwe kesi, ilhali washukiwa wa uasi walikuwa wakikamatwa na kuuawa na Warumi bila kesi?

Philo wa Alexandria (On the Embassy to Gaius, XXXVIII) anazungumzia ‘mauaji ya daima ya Pilato dhidi ya watu ambao hawakuhukumiwa wala kushtakiwa rasmi.’

Na kwa nini Warumi wangemruhusu mhalifu aliyepatikana na hatia kushushwa karibu mara moja kutoka msalabani na kuwekwa kaburini?

Kusulubishwa kulichaguliwa hasa ili kutoa ujumbe wa hadharani kwamba adhabu ya kikatili na ya kudhalilisha zaidi inawasubiri wale wanaopinga mamlaka ya Roma.

Mtazamo wa Warumi kuhusu jambo hili labda umeelezwa vizuri zaidi na Quintilian (BK 35–95, Decl. 274) aliposema:“Kila tunapowasulubisha wenye hatia, tunachagua barabara zenye watu wengi zaidi, ili watu wengi waone na waingiwe na hofu hii.

Kwa maana adhabu hazihusiani sana na kulipiza kisasi bali na athari yake ya kuwa mfano kwa wengine.

”Karne moja kabla ya hapo, baada ya ‘uasi wa watumwa’ ulioongozwa na Spartacus, wafungwa 6,000 walisulubishwa kando ya Via Appia kati ya miji ya Roma na Capua, kama onyo la kutisha dhidi ya maasi mengine.

Bila shaka maiti hizo ziliachwa msalabani zioze au ziwe chakula cha wanyama wakali na ndege .

Lakini ikiwa simulizi la “Mateso” lilikuwa kweli tamasha la mungu wa jua anayezaliwa upya, basi inaeleweka kikamilifu kwa nini mhusika ‘aliyetolewa dhabihu’ angeondolewa jukwaani na baadaye kuonekana tena katika sehemu inayofuata ya tamthilia, akiwa ‘amezaliwa upya’...
 
Maandiko yanayodaiwa kwamba ni ya Mungu ni mengi sana.

Kuna Biblia ya wakristo.

Kuna Quran ya waislamu.

Kuna Torah ya wayahudi.

Kuna Tripitaka ya wabudha.

Kuna The Vedas ya wahindu.

Kuna The Kojik ya washinto kule Japan.

Kuna The Guru Granth Sahib ya wasikhism.

Kuna Rastafar Bible ya Rastafarians.

Kila muumini wa vitabu hivi aamini kwamba KITABU chake pekee ndicho neno la Mungu. Na maandiko ya vitabu vingine sio ya Mungu.

Sasa Mungu mmoja hawezi kuwa na maandiko mengi yanayo tofautiana maelezo.

Mungu huyo angelikuwepo, kungelikuwa na KITABU kimoja tu, kwa watu wote ulimwenguni wote.

Mungu hayupo, Ni binadamu tu waliandika hadithi zao uchwara kwenye vitabu na kuanza kuita Neno la Mungu.

If human beings can build a house and call it, the house of God. They can also write a book 📖 and call it, the word of God.

Hakuna Mungu.

Hakuna Neno la Mungu.

Kuna vitabu vilivyoandikwa na wanadamu kama sisi, vinavyoitwa neno la Mungu. Ambavyo havina ukweli wowote ule. Ni hadithi na hekaya tu.

Ni kweli kwamba duniani kuna vitabu vingi vya dini, lakini wingi wa madai hauonyeshi kwamba madai yote ni ya kweli au yote ni ya uongo. Kama ilivyo katika sayansi, kuwepo kwa nadharia nyingi hakumaanishi kwamba hakuna nadharia sahihi.

Kwa mtazamo wa Uislamu, Qur'an haitambulishwi kuwa ya Mungu kwa sababu tu Waislamu wanaamini hivyo, bali kwa sababu inatoa ushahidi wake yenyewe:

Qur'an ilihifadhiwa kwa lugha yake ya asili tangu ilipoteremshwa. Mamilioni ya watu wameihifadhi kwa kukariri kizazi baada ya kizazi, na maandishi yake yamebaki bila matoleo yanayopingana katika msingi wa matini wake.

Qur'an ilitoa changamoto kwa watu walete sura moja mfano wake ikiwa ni maneno ya mwanadamu (Qur'an 2:23; 10:38).

Mtume Muhammad ﷺ alikuwa hajulikani kama mwandishi, mshairi au msomi wa maandiko, lakini alileta kitabu chenye mfumo wa kipekee wa lugha, sheria, maadili na mafundisho ya tauhidi.

Qur'an inawathibitisha manabii waliotangulia kama Ibrahim, Musa na Isa (Yesu) na kufundisha ujumbe mmoja wa kumuabudu Mungu Mmoja.

Tofauti na maandiko mengi ya kale, Qur'an inadai waziwazi kwamba Mungu mwenyewe ndiye atakayeilinda:
“Hakika Sisi ndio tulioteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakaoulinda.” (Qur'an 15:9)

Kwa hiyo Mwislamu hasemi “Qur'an ni ya Mungu kwa sababu nimezaliwa katika Uislamu.” Hoja yake ni kwamba baada ya kuchunguza madai ya vitabu mbalimbali, Qur'an ina ushahidi wa kihistoria, uhifadhi wa matini, na ujumbe wa tauhidi unaoifanya isimame tofauti na vitabu vingine.

Bila shaka kila mtu ana haki ya kuchunguza ushahidi huo na kufikia hitimisho lake mwenyewe.
 
BIBLIA ni Kitabu cha Historia ya Ulimwengu huu.

Ukweli wa ulimwengu huu.

View attachment 3599523


Vitabu 66. Waandishi 40. Miaka 1,500.

Lakini ni simulizi moja, sauti moja, ujumbe mmoja!

Hakuna kitabu kingine duniani kinachofanana na hiki! HAKUNA!

Miunganiko hii 63,779 si jambo la ustadi wa kawaida tu! Haiwezekani kuratibiwa kwa usahihi huo wote! ! ! !

Isipokuwa kama Mwandishi wake ni Mungu Mwenyewe.
View attachment 3599524



Hii si sanaa! ! Ni ramani ya kuona ya Biblia.

Kila mstari ulio chini unawakilisha sura moja.

Kadiri mstari unavyokuwa mrefu, ndivyo sura hiyo inavyounganishwa na mistari mingi zaidi!

Mikunjo iliyo juu inaunganisha mistari ya Biblia kupitia unabii, ishara, au mada zinazofanana.

Rangi zinaonyesha umbali kati ya mistari inayounganishwa: Rangi za baridi zinaonyesha mistari iliyo karibu, Rangi za joto zinaonyesha mistari iliyo mbali zaidi.


Unachokiona si jambo la bahati nasibu.

Ni alama ya kipekee ya Mwandishi wa Kimungu.

View attachment 3599527



 
hivi unajua sababu kwanza ya kuwepo agao jipya na la kale kwenye biblia?
Biblia Ina vitabu 73 agano la kale lina vitabu 46 pamoja na vitabu 7 vya deuterokanoni na maudhui ya ziada ya deuterokanoniki katika vitabu 2 agano jipya Lina vitabu 27 ili uilewe DINI ni lazima ujifunze fasihi teule ya uandishi Kisha theolojia level 1-7, ili uilewe theolojia ni lazima ujifunze falsafa, ili uielewe falsafa ni lazima ujifunze saikolojia na ili uisimike DINI ni lazima utumie saikolojia pumbazi a.k.a ujasusi wa vita ya akili na hisia baada ya kufundishwa Kitu kiitwacho mantic, sayansi ya lugha, historia ya Dini, utawala + occultism (elimu ya siri hii ni kwa viongozi wa juu katika DINI/forbidden knowledge) mtu huyu anakuwa kwenye level ya 7 ya walimwengu hivyo utambuzi wake ni tofauti na mbumbumbu ambaye akiambiwa habari ya bustani ya Eden ama Yesu alizaliwa bila sex ama alipaa anachukua kama ilivyo😁 Ila hawa wabobezi ndio wanakuwa mawakala wa kupotosha umati wa Dunia yetu wakihakikishiwa mkate/good life.
hivi unajua sababu kwanza ya kuwepo agao jipya na la kale kwenye biblia?
 
Mtoa post
Inaonekana unaiamini quaran sana na unaamini haina mkanganyo

Soma quaran 19:1
Njoo utuambie maana yake ili tujue kuwa quaran ya mudy mwarabu imenyooka.
Sijasema kama quaran imenyooka 100% na sio kwamba nipo upande huo, sipo upande wowote katika hizo DINI mbili kubwa isipokuwa hoja yangu ilimaanisha angalau quaran Ina unafuu kimaandiko Ila tukirudi kwenye mada kwamba vitabu vya Mungu sijui DINI imeletwa na Mungu vyote vinapotosha Mungu hana Dini wala kitabu.
 
Back
Top Bottom