Biblia: Kitabu cha Mkanganyiko au Neno la Mungu?

Ndiyo maana mimi nimekomaa na Korani tu. Yenyewe imenyoka bila mikanganyiko yo yote. Na imeshushwa kutoka mbinguni na kupokelewa na mtu mmoja tu tena asiyejua kusoma wala kuandika. Kitabu cha maajabu sana. Kitabu cha kweli. Kitabu cha Allah!
 
Kwani mtoa mada haupendi mafundisho mazuri ya kwenye Biblia ?
Kama hili

Mathayo (Mat) 19:19

Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Honour thy father and thy mother: and, Thou shalt love thy neighbour as thyself.
 
Mungu ambaye Mo29 watu walichinjwa akiwa anaona ni Mungu wa ajabu sana
 
Mi ninachojua MUNGU yupo.

Amri kumi zipo na zinajidhihirisha zenyewe.

Katika zote amri kuu ni UPENDO.

hayo mambo mengine yoooooooooooteee yapo hapo kwenye herufi kubwa hiii ya mwisho baaasi.
 
Kuna mwandish mzungu kwenye biblia? au mm nashndwa kuelewa mzungu ni nani na jews ni nani
 
Hapa mtoa mada ameongelea Biblia sidhani kama ametaja Qur’an
 
Al-mukheef
 
BIBLIA ni Kitabu cha Historia ya Ulimwengu huu.

Ukweli wa ulimwengu huu.




Vitabu 66. Waandishi 40. Miaka 1,500.

Lakini ni simulizi moja, sauti moja, ujumbe mmoja!

Hakuna kitabu kingine duniani kinachofanana na hiki! HAKUNA!

Miunganiko hii 63,779 si jambo la ustadi wa kawaida tu! Haiwezekani kuratibiwa kwa usahihi huo wote! ! ! !

Isipokuwa kama Mwandishi wake ni Mungu Mwenyewe.




Hii si sanaa! ! Ni ramani ya kuona ya Biblia.

Kila mstari ulio chini unawakilisha sura moja.

Kadiri mstari unavyokuwa mrefu, ndivyo sura hiyo inavyounganishwa na mistari mingi zaidi!

Mikunjo iliyo juu inaunganisha mistari ya Biblia kupitia unabii, ishara, au mada zinazofanana.

Rangi zinaonyesha umbali kati ya mistari inayounganishwa: Rangi za baridi zinaonyesha mistari iliyo karibu, Rangi za joto zinaonyesha mistari iliyo mbali zaidi.


Unachokiona si jambo la bahati nasibu.

Ni alama ya kipekee ya Mwandishi wa Kimungu.

 

Je, si jambo la busara kuuliza ni nani hasa aliyerekodi si tu mojawapo ya sala za mwisho za huyo mtu-mungu, bali pia tukio la mwisho ambapo huyo shujaa mkuu aliyehai alikuwa pamoja na wafuasi wake?

Mashahidi pekee walikuwa wamelala.‘Naye akasema, “Aba, Baba, yote yanawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; lakini si nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.”

Akaja akawakuta wamelala, akamwambia Petro, “Simoni, umelala?

Hukuweza kukesha saa moja?

Kesheni na kuomba msije mkaingia majaribuni. Roho iko tayari, lakini mwili ni dhaifu.

”Akaenda tena akaomba, akisema maneno yaleyale.

Aliporudi, akawakuta tena wamelala, kwa maana macho yao yalikuwa mazito; wala hawakujua la kumjibu.

Akaja mara ya tatu, akawaambia, “Endeleeni kulala na kupumzika; imetosha. Saa imefika; tazama, Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwa wenye dhambi.”– Marko 14:36-41 (toleo la Mathayo linafanana karibu kabisa; Luka amelifupisha, na Yohana ameacha kabisa tukio hili.)

Lakini bila shaka, kama tamthilia takatifu – fabula praetexta – mizunguko hiyo ya kwenda na kurudi pamoja na hotuba za kishairi kwa hadhira ni hasa kile tunachotarajia.

Kinakufanya ufikiri.

Vipengele vingi vya simulizi la “Mateso” (Passion) havina mantiki kihistoria.

Kwa nini Yesu afanyiwe kesi, ilhali washukiwa wa uasi walikuwa wakikamatwa na kuuawa na Warumi bila kesi?

Philo wa Alexandria (On the Embassy to Gaius, XXXVIII) anazungumzia ‘mauaji ya daima ya Pilato dhidi ya watu ambao hawakuhukumiwa wala kushtakiwa rasmi.’

Na kwa nini Warumi wangemruhusu mhalifu aliyepatikana na hatia kushushwa karibu mara moja kutoka msalabani na kuwekwa kaburini?

Kusulubishwa kulichaguliwa hasa ili kutoa ujumbe wa hadharani kwamba adhabu ya kikatili na ya kudhalilisha zaidi inawasubiri wale wanaopinga mamlaka ya Roma.

Mtazamo wa Warumi kuhusu jambo hili labda umeelezwa vizuri zaidi na Quintilian (BK 35–95, Decl. 274) aliposema:“Kila tunapowasulubisha wenye hatia, tunachagua barabara zenye watu wengi zaidi, ili watu wengi waone na waingiwe na hofu hii.

Kwa maana adhabu hazihusiani sana na kulipiza kisasi bali na athari yake ya kuwa mfano kwa wengine.

”Karne moja kabla ya hapo, baada ya ‘uasi wa watumwa’ ulioongozwa na Spartacus, wafungwa 6,000 walisulubishwa kando ya Via Appia kati ya miji ya Roma na Capua, kama onyo la kutisha dhidi ya maasi mengine.

Bila shaka maiti hizo ziliachwa msalabani zioze au ziwe chakula cha wanyama wakali na ndege .

Lakini ikiwa simulizi la “Mateso” lilikuwa kweli tamasha la mungu wa jua anayezaliwa upya, basi inaeleweka kikamilifu kwa nini mhusika ‘aliyetolewa dhabihu’ angeondolewa jukwaani na baadaye kuonekana tena katika sehemu inayofuata ya tamthilia, akiwa ‘amezaliwa upya’...
 

Ni kweli kwamba duniani kuna vitabu vingi vya dini, lakini wingi wa madai hauonyeshi kwamba madai yote ni ya kweli au yote ni ya uongo. Kama ilivyo katika sayansi, kuwepo kwa nadharia nyingi hakumaanishi kwamba hakuna nadharia sahihi.

Kwa mtazamo wa Uislamu, Qur'an haitambulishwi kuwa ya Mungu kwa sababu tu Waislamu wanaamini hivyo, bali kwa sababu inatoa ushahidi wake yenyewe:

Qur'an ilihifadhiwa kwa lugha yake ya asili tangu ilipoteremshwa. Mamilioni ya watu wameihifadhi kwa kukariri kizazi baada ya kizazi, na maandishi yake yamebaki bila matoleo yanayopingana katika msingi wa matini wake.

Qur'an ilitoa changamoto kwa watu walete sura moja mfano wake ikiwa ni maneno ya mwanadamu (Qur'an 2:23; 10:38).

Mtume Muhammad ﷺ alikuwa hajulikani kama mwandishi, mshairi au msomi wa maandiko, lakini alileta kitabu chenye mfumo wa kipekee wa lugha, sheria, maadili na mafundisho ya tauhidi.

Qur'an inawathibitisha manabii waliotangulia kama Ibrahim, Musa na Isa (Yesu) na kufundisha ujumbe mmoja wa kumuabudu Mungu Mmoja.

Tofauti na maandiko mengi ya kale, Qur'an inadai waziwazi kwamba Mungu mwenyewe ndiye atakayeilinda:
“Hakika Sisi ndio tulioteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakaoulinda.” (Qur'an 15:9)

Kwa hiyo Mwislamu hasemi “Qur'an ni ya Mungu kwa sababu nimezaliwa katika Uislamu.” Hoja yake ni kwamba baada ya kuchunguza madai ya vitabu mbalimbali, Qur'an ina ushahidi wa kihistoria, uhifadhi wa matini, na ujumbe wa tauhidi unaoifanya isimame tofauti na vitabu vingine.

Bila shaka kila mtu ana haki ya kuchunguza ushahidi huo na kufikia hitimisho lake mwenyewe.
 



Your browser is not able to display this video.
 
hivi unajua sababu kwanza ya kuwepo agao jipya na la kale kwenye biblia?
Biblia Ina vitabu 73 agano la kale lina vitabu 46 pamoja na vitabu 7 vya deuterokanoni na maudhui ya ziada ya deuterokanoniki katika vitabu 2 agano jipya Lina vitabu 27 ili uilewe DINI ni lazima ujifunze fasihi teule ya uandishi Kisha theolojia level 1-7, ili uilewe theolojia ni lazima ujifunze falsafa, ili uielewe falsafa ni lazima ujifunze saikolojia na ili uisimike DINI ni lazima utumie saikolojia pumbazi a.k.a ujasusi wa vita ya akili na hisia baada ya kufundishwa Kitu kiitwacho mantic, sayansi ya lugha, historia ya Dini, utawala + occultism (elimu ya siri hii ni kwa viongozi wa juu katika DINI/forbidden knowledge) mtu huyu anakuwa kwenye level ya 7 ya walimwengu hivyo utambuzi wake ni tofauti na mbumbumbu ambaye akiambiwa habari ya bustani ya Eden ama Yesu alizaliwa bila sex ama alipaa anachukua kama ilivyo😁 Ila hawa wabobezi ndio wanakuwa mawakala wa kupotosha umati wa Dunia yetu wakihakikishiwa mkate/good life.
hivi unajua sababu kwanza ya kuwepo agao jipya na la kale kwenye biblia?
 
Mtoa post
Inaonekana unaiamini quaran sana na unaamini haina mkanganyo

Soma quaran 19:1
Njoo utuambie maana yake ili tujue kuwa quaran ya mudy mwarabu imenyooka.
Sijasema kama quaran imenyooka 100% na sio kwamba nipo upande huo, sipo upande wowote katika hizo DINI mbili kubwa isipokuwa hoja yangu ilimaanisha angalau quaran Ina unafuu kimaandiko Ila tukirudi kwenye mada kwamba vitabu vya Mungu sijui DINI imeletwa na Mungu vyote vinapotosha Mungu hana Dini wala kitabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…