Biblia Mwanzo 4: Kwa nini Kaini baada ya kumuua Abel, aliogopa watu wengine watamuua, hao watu ni kina nani?

Biblia Mwanzo 4: Kwa nini Kaini baada ya kumuua Abel, aliogopa watu wengine watamuua, hao watu ni kina nani?

watoto wengine wa Adam ni wadogo kwa Cain,hata Kama walizaa na hao watoto kuolewa na Cain,bado si kweli ukizingatia umri,na Cain anaongea wakati uliopo ambao Adam hakuwa na watoto wengine
Tayari Adamu alikuwa na watoto wengine ukiacha Cain na Abel

Hawa wadogo zake wangeweza kumuua kwa sababu ya kumuua ndugu yao Abel

Miaka ya zamani watu walikuwa wanaishi mpaka miaka 800

Inawezekana tayari wadogo zake walikuwa watu wazima ambao wangeweza kumdhuru kaka yao
 
Maswali ya Vijana haya....! Na mimi nilikua namsumbua sana Mwalimu wangu wa Biblia Kanisani...!

Anyway....!
Ukweli ni kwamba kulikua na Watu wengine wakiishi kabla ya Eden, kabla ya Adam na Eva....!
Ila mpango wa Mungu juu ya kizazi kipya, kwa lengo moja ya kumwabudu yeye, ulianzia kwa Adam na Eva......!

NB.
Maandishi ya Biblia, Vitu vingi vya Kiroho kama fimbo ya Mussa na Vitu vya kufanana na hivyo, vilichukuliwa Israel na kupelekwa Rome - Italy kwa sababu ni wakati huo ndo Roman anatawala Dunia...!
So hata Biblia ilienda kuunganishwa huko Rome na kupatikana Biblia hii tunayotumia leo...!

Wale watu waliounganisha Biblia pamoja, pia kuna baadhi ya Mistari ikabidi waiondoe, kuna baadhi ya Vitabu ikabidi waviondoe....!
Kuna Vitabu vilikua vinaelezea namna ya kufanya Uchawi, na namna ya kutibu Uchawi, kwa Mafundisho ya Fallen Angels..

Hata Kisa cha Adam ni kama kimeanzia kati, kisa cha Adamu kilianzia mbali, ambapo Adam alioa Mwanamke wa kwanza toka kwenye Jamii ambayo Kaini anamwambia Mungu wakimuona watamuua, na yule Mwanamke alivyomtenda Adamu, Adam akaanza kumlilia Mungu juu ya Mwanamke aliyemtesa, kufanya Jeuri, kumsaliti waziwazi....!

Mungu ndo anamwambia Adam this time atamuumba Mwanamke wake kutoka katika Mifupa yake etc......!

Lengo la Biblia ni kuwafundisha Watu mambo ya rohoni, Wokovu na kumtegemea Mungu ili siku ya Hukumu watu waende Mbinguni...!

Mambo ya Uchawi na Story zingine ambazo zilipunguzwa hazikua na faida yoyote Kiroho....!
Hata sasa kuna Mijadala mbalimbali Wataalamu wa Sheria za Dini wakihoji uhalali wa Kitabu cha Wimbo ulio bora, ukionekana hauna Faida yoyote Kiroho, Ni Mfalme Suleimani enzi hizo akimwandikia Mpenzi wake na kumsifu jinsi alivyokua Mzuri etc...!

Kwangu mimi muhimu ni kwamba Yesu Kristo alikufa na kufufuka kwa ajiri yangu, na kwamba yeye ndo njia ya kweli na Uzima, bila yeye hakuna Mbingu..... Hilo ndo Muhimu, kuishi kadri ya Mafundisho yake....!

Habari za Watu waliotaka kumuua Kaini walitoka wapi, ama mke wa Kaini alitoka wapi, sio muhimu kuliko habari kutubu na kuiamini Injili kwa sababu ule Mwisho umekaribia sana...!
 
Bible xs walokore zinambo ya ajabu sana.
Msingi wa dini uko kuanzia mwanzo 1 inayoelezea uumbaji wa Mungu wa binadamu wa Kwanza.

Baada ya Adamu kuubwa, alipewa mke wake akamuita Eva, wakazaa watoto 2, mmoja Abeli mwingine Kaini.

Hao watoto mmoja akawa mkulima (Kaini) na mwingine Abel mfungaji. Mmoja, Abel akapata kibali machoni pake Bwana baada ya kua anamtolea dhabihu ya mwana kondoo alienona( sijui kwa nini Mungu anapenda vitu vinono) na mwingine akawa anatoa dhabihu ya mazao, bwana hakuyapenda. Hata wewe ungekubali, mwingine anakuletea nyama iliyonona mwingine anakuletea mihogo sijui viazi, magimbi, utampenda nani?

Msingi wa hoja yangu uko Mwanzo 4:12- 14 ambapo baada ya Kaini kumuua kaka yake Abeli, Mungu akamtimua Kaini kwenye ardhi aliyokua amewaweka na akamuagiza atoke kwenye eneo lake na kwenda huko kutangatanga.

Kaini akaomba kwamba akitimuliwa kwenye ardhi ile ya kwao akaenda kwenye ardhi nyingine huko nje kutangatanga itakua ni rahisi mtu yoyote yule kumuona na kumuua ama kumdhuru.

Mwanzo 4:15 Mungu anamuahidi Kaini yoyote atakaemfanyia jambo baya Kaini ataadhibiwa mara 7 na Mungu akaahidi kumuwekea alama maalum Kaini ili watu wengine huko nje wamtambue na wasije kumdhuru ama kumuua.

Swali langu linakuja, kama Adam ndio alikua binadamu wa Kwanza, Abel na Kaini ndio walikua watoto wa Adam pekee, Kaini akamuua kaka yake Abel akabaki mwenyewe, hao watu ambao Kaini alikua anahofu watamuua walitoka wapi?

Kumbuka aliefukuzwa Eden ni kaini tu. Na kaini baada ya kufukuzwa Eden akaenda huko kwenye kutangatanga akapata mke, wakazaa mtoto Enoch na kuendelea.

Je biblia inadanganya kuhusu binadamu wa kwanza hapa Duniani ama inajichanganya?
 
Kwa hiyo tusemeje sasa....hakuna Mungu?kama walikuwepo na haikuandikwa kama walikuwepo watu leo tukifahamu then ni kwa faida gani?

Yote yatadhihiri kwa kila mmoja wetu siku siyo nyingi,na hivi hata kufika 70 ni mtihani basi hamna haja ya kuumiza vichwa tungoje!
Kwa nini hawakuandikwa, lengo la kutokuwataja hao watu ilikua ni nini? Ni obvious kulikua na nia ovu, ill intent watu wengine waaminishwe kwamba binadamu wa kanza hii Dunia alikua adam na aliumbwa na Mungu, je hao wengine ambao hawakutajwa waliumbwa na nani?

Habari za Mungu ni hadithi tu kama hadithi nyingine, hazima maana yoyote, Mungu hayupo.
 
Kabla ya kuubwa kwa Adamu (na tuumbe mwanadamu kwa mfano wetu) walikuwepo viumbe wengine Duniani.

NI Adamu pekee ndiye alikuwa mwanadamu kwa kwamza aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu mwenyezi.
Hao wengine waliokuwepo waliumbwa na nani na kwa mfano wa nani? Walijiumba wenyewe?
 
Adam alikua binadamu wa kwanza na Sio mtu wa kwanza watu walikuwepo long time ago,

Bible Mwanzo inasema Bwana Mungu akapanda bustani Mashariki mwa Edeni
Nukuu 'mashariki mwa'
Ikiwa na maana Edeni ulikua mji wanamoishi watu ila Bwana Mungu akapanda bustani huko na kumuweka Adam,

Pili Cain alipomuua ndugu yake aliwekwa alama ili kila amuonaye asimuue means kuna wauaji huko yaani other people,
Pia next chapter jamaa anaenda kaa nchi ya NODI
(Land of Nod )
Sass jiulize watu walikua watatu hiyo nchi ya Nod waliishi nyau?😁
Nchi wanaishi watu na ndiko Cain alikopata mke akamuoa,
Ukienda next chapter utakuta Dunia haikukaliwa na Binadamu tu Kulikua na
Watu, Nephilim (giants),Na Wana wa Mungu wengi tu ambao baadae walizaa na wanadamu
Kumbuka kipindi hiki Dunia ilikua advanced kwenye science na Technology kuliko sasa na kazi zake zipo mpaka leo ukitaka kujua in deep juu ya maisha ya kale tafuta
THE CHRONICLES OF ANNUNAK

Utaupata uhalisia wa Haya mambo na balaa lake!
Hao other people waliumbwa na nani, ama walikua wamejiumba wenyewe?
 
Kuna kitu hakipo sawa, alieandika biblia hakuwa makini aliacha loopholes nyigi sana. Kaini na Abeli ndio uzao wa kwanza wa Adama na Eva, halafu nao wakazaa, walizaa na kina nani? Adam ndi kiumbe wa kwanza kwa mujibu wake na Eva ni ubavu wake.
 
Biblia zama za kale ilikuwa hairekodi watoto wa kike waliozaliwa, hivyo hata kaini alioa dada yake.
Kwa hiyo watu huko ambao wangemuua walikuwa ndugu zake mwenyewe.
 
Kuna kitu hakipo sawa, alieandika biblia hakuwa makini aliacha loopholes nyigi sana. Kaini na Abeli ndio uzao wa kwanza wa Adama na Eva, halafu nao wakazaa, walizaa na kina nani? Adam ndi kiumbe wa kwanza kwa mujibu wake na Eva ni ubavu wake.
Babu walizaa na dada zao
 
"Biblia iliandikwa kwa ajili ya watu wenye akili siyo wenye elimu " - Galileo Galilei .
 
Tayari Adamu alikuwa na watoto wengine ukiacha Cain na Abel

Hawa wadogo zake wangeweza kumuua kwa sababu ya kumuua ndugu yao Abel

Miaka ya zamani watu walikuwa wanaishi mpaka miaka 800

Inawezekana tayari wadogo zake walikuwa watu wazima ambao wangeweza kumdhuru kaka yao
Kumbuka aliefukuzwa Karibu na eneo salama(secured area) alikua ni Kaini ndio maana anasema Mungu ukiniondoa hapa kwenye eneo lako nitaenda huko kwa nchi nyingi watu wataniua.

Kwa maana kwamba huo uzao mwingine wa Adam haukuondolewa kwenye protected area, ni Kaini tu. Hivyo alieenda kutanga tanga ni kaini na sio hao wengine, kwa maana hiyo isingeweza yeye kukutana na watu wako kwenye protected area, ambao hawakufukuzwa, ambao hawakua na kosa lolote.

Hoja kwamba kaini alikua akihofia wadogo zake haona mantiki.
 
Hao other people waliumbwa na nani, ama walikua wamejiumba wenyewe?
Hao waliumbwa katika uumbaji wa Mwanzo kabla ya Adam wa Eden ,
Adam hakua binadamu wa kwanza walikuwepo wengine,
Ila yeye ndie aliwekwa Eden akawa wa kwanza kufanya ushirika na Mungu kumbuka Mpaka Adamu anaumbwa Dunia ilikua corrupted na race nyingine kutoka Galaxy za mbali kama Andromedan, Annunak (Nephilim) from Nibiru, Orion na mifumo mingine Mingi ya nyota hao wote wanaitwa Jeshi la Mbinguni walikuja Duniani mamilioni ya miaka iliyopita na walileta ustaraabu unaohusishwa Science na Teknolojia kubwa kiasi kwamba Earthers wakaanza corrupt DNA zao na hao viumbe na kuichafua Dunia,

Adam alikua second project na ndio maana Mungu akapanda bustani Mashariki mwa' Eden ili kumtenga na corrupted ila still aliharibu matokeo yake akafukuzwa Eden na kurudi nje kuendelea kujoin na wengine waliopotea,
Mkuu hii Dunia ina historia ya kutisha sana before and after Adam,
Usione wahindi,wachina,Wamisri,
wamaya ustaraabu wao wa kuabudu miungu ulikuja bahati mbaya hao waliabudu miungu inayoonekana live live na ndio iliyojenga ma historical sites ya ajabu ajabu kama Matemple ya mawe, Mapyramids na underground tunnels around the world nk
Hujawahi sikia conspiracy theory juu kizazi cha Reptilian kinachoishi Duniani kwa mamilioni ya miaka hapa Duniani?
Hao ndio mijusi wa kidrako kuna siri na vyama vya siri wanaujua ukweli ila unafunikwa na propaganda

Historical sites nyingi za kale hazikujengwa na Binadamu wa kawaida yaani Humanoid ila ni hao viumbe kazi yao!
 
Back
Top Bottom