Biblia Mwanzo 4: Kwa nini Kaini baada ya kumuua Abel, aliogopa watu wengine watamuua, hao watu ni kina nani?

Biblia Mwanzo 4: Kwa nini Kaini baada ya kumuua Abel, aliogopa watu wengine watamuua, hao watu ni kina nani?

Kwa nini hawakuandikwa, lengo la kutokuwataja hao watu ilikua ni nini? Ni obvious kulikua na nia ovu, ill intent watu wengine waaminishwe kwamba binadamu wa kanza hii Dunia alikua adam na aliumbwa na Mungu, je hao wengine ambao hawakutajwa waliumbwa na nani?

Habari za Mungu ni hadithi tu kama hadithi nyingine, hazima maana yoyote, Mungu hayupo.
Sawa walikuwepo watu kabla yao,pia sawa Mungu hayupo,tukiiweka hivi hii kutakuwa na tatizo lolote mkuu?
 
Msingi wa dini uko kuanzia mwanzo 1 inayoelezea uumbaji wa Mungu wa binadamu wa Kwanza.

Baada ya Adamu kuubwa, alipewa mke wake akamuita Eva, wakazaa watoto 2, mmoja Abeli mwingine Kaini.

Hao watoto mmoja akawa mkulima (Kaini) na mwingine Abel mfungaji. Mmoja, Abel akapata kibali machoni pake Bwana baada ya kua anamtolea dhabihu ya mwana kondoo alienona( sijui kwa nini Mungu anapenda vitu vinono) na mwingine akawa anatoa dhabihu ya mazao, bwana hakuyapenda. Hata wewe ungekubali, mwingine anakuletea nyama iliyonona mwingine anakuletea mihogo sijui viazi, magimbi, utampenda nani?

Msingi wa hoja yangu uko Mwanzo 4:12- 14 ambapo baada ya Kaini kumuua kaka yake Abeli, Mungu akamtimua Kaini kwenye ardhi aliyokua amewaweka na akamuagiza atoke kwenye eneo lake na kwenda huko kutangatanga.

Kaini akaomba kwamba akitimuliwa kwenye ardhi ile ya kwao akaenda kwenye ardhi nyingine huko nje kutangatanga itakua ni rahisi mtu yoyote yule kumuona na kumuua ama kumdhuru.

Mwanzo 4:15 Mungu anamuahidi Kaini yoyote atakaemfanyia jambo baya Kaini ataadhibiwa mara 7 na Mungu akaahidi kumuwekea alama maalum Kaini ili watu wengine huko nje wamtambue na wasije kumdhuru ama kumuua.

Swali langu linakuja, kama Adam ndio alikua binadamu wa Kwanza, Abel na Kaini ndio walikua watoto wa Adam pekee, Kaini akamuua kaka yake Abel akabaki mwenyewe, hao watu ambao Kaini alikua anahofu watamuua walitoka wapi?

Kumbuka aliefukuzwa Eden ni kaini tu. Na kaini baada ya kufukuzwa Eden akaenda huko kwenye kutangatanga akapata mke, wakazaa mtoto Enoch na kuendelea.

Je biblia inadanganya kuhusu binadamu wa kwanza hapa Duniani ama inajichanganya?
Kibiblia tunaweza sema, Adam alikua na watoto wengine ambao hawakutajwa coz walikua hawana role yoyote kwenye mtiririko wa maandiko hivyo hao pia walikua threat kwa Cain. Kumbuka zamani watu waliishi miaka mingi so kama cain alikua na miaka say 100 kuna possibility ya ndugu zake kuwa na 40s hivi so wangeweza kuwa threat kwake katika miji mingine.

Kihistoria tunasema Adam hakuwa mtu wa kwanza, maana upo ushahidi wa uwepo wa wanadamu kwa miaka zaidi ya elfu 6 inayotajwa kwenye biblia.

Kitheolojia tunasema Adam hakuwa binadamu wa kwanza bali alikua mtumishi/nabii/mtume etc wa kwanza wa Mungu. So kulikua na viumbe wengine ila Adam ndio alikua topameumbwa/tengenezwa/mentored kufanana na Mungu. So Adam alihofia hao viumbe/binadamu wengine wangemdhuru.

Na hoja ya kwamba kulikua na viumbe wengine tunaweza ona kwenye mwanzo 6 na kuendelea.

Further readings
Je, huu ni ukweli uliofichwa kwa miaka mingi?

Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu
 
1. Hoja ya kwanza Adam alikua na watoto wengine ambao hawakutajwa bado inabakia kua ni ya kihisia zaidi maana haijaandikwa popote. Basi tukubali alikua na watoto wengine. Lakini kaini hakua anawahofia hao watoto wengine kwa sababu wao bado alibakia kwenye eneo maalumu ama eneo tegemezi la Mungu, hawakufukuzwa.

Kaini alikua anahofia watu ambao angekutana nao baada ya kufukuzwa kutoka eneo tengwa la Mungu walipokua wakiishi. Kaini hakusema nikikaa hapa hawa wataniua, alisema nikienda huko hao wa huko wataniua.

Pia kwa mantiki ya mwandishi, kaini ndio mtoto wa Adam aliefanya kosa la mauaji na alikua akijua ni kosa, hao wengine wasingeweza kufanya kosa la kumuua Kaini kwani walikua wakijua kuua ni kosa na Mungu hapendi. Hivyo ndugu zake hawakua threat kabisa kwake.

2. Iwapo kulikua na watu wengine ambao wangemuua kaini, hao watu wengine walitoka wapi, waliumbwa na nani kama Adam ndio binadamu wa Kwanza kuumbwa?
 
Back
Top Bottom