Biblia Mwanzo 4: Kwa nini Kaini baada ya kumuua Abel, aliogopa watu wengine watamuua, hao watu ni kina nani?

watoto wengine wa Adam ni wadogo kwa Cain,hata Kama walizaa na hao watoto kuolewa na Cain,bado si kweli ukizingatia umri,na Cain anaongea wakati uliopo ambao Adam hakuwa na watoto wengine
Tayari Adamu alikuwa na watoto wengine ukiacha Cain na Abel

Hawa wadogo zake wangeweza kumuua kwa sababu ya kumuua ndugu yao Abel

Miaka ya zamani watu walikuwa wanaishi mpaka miaka 800

Inawezekana tayari wadogo zake walikuwa watu wazima ambao wangeweza kumdhuru kaka yao
 
Maswali ya Vijana haya....! Na mimi nilikua namsumbua sana Mwalimu wangu wa Biblia Kanisani...!

Anyway....!
Ukweli ni kwamba kulikua na Watu wengine wakiishi kabla ya Eden, kabla ya Adam na Eva....!
Ila mpango wa Mungu juu ya kizazi kipya, kwa lengo moja ya kumwabudu yeye, ulianzia kwa Adam na Eva......!

NB.
Maandishi ya Biblia, Vitu vingi vya Kiroho kama fimbo ya Mussa na Vitu vya kufanana na hivyo, vilichukuliwa Israel na kupelekwa Rome - Italy kwa sababu ni wakati huo ndo Roman anatawala Dunia...!
So hata Biblia ilienda kuunganishwa huko Rome na kupatikana Biblia hii tunayotumia leo...!

Wale watu waliounganisha Biblia pamoja, pia kuna baadhi ya Mistari ikabidi waiondoe, kuna baadhi ya Vitabu ikabidi waviondoe....!
Kuna Vitabu vilikua vinaelezea namna ya kufanya Uchawi, na namna ya kutibu Uchawi, kwa Mafundisho ya Fallen Angels..

Hata Kisa cha Adam ni kama kimeanzia kati, kisa cha Adamu kilianzia mbali, ambapo Adam alioa Mwanamke wa kwanza toka kwenye Jamii ambayo Kaini anamwambia Mungu wakimuona watamuua, na yule Mwanamke alivyomtenda Adamu, Adam akaanza kumlilia Mungu juu ya Mwanamke aliyemtesa, kufanya Jeuri, kumsaliti waziwazi....!

Mungu ndo anamwambia Adam this time atamuumba Mwanamke wake kutoka katika Mifupa yake etc......!

Lengo la Biblia ni kuwafundisha Watu mambo ya rohoni, Wokovu na kumtegemea Mungu ili siku ya Hukumu watu waende Mbinguni...!

Mambo ya Uchawi na Story zingine ambazo zilipunguzwa hazikua na faida yoyote Kiroho....!
Hata sasa kuna Mijadala mbalimbali Wataalamu wa Sheria za Dini wakihoji uhalali wa Kitabu cha Wimbo ulio bora, ukionekana hauna Faida yoyote Kiroho, Ni Mfalme Suleimani enzi hizo akimwandikia Mpenzi wake na kumsifu jinsi alivyokua Mzuri etc...!

Kwangu mimi muhimu ni kwamba Yesu Kristo alikufa na kufufuka kwa ajiri yangu, na kwamba yeye ndo njia ya kweli na Uzima, bila yeye hakuna Mbingu..... Hilo ndo Muhimu, kuishi kadri ya Mafundisho yake....!

Habari za Watu waliotaka kumuua Kaini walitoka wapi, ama mke wa Kaini alitoka wapi, sio muhimu kuliko habari kutubu na kuiamini Injili kwa sababu ule Mwisho umekaribia sana...!
 
Bible xs walokore zinambo ya ajabu sana.
 
Kwa nini hawakuandikwa, lengo la kutokuwataja hao watu ilikua ni nini? Ni obvious kulikua na nia ovu, ill intent watu wengine waaminishwe kwamba binadamu wa kanza hii Dunia alikua adam na aliumbwa na Mungu, je hao wengine ambao hawakutajwa waliumbwa na nani?

Habari za Mungu ni hadithi tu kama hadithi nyingine, hazima maana yoyote, Mungu hayupo.
 
Kabla ya kuubwa kwa Adamu (na tuumbe mwanadamu kwa mfano wetu) walikuwepo viumbe wengine Duniani.

NI Adamu pekee ndiye alikuwa mwanadamu kwa kwamza aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu mwenyezi.
Hao wengine waliokuwepo waliumbwa na nani na kwa mfano wa nani? Walijiumba wenyewe?
 
Hao other people waliumbwa na nani, ama walikua wamejiumba wenyewe?
 
Kuna kitu hakipo sawa, alieandika biblia hakuwa makini aliacha loopholes nyigi sana. Kaini na Abeli ndio uzao wa kwanza wa Adama na Eva, halafu nao wakazaa, walizaa na kina nani? Adam ndi kiumbe wa kwanza kwa mujibu wake na Eva ni ubavu wake.
 
Biblia zama za kale ilikuwa hairekodi watoto wa kike waliozaliwa, hivyo hata kaini alioa dada yake.
Kwa hiyo watu huko ambao wangemuua walikuwa ndugu zake mwenyewe.
 
Kuna kitu hakipo sawa, alieandika biblia hakuwa makini aliacha loopholes nyigi sana. Kaini na Abeli ndio uzao wa kwanza wa Adama na Eva, halafu nao wakazaa, walizaa na kina nani? Adam ndi kiumbe wa kwanza kwa mujibu wake na Eva ni ubavu wake.
Babu walizaa na dada zao
 
"Biblia iliandikwa kwa ajili ya watu wenye akili siyo wenye elimu " - Galileo Galilei .
 
Kumbuka aliefukuzwa Karibu na eneo salama(secured area) alikua ni Kaini ndio maana anasema Mungu ukiniondoa hapa kwenye eneo lako nitaenda huko kwa nchi nyingi watu wataniua.

Kwa maana kwamba huo uzao mwingine wa Adam haukuondolewa kwenye protected area, ni Kaini tu. Hivyo alieenda kutanga tanga ni kaini na sio hao wengine, kwa maana hiyo isingeweza yeye kukutana na watu wako kwenye protected area, ambao hawakufukuzwa, ambao hawakua na kosa lolote.

Hoja kwamba kaini alikua akihofia wadogo zake haona mantiki.
 
Hao other people waliumbwa na nani, ama walikua wamejiumba wenyewe?
Hao waliumbwa katika uumbaji wa Mwanzo kabla ya Adam wa Eden ,
Adam hakua binadamu wa kwanza walikuwepo wengine,
Ila yeye ndie aliwekwa Eden akawa wa kwanza kufanya ushirika na Mungu kumbuka Mpaka Adamu anaumbwa Dunia ilikua corrupted na race nyingine kutoka Galaxy za mbali kama Andromedan, Annunak (Nephilim) from Nibiru, Orion na mifumo mingine Mingi ya nyota hao wote wanaitwa Jeshi la Mbinguni walikuja Duniani mamilioni ya miaka iliyopita na walileta ustaraabu unaohusishwa Science na Teknolojia kubwa kiasi kwamba Earthers wakaanza corrupt DNA zao na hao viumbe na kuichafua Dunia,

Adam alikua second project na ndio maana Mungu akapanda bustani Mashariki mwa' Eden ili kumtenga na corrupted ila still aliharibu matokeo yake akafukuzwa Eden na kurudi nje kuendelea kujoin na wengine waliopotea,
Mkuu hii Dunia ina historia ya kutisha sana before and after Adam,
Usione wahindi,wachina,Wamisri,
wamaya ustaraabu wao wa kuabudu miungu ulikuja bahati mbaya hao waliabudu miungu inayoonekana live live na ndio iliyojenga ma historical sites ya ajabu ajabu kama Matemple ya mawe, Mapyramids na underground tunnels around the world nk
Hujawahi sikia conspiracy theory juu kizazi cha Reptilian kinachoishi Duniani kwa mamilioni ya miaka hapa Duniani?
Hao ndio mijusi wa kidrako kuna siri na vyama vya siri wanaujua ukweli ila unafunikwa na propaganda

Historical sites nyingi za kale hazikujengwa na Binadamu wa kawaida yaani Humanoid ila ni hao viumbe kazi yao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…