Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 3,114
- 6,309
Kila kona ya hiki kitabu ukikisoma vizuri utagundua kuna matatizo mengi mno ya kimantiki sasa sijui inatokea vipi mtu mdadisi, mwenye kufikiria kwa kina anakaa na kukubali tu kila neno lilipo binafsi naona ni kitabu ambacho kina stori tu na hamna kitu cha maana ukiangazia Dunia tuliyonayo Leo:
Kuna maswali machache hapa ningepenga kuyaacha kwa wanaoamini hiki kitabu:
Tukirudi katika mwanzo: Kama Mungu alijua kwa 100% kabla hajamuumba mwanadamu wa kwanza (Adam) au kabla hajakumba wewe na mimi kwamba tutatenda dhambi na hatimaye kwenda motoni, je, mwanadamu ana uhuru wa kweli wa kuchagua?
Kama Mungu alijua matokeo hayo yote bila shaka yoyote na bado akaamua kutuumba katika mfumo huo huo, maana yake matokeo hayo yalitengenezwa na Yeye kabla hata hatujazaliwa. Inakuwaje tena atuadhibu kwa makosa aliyotengeneza Mfumo utakaoyasababisha kabla hatujawepo?
2. Kama kifo na saratani vilikuwepo mamilioni ya miaka kabla ya mwanadamu kuwepo, inakuwaje Biblia iseme kifo na mateso yote yalisababishwa na dhambi ya mwanadamu? Je, Maandiko yanasimamia uhalisia gani?