Ni Wanawake yupi au Akina Nani Waliofika kaburini asubuhi ya ufufuo, na walimkuta nani kaburini?
Tukirudi na kulinganisha injili zote nne kuhusu asubuhi ya siku ya kwanza ya wiki pale kaburini, kuna migongano ya wazi katika walioenda, waliowakuta, na mambo yaliyotokea.
1: Hivi vifungu vinajibu nani Aliyekwenda Kaburini?
- Yohana 20:1 Ni Mariamm, Magdalena pekee ("siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalena alikwenda kaburini asubuhi bado kungali giza...").
- Mathayo 28:1 Walikuwa wanawake 2: Mariamu Magdalena na Mariamu yule mwingine.
- Marko 16:1 Walikuwa wanawake 3: Mariam, Magdalena, Mariamu mama yake Yakobo, na Salome.
- Luka 24:10 Walikuwa zaidi ya 4: Mariam, Magdalena, Yohana, Mariamu mama yake Yakobo, na "wengine waliokuwa pamoja nao".
2: Walimkuta Nani au kitu gani ndani au nje ya kaburi?
- Mathayo 28:2-5 Lilitokea tetemeko kubwa la ardhi, malaika mmoja alishuka kutoka mbinguni, akavingirisha jiwe, kisha akaketi juu ya lile jiwe nje ya kaburi.
- Marko 16:5 Hakuna tetemeko wala malaika aliyeketi juu ya jiwe nje. Ingawa waliingia ndani ya kaburi, walimkuta kijana mmoja ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe.
- Luka 24:4 Walipoingia ndani, walimkuta watu wawili malaika 2 wamesimama karibu nao, wenye mavazi ya kung'aa.
- Yohana 20:11-12 Mariam, Magdalena alikuwa peke yake nje akilia. Alipochungulia ndani ya kaburi, aliona malaika wawili wameketi, mmoja kichwani na mwingine miguuni pale ulipolazwa mwili wa yesu.
Kama shahidi wa kwanza anasema alikwenda mtu mmoja pekee na kukuta malaika mmoja ameketi juu ya jiwe nje. Na shahidi wa pili anasema walikwenda kundi la wanawake zaidi ya wanne na kukuta malaika wawili wakiwa wamesimama ndani
Maelezo haya mawili hayawezi kuwa sahihi yote kwa pamoja kimantiki.
Vilevile, Mathayo anadai jiwe lilivingirishwa mbele ya macho ya wale wanawake pale malaika aliposhuka na kusababisha tetemeko.
Marko, Luka, na Yohana wanadai wanawake hao walikuta jiwe limekwisha vingirishwa tayari kabla hawajafika.
Kama ufufuo wa Yesu ndilo tukio muhimu zaidi katika historia ya Ukristo, kwanini waandishi wote wanatofautiana kiasi hiki kwenye maelezo ya msingi kuhusu siku hiyo?