Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 3,114
- 6,309
Hehe! Taratibu tu mtafunguka, vitabu vya dini ukitafakari kwa kina utagundua madhaifu mengi sana!.
Shida watu wanavisoma vile vitabu huku wakiwa tayari wamelishwa vitu vya hovyo kichwani mwao hivyo wanaamini akitafari au aki judge sana basi anakufuru!!.
Ukiwa na akili ndogo huwezi kuielewa biblia.Kila kona ya hiki kitabu ukikisoma vizuri utagundua kuna matatizo mengi mno ya kimantiki sasa sijui inatokea vipi mtu mdadisi, mwenye kufikiria kwa kina anakaa na kukubali tu kila neno lilipo binafsi naona ni kitabu ambacho kina stori tu na hamna kitu cha maana ukiangazia Dunia tuliyonayo Leo:
Kuna maswali machache hapa ningepenga kuyaacha kwa wanaoamini hiki kitabu:
Tukirudi katika mwanzo: Kama Mungu alijua kwa 100% kabla hajamuumba mwanadamu wa kwanza (Adam) au kabla hajakumba wewe na mimi kwamba tutatenda dhambi na hatimaye kwenda motoni, je, mwanadamu ana uhuru wa kweli wa kuchagua?
Kama Mungu alijua matokeo hayo yote bila shaka yoyote na bado akaamua kutuumba katika mfumo huo huo, maana yake matokeo hayo yalitengenezwa na Yeye kabla hata hatujazaliwa. Inakuwaje tena atuadhibu kwa makosa aliyotengeneza Mfumo utakaoyasababisha kabla hatujawepo?
2. Kama kifo na saratani vilikuwepo mamilioni ya miaka kabla ya mwanadamu kuwepo, inakuwaje Biblia iseme kifo na mateso yote yalisababishwa na dhambi ya mwanadamu? Je, Maandiko yanasimamia uhalisia gani?
Ukiwa na akili ndogo huwezi kuielewa biblia.
Ukikichunguza sana unaweza hata kuquestion imani yako, Kuna mkanganyiko mkubwa sana wa kimantiki
Mkuu sasa naomba twende taratibu, kabla ya yote nikupongeze kwa ujasiri wako wa kuhoji na kutafuta majibu kwa kina. Imani ya Kikristo haigopi maswali; neno linasema, "Njoni sasa, tusemezane" (Isaya 1:18).
1. Kuhusu Uhuru wa Kuchagua (Free Will) na Kujua kwa Mungu (Omniscience)
Swali lako ni zuri sana: Kama Mungu anajua 100% kuwa fulani ataenda motoni, je, kuna uhuru wa kuchagua?
Kama Wainjilisti, tunatofautisha kati ya "Kujua mapema" (Foreknowledge) na "Kupangia mtu matokeo" (Predestination/Determinism). Kujua kwa Mungu hakuharibu uhuru wako wa kuchagua.
Mfano mwepesi, ukikaa ghorofani na kuona magari mawili yakija kwa kasi kwenye makutano ya barabara, unaweza kujua 100% kuwa yataigongana baada ya sekunde 5. Je, ujuzi wako ndio ulioyasababisha yagongane? Hapana. Dereva ana uhuru wa kukanyaga breki, lakini wewe unaona matokeo kabla hayajatokea kwa sababu uko juu yao. Mungu yuko nje ya muda (Time), anaona mwanzo na mwisho wetu, lakini bado anatuachia uamuzi mkononi mwetu.
Kuhusu Mfumo, Mungu hajatengeneza mfumo wa mwanadamu kufeli. Alitengeneza mfumo wa Upendo wa Kweli. Huwezi kuwa na upendo wa kweli bila uhuru wa kukataa. Kama Mungu angetuumba tusiweze kufanya dhambi, tusingekuwa wanadamu wenye utashi, tungekuwa "Roboti". Mungu alitaka viumbe wanaoweza kuchagua kumpenda. Adhabu haiji kwa sababu Mungu alitengeneza mfumo ufeli, bali inakuja kwa sababu mwanadamu anakataa mkono wa wokovu ambao Mungu ameweka wazi kwa kila mtu kupitia kwa Yesu Kristo (Yohana 3:16).
Kuhusu Kifo, Saratani (Cancer), na Historia ya Dunia Mamilioni ya Miaka Iliyopita
Hapa unagusa sayansi ya miamba na visukuku (Fossils) inayoonyesha uwepo wa magonjwa na vifo vya wanyama (kama dinosaurs) kabla ya Adamu. Maandiko yanaposimamia uhalisia, yanajibiwa kwa mitazamo miwili mikuu ya kiteolojia:
Kifo cha Kiroho na Uhusiano: Biblia inaposema “kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo kifo” (Warumi 5:12), inazungumzia hasa Kifo cha Kiroho cha mwanadamu (kutengwa na Mungu) na kuanza kwa uharibifu wa mwili wa mwanadamu aliyeumbwa kwa mfumo wa kuishi milele. Kifo kilicholetwa na dhambi ya Adamu ni kile kilichomnyonga mwanadamu, kiumbe pekee kilichopewa pumzi ya Mungu na utashi.
Dunia Iliyofanywa Upya (Creation/Re-creation): Wasomi wengi wa Maandiko wanaamini kuwa ulimwengu wa kibaolojia uliokuwepo kabla ya mwanadamu (mamilioni ya miaka) ulikuwa chini ya utaratibu wa asili wa kuzaliwa na kufa kwa viumbe visivyo na roho (wanyama na mimea). Adamu alipofanya dhambi, laana haikuishia kwake tu, bali iliharibu mfumo mzima wa mazingira yanayomzunguka mwanadamu (Mwanzo 3:17-18).
Kwahiyo biblia sio kitabu cha stori tu; ni maktaba inayobeba uhusiano wa Mungu na mwanadamu. Ukisoma kwa jicho la kutafuta "makosa ya kimantiki", utaona utata mwingi. Lakini ukisoma kwa jicho la kutafuta Moyo wa Mungu kwa mwanadamu, utagundua kuwa katika ulimwengu huu uliojaa maumivu, Biblia bado ndio dira pekee inayompa mwanadamu matumaini ya uzima wa milele na amani ya ndani inayopita akili zote.
Sisi Wakatoliki Walei tushaambiwa na tunaamini "The Word of God is Dogma"!Kila kona ya hiki kitabu ukikisoma vizuri utagundua kuna matatizo mengi mno ya kimantiki sasa sijui inatokea vipi mtu mdadisi, mwenye kufikiria kwa kina anakaa na kukubali tu kila neno lilipo binafsi naona ni kitabu ambacho kina stori tu na hamna kitu cha maana ukiangazia Dunia tuliyonayo Leo:
Kuna maswali machache hapa ningepenga kuyaacha kwa wanaoamini hiki kitabu:
Tukirudi katika mwanzo: Kama Mungu alijua kwa 100% kabla hajamuumba mwanadamu wa kwanza (Adam) au kabla hajakumba wewe na mimi kwamba tutatenda dhambi na hatimaye kwenda motoni, je, mwanadamu ana uhuru wa kweli wa kuchagua?
Kama Mungu alijua matokeo hayo yote bila shaka yoyote na bado akaamua kutuumba katika mfumo huo huo, maana yake matokeo hayo yalitengenezwa na Yeye kabla hata hatujazaliwa. Inakuwaje tena atuadhibu kwa makosa aliyotengeneza Mfumo utakaoyasababisha kabla hatujawepo?
2. Kama kifo na saratani vilikuwepo mamilioni ya miaka kabla ya mwanadamu kuwepo, inakuwaje Biblia iseme kifo na mateso yote yalisababishwa na dhambi ya mwanadamu? Je, Maandiko yanasimamia uhalisia gani?
Ndiyo maana watu wasioamini kuhusu dini wanazidi kuongezekaSana mkuu, no vile wakristo wanafundishwa kuitetea Biblia lakini ukisoma kwa makini Kuna matatizo ya wazi.
Mkuu sasa naomba twende taratibu, kabla ya yote nikupongeze kwa ujasiri wako wa kuhoji na kutafuta majibu kwa kina. Imani ya Kikristo haigopi maswali; neno linasema, "Njoni sasa, tusemezane" (Isaya 1:18).
1. Kuhusu Uhuru wa Kuchagua (Free Will) na Kujua kwa Mungu (Omniscience)
Swali lako ni zuri sana: Kama Mungu anajua 100% kuwa fulani ataenda motoni, je, kuna uhuru wa kuchagua?
Kama Wainjilisti, tunatofautisha kati ya "Kujua mapema" (Foreknowledge) na "Kupangia mtu matokeo" (Predestination/Determinism). Kujua kwa Mungu hakuharibu uhuru wako wa kuchagua.
Mfano mwepesi, ukikaa ghorofani na kuona magari mawili yakija kwa kasi kwenye makutano ya barabara, unaweza kujua 100% kuwa yataigongana baada ya sekunde 5. Je, ujuzi wako ndio ulioyasababisha yagongane? Hapana. Dereva ana uhuru wa kukanyaga breki, lakini wewe unaona matokeo kabla hayajatokea kwa sababu uko juu yao. Mungu yuko nje ya muda (Time), anaona mwanzo na mwisho wetu, lakini bado anatuachia uamuzi mkononi mwetu.
Kuhusu Mfumo, Mungu hajatengeneza mfumo wa mwanadamu kufeli. Alitengeneza mfumo wa Upendo wa Kweli. Huwezi kuwa na upendo wa kweli bila uhuru wa kukataa. Kama Mungu angetuumba tusiweze kufanya dhambi, tusingekuwa wanadamu wenye utashi, tungekuwa "Roboti". Mungu alitaka viumbe wanaoweza kuchagua kumpenda. Adhabu haiji kwa sababu Mungu alitengeneza mfumo ufeli, bali inakuja kwa sababu mwanadamu anakataa mkono wa wokovu ambao Mungu ameweka wazi kwa kila mtu kupitia kwa Yesu Kristo (Yohana 3:16).
Kuhusu Kifo, Saratani (Cancer), na Historia ya Dunia Mamilioni ya Miaka Iliyopita
Hapa unagusa sayansi ya miamba na visukuku (Fossils) inayoonyesha uwepo wa magonjwa na vifo vya wanyama (kama dinosaurs) kabla ya Adamu. Maandiko yanaposimamia uhalisia, yanajibiwa kwa mitazamo miwili mikuu ya kiteolojia:
Kifo cha Kiroho na Uhusiano: Biblia inaposema “kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo kifo” (Warumi 5:12), inazungumzia hasa Kifo cha Kiroho cha mwanadamu (kutengwa na Mungu) na kuanza kwa uharibifu wa mwili wa mwanadamu aliyeumbwa kwa mfumo wa kuishi milele. Kifo kilicholetwa na dhambi ya Adamu ni kile kilichomnyonga mwanadamu, kiumbe pekee kilichopewa pumzi ya Mungu na utashi.
Dunia Iliyofanywa Upya (Creation/Re-creation): Wasomi wengi wa Maandiko wanaamini kuwa ulimwengu wa kibaolojia uliokuwepo kabla ya mwanadamu (mamilioni ya miaka) ulikuwa chini ya utaratibu wa asili wa kuzaliwa na kufa kwa viumbe visivyo na roho (wanyama na mimea). Adamu alipofanya dhambi, laana haikuishia kwake tu, bali iliharibu mfumo mzima wa mazingira yanayomzunguka mwanadamu (Mwanzo 3:17-18).
Kwahiyo biblia sio kitabu cha stori tu; ni maktaba inayobeba uhusiano wa Mungu na mwanadamu. Ukisoma kwa jicho la kutafuta "makosa ya kimantiki", utaona utata mwingi. Lakini ukisoma kwa jicho la kutafuta Moyo wa Mungu kwa mwanadamu, utagundua kuwa katika ulimwengu huu uliojaa maumivu, Biblia bado ndio dira pekee inayompa mwanadamu matumaini ya uzima wa milele na amani ya ndani inayopita akili zote.
Jerome mwenyewe alikiri kwamba tafsiri ni kazi yenye changamoto, na wakati mwingine alichagua maana aliyodhani ndiyo inayofaa zaidi kimuktadha.Ni Wanawake yupi au Akina Nani Waliofika kaburini asubuhi ya ufufuo, na walimkuta nani kaburini?
Tukirudi na kulinganisha injili zote nne kuhusu asubuhi ya siku ya kwanza ya wiki pale kaburini, kuna migongano ya wazi katika walioenda, waliowakuta, na mambo yaliyotokea.
1: Hivi vifungu vinajibu nani Aliyekwenda Kaburini?
- Yohana 20:1 Ni Mariamm, Magdalena pekee ("siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalena alikwenda kaburini asubuhi bado kungali giza...").
- Mathayo 28:1 Walikuwa wanawake 2: Mariamu Magdalena na Mariamu yule mwingine.
- Marko 16:1 Walikuwa wanawake 3: Mariam, Magdalena, Mariamu mama yake Yakobo, na Salome.
- Luka 24:10 Walikuwa zaidi ya 4: Mariam, Magdalena, Yohana, Mariamu mama yake Yakobo, na "wengine waliokuwa pamoja nao".
2: Walimkuta Nani au kitu gani ndani au nje ya kaburi?
- Mathayo 28:2-5 Lilitokea tetemeko kubwa la ardhi, malaika mmoja alishuka kutoka mbinguni, akavingirisha jiwe, kisha akaketi juu ya lile jiwe nje ya kaburi.
- Marko 16:5 Hakuna tetemeko wala malaika aliyeketi juu ya jiwe nje. Ingawa waliingia ndani ya kaburi, walimkuta kijana mmoja ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe.
- Luka 24:4 Walipoingia ndani, walimkuta watu wawili malaika 2 wamesimama karibu nao, wenye mavazi ya kung'aa.
- Yohana 20:11-12 Mariam, Magdalena alikuwa peke yake nje akilia. Alipochungulia ndani ya kaburi, aliona malaika wawili wameketi, mmoja kichwani na mwingine miguuni pale ulipolazwa mwili wa yesu.
Kama shahidi wa kwanza anasema alikwenda mtu mmoja pekee na kukuta malaika mmoja ameketi juu ya jiwe nje. Na shahidi wa pili anasema walikwenda kundi la wanawake zaidi ya wanne na kukuta malaika wawili wakiwa wamesimama ndani
Maelezo haya mawili hayawezi kuwa sahihi yote kwa pamoja kimantiki.
Vilevile, Mathayo anadai jiwe lilivingirishwa mbele ya macho ya wale wanawake pale malaika aliposhuka na kusababisha tetemeko.
Marko, Luka, na Yohana wanadai wanawake hao walikuta jiwe limekwisha vingirishwa tayari kabla hawajafika.
Kama ufufuo wa Yesu ndilo tukio muhimu zaidi katika historia ya Ukristo, kwanini waandishi wote wanatofautiana kiasi hiki kwenye maelezo ya msingi kuhusu siku hiyo?
Ndiyo maana watu wasioamini kuhusu dini wanazidi kuongezeka