Biblia ni kitabu kinachoongoza kuwa na migongano mingi na pia ni illogical


This is true mkuu maana watu wengi wanaozaliwa katika tamaduni fulani za kidini wanapokutana na kitu kinachobadilisha mtazamo wao mara nyingi hukimbilia kudismiss hoja hata kama ni ya kweli. Kuna kitu nimejifunza sana mkuu kwenye huu Uzi wadau wanakwepa maswali kwasababu ya hii cognitive dissonance, wanahisi kama identity yao inakosolewa au inapingwa basi wanatafuta namna kukwepa swali maana linaweza kuwavuruga wanachokiamini.

Unapogusia dini za watu unakuwa umegusia identity ya wanaoamini. And I think hii kitu ipo kwenye physchology kabisa mkuu kuna issue ya defensive mechanism ambavyo hutokea kwa watu kila unapojaribu kugusa identity yao. Alarm ya defensive iki fire tu watu hukimbilia kwenye personal attack na kuacha ukweli.

Well analyzed boss 🤝
 
Lakini mbona maandiko hayo yanakasoro? Yana migongano, hayaakisi ulimwengu wa sasa na sayansi yetu ilivyo, Ina vitu ambavyo ni impossible vina violate laws of physics?,
Tuweke mambo sawa. Sisi tunaoishi leo tunaishi wakati wa "Sheria ya Kristo" hivyo ambacho hakielezwi vizuri Agano la kale kinaelezwa vizuri Agano Jipya.

Nafikiri si sahihi kusema masimulizi ya biblia (maandiko) yana kasoro kwa sababu yenyewe (maandiko) yameandikwa kutoka kwa desturi, miiko, mila: ibada, sadaka, taamuli; tamaduni na kadhalilka.

Matendo hayo, ambayo kwa kweli yamekuwepo na yamekuwa yakifanywa na jamii za watu wote popote ndiyo kwayo masimulizi ya biblia imeandikwa.

Kumbe kimsingi kasoro ni matendo hayo, ambayo kwa kweli yameonyesha kuwepo kwa kasoro nyingi. Na hili linaendelea hata leo.

Leo fikiria, katika dini hizohizo zinazokubali kwamba kuna Mungu mmoja lakini kwenye suala la ndoa kwa mfano, dini moja inasema ndoa ni ya mume mmoja na mke mmoja na nyingine inasema ndoa inaweza kuwa ya mume mmoja na mke zaidi ya mmoja.
 


Kama hayana kasoro, embu elezea ushahidi wa Nuhu, Adam alikuwa anawatoto wangapi, Kaini baada ya kwenda nchi ya mbali hiyo nchi ilitoka wapi ilihali wao ni watoto wa adamu na Adamu ni binadamu wa kwanza?

Lugha zimetoka wapi, wakati study of linguistics inatuonesha namna tulivyo evolve over time.
 
Lugha ni kwa ajili ya mawasiliano. Yaani kuhamisha maana kutoka kichwani mwangu kwenda kichwani mwako.

Kichwani mwetu kuna nini? Kuna mawazo (thought). Hii thought tunaiweka katika matendo na hapo ndipo dhana ya mawasiliano inakamilika.

Kwahiyo maandiko ni mawazo (thought) na matendo, ambayo yamehamishwa kutoka vichwani mwa watu mbalimbali kwa nyakati mbalimbali na kuwekwa katika maandishi ili watu wengine wa nyakati zilizopo na zitakazokuja waweze kusoma na kuhamishia vichwani mwao.

Kwa msingi huo chenye kasoro hapo sio lugha au maandishi. Chenye kasoro ni maana (mawazo (thought) na matendo), ambayo ndio tunahihamisha kutoka vichwani mwetu kwenda vichwani mwa wengine kwa kutumia lugha.

Kuhusu Adamu. Sifikiri kuwa Adamu ndiye binadamu wa kwanza. Nafikiri simulizi hilo linataka kutuambia lazima kulikuwa na mwanamume na mwanamke wa kwanza kuumbwa.

Hilo la lugha imetoka wapi. Umelieleza vizuri kisayansi. Kwenye biblia "lugha imetoka wapi" inaelezwa kama unavyoelezwa ulimwengu.
 
Dhambi ni dhana ya kutungwa tu na dini. Kwa viumbe hai wanacho experience kwa uhalisia ni maumivu na mateso.
 
Dhambi ni dhana ya kutungwa tu na dini. Kwa viumbe hai wanacho experience kwa uhalisia ni maumivu na mateso.
KWa nini usifanye ubaya wote unaojua wewe, kaue, kadanganye, kaibe, kadhulumu... nini kinakuzuia?
 
KWa nini usifanye ubaya wote unaojua wewe, kaue, kadanganye, kaibe, kadhulumu... nini kinakuzuia?

Sheria na intelligence. Tukitumia dhana ya first principle of thinking binadamu hamiliki chochote lakini kutokana na maendeleo tumejimilikisha Ardhi, product mbalimbali tunazotengeneza, wanyama wa kufugwa makazi, mazao lakini vyote hivyo ni kwasababu ya maisha ambayo tumeyachagua tukija upande wa nature hamna anaemiliki chochote everything is free out there kwahiyo dhana ya wizi imetengenezwa pale binadamu alipoanza kujimilikisha but by nature everything is free ni kama wanyama porini no one owns anything kila kiumbe kipo kwenye habitat yake.
 
KWamba wanyama wa kufuga tulijipa sisi? Uliwaumba wewe hao wanyama?

Nature nani aliiumba? Who made nature? Did something just appear? And why kila kitu kinakufa ambacho ni organic?
 
Biblia si ya kusomwa kama novel hutaelewa. Husomwa na kueleweka kwa watu wa kiroho tu
 
KWamba wanyama wa kufuga tulijipa sisi? Uliwaumba wewe hao wanyama?

Nature nani aliiumba? Who made nature? Did something just appear? And why kila kitu kinakufa ambacho ni organic?

We don't know but I believe we are part of the star, since the building blocks of life are from cosmos. I mean I believe what Carl Sagan said. There is evolution which made us here so that's what I know I don't know where did we come from. We can't dismiss it's God since we have not figured it out one day humanity will do it.
 
karibu

https://www.jamiiforums.com/threads...otent-singularity-imeandaliwa-na-iit.2483819/
 
Kwaiyo ulitaka ukitaka kufanya dhambi kwa mkono mkono uvunjike ? Wewe ni mfano wa Mungu tumia akili yako ikupe maarifa Unazungumzia ukuu na uweza wa ajabu ambao hauzungumziki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…