Kwa kifupi sana.
Mfalme Constantino wa dola ya rumi (roman) kipindi hiko wakiwa wanatawala dunia, aliwahi kupigana vita na aliweka ishara ya msalaba kama ishara kuu ndani ya jeshi lake. Akashinda ile vita, kwahiyo akatoa agizo dunia nzima kuwe na dini moja tu, ya Kikristo japo mwanzoni dola hiihii ya Rumi ilikuwa ikiipinga mno dini ya Kikristo na hata kuchoma moto maandiko matakatifu yaliyoachwa na waasisi wa imani hiyo, yaani mitume na manabii.
Unfortunately, ndani ya serikali yake, alijali sana kuwaweka Wakristo, matokeo yake dini ikaanza kupoteza ile nguvu ya rohoni na kutoka ktk ile misingi ya mitume na manabii. Tamaduni za kirumi kama kuabudu sanamu, sikukuu n.k vikaanza kuingizwa ndani ya kanisa. Kanisa likafa kabisa rohoni, likabaki jina tu la Ukristo ila rohoni hakukuwa tena na ile nguvu.
Miaka mingi mbele, kwa kufanya utafiti mbalimbali walitokea watu kadhaa wakasema kwamba imani ya Kikristo imepotoshwa na Kanisa Katoriki kwa kufanya ibada za sanamu, kuingiza sikukuu zisizo na maana ndani ya kanisa pamoja na mafundisho manyonge. Watu hawa kwa Historia ya Kanisa wanafahamika kama wana wa uamsho.
Watu hao kuna akina Max, Martin Luther n.k kabla ya Martin Luther walikuwepo watu kadhaa kama watano ambao walichallenge uendeshwaji wa Imani ya Kikristo unaoongozwa na Rumi(Roma) ila tunamtambua Martin Luther sababu yeye aliachana nyaraka nyingi na ndie mwana uamsho mkubwa wa mwisho.
Rumi walihizinisha vitabu 72 na kuundwa Biblia, ndani ya hivyo vitabu 72, Martin Luther King aliviona vitabu 6 havina mafundisho mazuri/umuhimu ktk makuzi ya maisha ya Mkristo kiroho. Ifahamike kuwa Martin Luther alikuwa msomi na Padre ndani ya Kanisa Katoriki.
Baada ya Martin Luther kusigana na viongozi wake, Martin Luther na Katoriki wakatengana, ndipo ukazaliwa uamsho mpya ndani ya Kanisa, hapo ndipo likaja dhehebu la KKKT, lilikuwa na uamsho mkubwa saana kiroho, huduma zote ambazo Yesu aliacha ndani ya Kanisa kupitia Roho Mtakatifu zilionekana, shetani jinsi alivyo na nguvu akapiga kanisa KKKT nalo likatawanyika, hapo sasa ukazaliwa Upentekoste, Pentecoste na KKKT ni kama baba mmoja ila mama tofauti.
Mwisho, tafsiri za Biblia zipo nyingi saana, wala usishtushwe na hizo tafsiri ila kwa sehemu kubwa maana ni ile ile. Ni sawa na kitabu kimoja cha Ushairi kisha kikachambuliwa na maprofessor wa kiswahili, wengine kutoka UDOM, wengine kutoka UDSM na wengine SAUT ila maana ni zile zile.