Biblia wanayotumia Wakotoliki na wanayotumia Walutheri pamoja na madhehebu mengine ni tofauti?

bibilia zote ni za wakatoliki ila wengine wamepunguza vitabu japo walutheri wengi wanatumia tena bibilia zenye vitabu vyote wao ni wanunuzi wa bibilia za kikatoliki.
Wakatoliki wanamatoleo matatu yanayotumika sana kwa sasa:-
  1. toleo la Iringa -hii inanunuliwa sana na walokole pamoja na walutheri
  2. bibilia ya Kiafrika hii watu wengi hawaipendi kwa kiswahili chake lakini kwangu ni best bible na rahisi kuisoma
  3. neno la MUNGU kwa watu wote -hii ni kiswahili cha kisasa ndogondogo
 
Acha uongo
Biblia ya kwanza ilikua imeandikwa kiebrania na aramaic na ilikua ni agano la kale kwa asilimia kubwa
 
Pamoja na kuwa na vitabu vingi lakini hamvisomi na wala hujui kilichoandikwa humo.
Msisitizo uko kwenye kumuomba bikira Maria na kubusu misalaba.
Kitabu kinachotumika ni Misale ya waumini tuu hakuna nje ya hapo.
Hata amri za Mungu zimechakachuliwa mkaruka amri ya " Usijifanyie samamu ya kuchonga wala mfano wa kitu chochote kilicho duniani wa mbinguni, ukaviabudu wala kuvitumikia".
Kutembeza sanamu la bikira Maria ni kutumikia hiyo sanamu.
 
Wakatoliki wana biblia yao wanayoiita misale ya waumini, ndiyo hiyo yenye vitabu vingi kama wamakabayo, sira na vingine. Mkanganganiko huu ndio huwapa waislam point ya kuuzodoa ukristo na kuona quran yao ipo sahihi kuliko biblia kumbe huko kwao nako ni abrakadabra tu afadhali ya biblia mtu yuko huru kuamini au kutokuamini na halazimishwi kuamini
 
Hii Ndiyo maana ya GT, kuleta kitu kikubwa bila ushahidi ni mbaya sana, sasa asiyependa apinge huo ushahidi.
 
Hii ni mada ingine mkuu. Kama unataka tujadili anzisha mada.

Mimi ni mkatoliki nadeclare interest na wewe useme dhehebu lako kisha tukutane kwenye hiyo mada. Usiharibu hii mada ya watu
 
Mkuu kuna Baadhi ya mambo uko Misinformed..
Nisamehe kama nitakuwa nimekuambia kwa Approach mbaya..

Ila Kajifunze kuhusu Constantine tena na how Aliweza kuaccept Imani ya Dini ya kikristo iingie nchini kwake hapo nahisi bado hukuelewa..

Pili Vitabu Vilifanyiwa finalization Na kikao cha mtaguso wa carthage "The Councils of Carthage"
Mnamo mwaka 393 AD mpaka mwaka 397 AD na hapo ndo walikuwa na significant role in confirming and finalizing the canon of the Bible..
Na ndo walipata Vitabu 72 na huku Vingine wakiviacha..

Na hapo ndo kulitokea Utengano kati ya Eastern na Western..Eastern wao wakaamua kuwa na Vitabu kwenye Biblia 76 mpaka 82 wakati West wakaamua kuwa na Vitabu 72..

Wakati huo Martine luther ameanza kufanya Reformation October 1517..

Ikiwa ni zaidi ya Miaka 1200 imepita Na kuondoa vitabu..
Swali ni kwamba Martine alitumia Vigezo gani kuondoa Vitabu vilivyokuwepo kwa Miaka 1200??
 
Correction: Martin Luther aliona vitabu sita haviendani na mafundisho na maslahi yake
 
Kwa sanamu nitawatetea kwa sababu biblia imeeleza maana nyingine ya Sanamu na sio vilivyotengenezwa..

Wakolosai 3:5

"Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, Hiyo ndiyo ibada ya sanamu;"

 
Martin luther alicopy na kupaste biblia ya kiyahudi baada ya kuona ile ya warumi imrongezwa vitabu ambayo wayahudi walivikataa kwamba havi-inspire kiroho
 
Martin luther alicopy na kupaste biblia ya kiyahudi baada ya kuona ile ya warumi imrongezwa vitabu ambayo wayahudi walivikataa kwamba havi-inspire kiroho
Hakukuwa na Biblia ya Kiyahudi wakati huo Tusipende kupotosha..

Watu wengi mnachanganya kati ya "Hebrew Canon" na "Masoretic Text"
Na ni Hofu kubwa mnazidi kupotosha sana..

Kwanza biblia ya kiyahudi (Tanakh) Ina vitabu 24..

Torah 5, Neviim 8, Ketuvim 11,..
Na haina Agano Jipya..

Sasa kama agano la kale la Tanakh ni 24..

Yye alipata wapi vitani 36 vya agano la kale?
 
Lete ushahidi kama kweli dini ni tool ya kutawala watu. Umesoma wapi hilo andiko?
🤣Umeona na wewe... we hushtuki mtu anakuletea kitabu anakuambia Mungu kaniambia nikiandike nikiokoe..na wewe unasema yes sir na kutoa sadaka...na kutawaliwa kiuchumi kisiasa mpaka maisha yako private unaambiwa mpaka upige style gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…