Bidhaa zimepanda bei, sasa Soda ni Tsh 600/=

Bidhaa zimepanda bei, sasa Soda ni Tsh 600/=

Serikali haina msimamo kabisa, kwani wenyewe si ndio waliondoa baadhi ya kodi na tozo kwenye vinywaji, budget ya 2021/2022 sasa kila kitu kinapanda hovyohovyo kwani na malighafi zinatoka Urusi au Ukraine

Sent from my CLT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Hizo soda za chupa au take away?
Hapo ndipo naona utofauti wa Tanganyika na Zanzibar, huku Nungwi - Zanzibar tumezoea kuuziwa soda 1000/1500 na tunaona fresh tu, tukija Tanganyika tukitoa 1000 tunaondoka hadi muuzaji/muhudumu akuite akurudishie chenchi ndipo unakumbuka uko Tanganyika na si Zanzibar.
 
Soda Leo nimenunua elf 11800 per creti moja mwanzo ilikua 9700 aisee na sasa ni rasmi soda za coca zinauzwa tsh 600 badala ya miatano ya awali,

ama kweli mama anaupiga mwingi.
Haupigi mwingi tu bali anatakeleza ilani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Soda Leo nimenunua elf 11800 per creti moja mwanzo ilikua 9700 aisee na sasa ni rasmi soda za coca zinauzwa tsh 600 badala ya miatano ya awali,

ama kweli mama anaupiga mwingi.
Nimepita mall hapa dodoma, club soda take away sh950
 
Soda, Sigara na Sukari Vipandishwe bei tu, sababu ni Sumu
 
Bei ya soda imerudi mahali pake, maana hapo kabla soda zilifika hadi sh.700
 
Soda ina sukari nyingi, sukari nyingi inasababisha magonjwa yanayohusiana na mifumo ya maisha.

Soda kwa wingi inasababisha kuongezeka uzito, kisukari na magonjwa ya moyo.

kuna documentary iko Netflix ( itakuwa na credibility na ubora wa kiwango fulani mpaka ikawekwa netflix) inaitwa WHAT THE HEALTH

inasema sukari haisababishi kisukari, kwa sababu kisukari ni mwili kushindwa kuchakata sukari... ni tatizo unalo tayari, inherent problem ya mwili wako.... Kisukari kinaletwa na vinasaba vyako pamoja na vyakula vibovu kama mafuta, nyama nyekundu, nyeupe, mayai, maziwa...

kuhusu sukari na unene (obesity), documentary inasema sukari ya ziada mwilini inaenda kutengeneza glycogen...glycogen haina shida.... tatizo la unene linaletwa na mafuta, na hili ndio wamelisisitiza sana....

kuhusu magonjwa ya moyo, hakuna utafiti ulio link magonjwa ya moyo na vyakula venye sukari

Wanaoongea kwenye documentary hiyo ni ma professa na watafiti wa afya, chemia ya uhai, madawa, the whole nine yard...
 
Back
Top Bottom