Episode 2.
Kwa majina anaitwa ERIC RICHARD LYNN WRIGHT amezaliwa tar 07/09/1964 katika jiji la CALIFORNIA ndani ya viunga vya COMPTON huko nchini MAREKANI.
Wazazi wake walikuwa ni waajiriwa, bwana RICHARD LYNN WRIGHT na mkewe KATHIE WRIGHT hawakusita kumpeleka kijana wao Shule, wakitamani siku moja awe daktari..
Lakini mambo hayakuwa kama walivyo tarajia wazazi hawa..Badala yake ERIC LYNN WRIGHT yeye hakuzingatia sana masomo isipokuwa alizingatia kuimba nyimbo za kufoka foka.
1977 yaani akiwa na umri wa miaka 13 tu! Alianza kuunda magenge ya mtaani kwa kushindana kuimba nyimbo za kufokafoka.
Maisha ya watu weusi marekani kwa miaka hiyo bado hayakuwa Rafiki, walinyimwa kazi, ni watu waliotengwa na kudharaulika.
Walitemwa mate na kuitwa niggaz.
Kupata kazi bado kulikuwa ni shughuli kubwa kwa mtu mweusi ili uwe na pesa ama tajiri iIibidi uwe jambazi, mcheza mpira, mwanariadha, Mwana muziki au gangster.
Gangsters ni vikundi vya mtaani, mara nyingi vikundi hivi hupokea order ya kuua, kupora ama kusambaza bangi na madawa ya kulevya.
Kwa kifupi ni vikundi vya kijambazi au ni magenge ya wahalifu "Criminal gang" wao huvunja sheria mara zote, vikundi hivi si rafiki na polisi hata kidogo.Kijana ERIC LYNN WRIGHT akadondokea kwenye vikundi vya gangster.
Alianza kuwa msambazaji wa drugs ndani ya viunga vya COMPTON na mwisho jina lake likaanza kutajwa ndani ya jiji la CALIFORNIA kwa kusambaza madawa ya kulevya.
Hapa ndipo alipoanza kujiita EAZY-E alipata pesa na vitu vyote vya samani ambavyo vijana wenzie ilikuwa ngumu kupata.
Mwaka 1980 akiwa na umri wa miaka 16 baba yake mzazi alimtaka anunue nyumba ili aanze maisha yake mwenyewe.
Hii ilikuja baada ya EAZY-E kuwa na tabia ya kuingia kwenye store au gereji ya baba na kufungua muziki kwa sauti kubwa huku akiimba na kurecodi muziki.
Eazy-E alinunua nyumba yake ya kwanza iliyokuwa karibu na wazazi wake.
Huku washikaji zake kama Dr Dre na Ice Cube na DJ Yella wakiifanya Nyumba hiyo kuwa maskani ya kujifunzia music.
Ni wakati huu pia Eazy-E anakutana na mzungu mmoja aliyefahamika kwa jina la JERRY HELLER.
JERRY HELLER akiwa kama "drug dealer" yaani muuza madawa ya kulevya, anaamua kuungana na kijana Eazy-E sababu Eazy-E alishakuwa na jina kubwa na mtandao wa watu.
Muungano wao ulikuwa mzuri na ukazaa matunda, wakapiga pesa na mwisho.
Wakawa gumzo ndani ya vilindi vya COMPTON na CALIFORNIA nzima.
Polisi wakaanza kuwa wageni wao kila kukicha, kuna wakati walikamatwa na kuulizwa wanapata wapi pesa zote hizo.Ili kutakatisha pesa ndipo EAZY-E Akapata wazo la kufungua studio.
Na kuipa jina la RUTHLESS RECORDS,Na pia EAZY-E mwenyewe akawa msanii huku akimfanya JERRY HELLER kuwa music manager wake.
hii ilikuwa ni mwaka 1987 mambo yalianzia hapaa.
Eazy-E Alianza kutoa nyimbo zenye maudhui ya kutetea mitaa kuwachana polisi na watu weupe wote wenye kuendekeza racism.
kusikia tusi kwenye nyimbo za Eazy-E si kitu cha ajabu, aliimba kwa sauti ya juu na msisitizo.
Eazy-E hakuishia hapo alizidi kupiga hatua na mwaka huo huo 1987 akaanzisha kundi la music na kulipa jina la N.W.A.
yaani NIGGAZ WIT ATTITUDES Kundi hili liliongozwa na Eazy-E huku akiwa na watu kama....Dr. Dre MC Ren, DJYella Ice Cube.
Hapa ndipo muziki wa HipHop ulianza Kubamba marekani na ulimwenguni.
Ni wao pia ndio walio itangaza COMPTON na CALIFORNIA kwa ujumlawalisumbua hawa vijana walivaa Nguo za hadhi ya juu na kuendesha magari ya kifahari.
Binafsi ninakiri NIGGAZ WIT ATTITUDES ama N.W.A lilikuwa ni kundi lililowahi kumiliki rundo la pesa.
Polisi Hawa kuvutiwa na kundi hili.
Siku moja JERRY HELLER akiwa Studio na vijana wake.
Mmoja wao ambaye ni Dr Dre alitoka njee kwa Lengo la kuzungumza na mpenzi wake, lakini hakuweza kuelewana na mpenzi wake kutokana na mtafaruku ulio tokea kati yao.
Baada ya mpenzi wake kuondoka mara polisi Wanafika na kumkuta Dr Dre na jamaa zake ambao DJ Yella, Ice Cube, MC Ren na Eazy-E.
ambao wakati huu kina Eazy-E walitoka nje kwa lengo la kumuuliza Dr Dre kama amefanikiwa kuyamaliza na mpenzi wake.
Sasa polisi baada ya kuwakuta vijana hawa wakawaamuru walale chini.
Na vijana walipokuwa wabishi kutii amri hiyo walimwagiwa vinywaji vyao, na kuamrishwa walale chini haraka iwezekanavyo.
Vijana wali too agizo Hilo, na kulala chini.
Ndipo manager JERRY HELLER anatoka ndani ya Studio na kuwakuta vijana wake wamewekwa chini ya ulinzi.
JERRY HELLER alikasilika na kuhoji sababu za vijana hao kuwekwa chini ya ulinzi.Aliambiwa vijana hao wanaonekana ni wahuni ni kama genge la kijambazi.
JERRY HELLER alikasirika na kuhoji sababu za vijana hao kuwekwa chini ya ulinzi.
Aliambiwa vijana hao wanaonekana ni wahuni ni kama genge la kijambazi.JERRY HELLER alilalama na kusema sababu vijana hao ni weusi ndio wanafanyiwa ivyo.
Ni wasanii wake na yuko nao studio ivyo hawastahili kufanyiwa hicho wanachofanyiwa.
Polisi wakamjibu JERRY HELLER anapoteza muda wake kuwasimamia vijana hao.
JERRY akapaza sauti.."hivi ndivyo mnavyo wakamata watu weusi na kuwafanyia..? ni unyanyasaji naomba muwaachie".
Baada ya malumbano ya muda mrefu polisi wanakubali kuwaachia vijana hawa.
Wakati wananyanyuka kutoka pale chini walipolala Ice Cube alitamka chini chini neno Fuvk police.
Wakati wana nyanyuka kutoka pale chini walipolala Ice Cube alitamka chinichini neno Fuvk police.
Dr dre akadakia na kusemaa.."That word sounds good"Kilichofuata wakaingia Studio na kuachiwa nyimbo.
Na kuipa jina la Fuvk Tha Police.Hii ni mwaka 1988 Katika nyimbo hiyo polisi wame kaangwa kama bagia.
Yaani katika nyimbo hiyo kundi la N.W.A limejivika wadhifa wa mahakama ili kuihukumu polisi dhidi ya matendo yao kwa watu weusi...
Lakini pia wanajaribu kufikisha Ujumbe kuwa wao ni wanamuziki, muziki ni kama mahakama, ila mahakama hii ya muziki inaweza kuhukumu na kufichua haki kisaikolojia..
Sasa.. mambo yakifichuliwa na walengwa kuhisi kama wako huchi, ndio hivyo mnasikiaga nyimbo za kichochezi..
Katika nyimbo hii, yanasikika, maneno yanayosema..
Right about now NWA court is in full effect, Judge Dre presiding in the case of NWA versus the police department"Kwamba...
"Hivi sasa mahakama ya NWA inafanya kazi kikamilifu"
Na Dr Dre ndiye jaji anayesimamia kesi ya NWA dhidi ya idara ya polisi.Sauti inasikika tenaa..."Prosecuting attourneys are MC Ren, Ice Cube and Eazy motherfuvkin' EOrder, order, order, Ice Cube.
take the motherfvckin' stand. Do you swear to tell the truth the whole truth, and nothin' but the truth so help your black a.s?".
Kwamba...Mawakili wanaoendesha mashtaka ni MC Ren, Ice Cube na Eazy-E aka Motherfuvkin' E.
Na mwisho sauti iliwauliza mawakili hawa kwamba je wanaapa kusema ukweli wote ili wawasaidie ndugu zao weusi dhidi ya kunyanyaswa na polisi mara zote..?.
Wanatumia neno "black a.s" yaani punda mweusi wakimaanisha mtu mweusi.
Kutokana na manyanyaso waliyokuwa wakipitia watu weusi nchini marekani, makundi kwa makundi wakajikuta Wanaipa masikio yao nyimbo hiyo, hii ikafanya nyimbo kuvuma na kubamba.
Wakiwa kwenye show kila wakati mashabiki zao waliomba wimbo huo wa F***k police.Ice Cube akisimama as mtunzi wa nyimbo hiyo lakini likewise ndiye anayesikika kutoa maneno makali katika verse ya kwanza.
Katika kazi kunakuwa na maslahi, kipato na kisha mafanikio.
Lakini Ice Cube alianza kunote kitu katika mafanikio ya kundi la N.W.A Kwamba Eazy-E na mshirika wake wa kibiashara ambaye ni JERRY HELLER walikuwa wakikusanya pesa nyingi huku wao wakipewa pesa kidogo.
Hili aliliona ICE CUBE na alipo ongea akaambiwa asaini mahali fulani.kwamba ndio mkataba, yeye alihitaji kusoma vipengere vyote akaambiwa asubiri mkataba utatoka kwa mwana sheria then atapatiwa.
Easy E na JERRY HELLER wakagundua kuwa ICE CUBE ni mtu mwenye misimamo mikali.
Maisha yakaendelea lakini jambo kubwa ambalo hakulijua ICE CUBE ni kwamba wenzake wote walisha saini yale makaratasi, ni yeye tu ndio hakusaini.
Yaani tayari Dr. Dre, MC Ren na DJ Yella walikuwa ndani ya mkataba kwa kujua au kuto kujua..
Kundi la NWA liliendelea kuwa tishio,
Kundi hili likavuma na kuendelea kufanya nyimbo nyingi huku ICE CUBE akisimama kama mwandishi wa nyimbo zote.
ICE CUBE ndiye mtu aliyekuwa akisisitiza kuhusu mikataba kwamba mambo yasiwe kishikaji bali yanapaswa kwenda kimaandishi.
JERRY HELLER akiwa kama manager wa kundi hilo.
Alimuahidi ICE CUBE kwamba mikataba itakuja iko inaandaliwa na mwanasheria mara zote alimwambia ivyo, but hakukuwa na mkataba wowote zaidi ya danadana.
Japo ICE CUBE alidai haki zake na kuzunguushwa zunguushwa bado aliendelea kuwa na furaha na kubaki katika kundi.
Sina shaka kwamba kundi lilifanya vizuri mpaka SUGE KNIGHT akaanza kujiweka karibu na wasanii wa Eazy-EMara kadhaa SUGE KNIGHT aliwatembelea kina Eazy-E.Huku 2pac naye akionekana kuwa karibu na Eazy-E, walitoa nyimbo kama.. Gangster Love, HomeboyzPay back, How we do.
Ni wakati huu pia SUGE KNIGHT alimwambia Eazy-E kwamba kwa hatua waliyoipiga anahitaji kuwa na mlinzi.
eazy e alisema haitaji hilo, SUGE KNIGHT alisikika akisema neno moja kwamba..."You never know what you need, until you need it" Ni wakati huu pia ICE CUBE hakukaa sana katika kundi na akaamua kujitoa.
I will be back, shout out to wisdom.
I mean no malice to nobody.
View attachment 2965187View attachment 2965188