Bifu linaendelea, Mume wa Waziri Gwajima akana kumtambua Mathias Gwajima kama Baba yake

Bifu linaendelea, Mume wa Waziri Gwajima akana kumtambua Mathias Gwajima kama Baba yake

Yalikuwa makosa makubwa ya mfumo kumwingiza mtu Kama huyu. Ni hatarii kwa nchi, Serikali. Anaweza tamka chochote, mahala popote, wakati wowote.
 
Yalikuwa makosa makubwa ya mfumo kumwingiza mtu Kama huyu. Ni hatarii kwa nchi, Serikali. Anaweza tamka chochote, mahala popote, wakati wowote.
kipindi icho mfumo haukuepo ilikua ni maamuzi ya msukuma mmoja
 
Huyo waziri alitakiwa asijibizane nae ili kulinda heshima yake na ya serikali.
Kinacho onekana Sasa Ni kuoneshana MAUBABE huyu kupitia kachucheri, Mwingine kupitia serikali bila kujali kuwa kailli anazotoa zitatekelezeka au laah!!!!
 
Nchii hii ngumu sanaa,yaan kiongoz wa din na wa serikali wameamua kuingia ligue ya kuchambanaa!!basii sawaa tuseme michambo inaruhusiwa!hadi na wasukuma nao kwel?aah!hapa kuna tatizo la kimfumo
 
Picha ya Marehemu Mzee Stiven Gwajima. Huyu ndiye alikuwa Mkwe wa Waziri wa Afya Dorothy Gwajima.

Mzee Stiven Gwajima alifariki dunia tarehe 30/9/2019 jijini Dar es Salaam. Mtoto wake Mwanasheria Msomi Methusela Gwajima amezungumza na #KitengeTV na kusema huyo ndio alikuwa Baba yake na Mkwe wa Waziri wa Afya na sio mwingine yeyote "Amesema jioni hii"...
Kama alishakufa , baba mkubwa au mdogo sio baba mkwe? Mnaishi Africa au ulaya?
 
Mufindi, Iringa

Jumapili jana 22-Agosti-2021 Askofu Gwajima aliweka bayana maelezo ya hoja zake kuhusu chanjo, na kuwataka waziri na naibu wake wenye dhamana wajibu hoja hizi kwa hoja zenye nguvu.

Akifafanua, askofu alionyesha kwamba mawaziri hao huko nyuma walizunguka kwenye vyombo vya habari wakieleza mashaka waliyonayo kwenye chanjo na kuhamasisha watanzania kujifukiza na kutumia miti-shamba kukabiliana na UVIKO-19.

Askofu Gwajima aliweka bayana zaidi kwa kuonyesha clip ya naibu waziri wa afya Dr. Mollel akifafanua kwenye runinga madhara ya muda mfupi na muda mrefu ya chanjo na kwamba chanjo hiyo inaweza kuathiri utu wa mtu, clip ambayo imezunguka sana kwenye mitandao ya kijamii.

Askofu pia alionyesha waziwazi ukosefu wa weledi wa waziri Dorothy katika kufafanua mambo, akisema waziri ameamuru majeshi yote [ yaani jeshi la magereza, polisi, jeshi la wananchi, takukuru n.k] yamkamate askofu Gwajima wakati hana mamlaka ya kuagiza majeshi hayo. Hiyo mamlaka anayo raisi.

Kabla ya kumaliza kufafanua askofu aliomba muongozo kutoka kwa baba yake Mzee Mathias Gwajima ambaye ni mkwe wa waziri wa afya. Mzee Mathias Gwajima alionyeshwa kusikitishwa na huyo mkwewe na kuamuru asitishe kutumia jina la Gwajima.

Baadae Maulidi Kitenge alipost kwenye ukurasa wake wa Facebook picha ya mzee Stiven Gwajima anayedaiwa kuwa baba mzazi wa mme wa waziri wa afya Methusela Gwajima, kwamba alifariki Septemba 2019.

Ikumbukwe wakati Askofu Gwajima anafafanua alisema baba wadogo wametangulia mbele ya haki, na mkubwa aliyebaki kwenye ukoo ni mzee Mathias Gwajima ambaye ni baba yake.

Wakili Methusela Gwajima, sambamba na post ya Maulidi Kitenge iliyokuwa na lengo la kuonyesha kwamba mkwe halali wa waziri wa afya ni marehemu Stiven Gwajima, alipost picha nyingine mtandaoni akisema huyo marehemu Stiven Gwajima ndo mkwe pekee wa waziri wa afya na hakuna mwingine.

Katika kufuatilia mambo huyu Methusela siku za nyuma aliibuka na kumtetea Paul Makonda wakati wa sekeseke ya madawa ya kulevya na kwamba alikuwa sawa kumtuhumu askofu Gwajima na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Haikuishia hapo, wakili huyu ambaye ni mme wa waziri wa afya baada ya kaka yake askofu Gwajima kugombea ubunge jimbo la Kawe naye alichukua fomu ya kugombea, akapita pita kwa wajumbe akisema yeye ndo Gwajima halisi "original" lakini hakuambulia chochote.

Methusela huyu ndiye aliyeongelewa na mke wake waziri wa afya kwamba ametest mitambo baada ya waziri kuchanja.

Kweli ukistaajabu ya Dorothy ya kucheza kiduku na kuamrisha majeshi yote; utayaona ya mme wake Methusela kumkana baba yake Mathias Gwajima.

Kwa akili za kawaida Methusela ilimbidi acheze vizuri na brand ya Gwajima ambayo askofu ameitengeneza, ili na yeye mambo yake yamwendee vizuri; lakini inaonekana anamhujumu kaka yake askofu Gwajima.

Makonda aliyekuwa anamtetea amepotea kwenye medani za siasa na uongozi sawa na maneno ya Askofu Gwajima; Methusela ameshindwa kuusoma mchezo??

Tulizoea kusema "kwako mwl Kashasha" buriani mchambuzi huyu wa soka...

Tungetamani kujua hii ngoma itaishia wapi; lakini askofu Gwajima amesema amefunga mjadala wa mambo ya chanjo; ili kumpa raisi nafasi ya kujenga nchi.

Kisimbo
Mwandishi wa Kujitegemea - Iringa.
 
Yani na ww umehukum moja kwa moja kuwa kamkana baba yake we una uhakika gani kuwa huyo ndo baba yake mzazi na wakat muhusika mwenyewe kasema baba yake kafariki 2019
 
Huyu wakili inaonekana Ana ugomvi na Wivu juu ya Gwajima Hana lolote apuuzwe tu
 
Nchii hii ngumu sanaa,yaan kiongoz wa din na wa serikali wameamua kuingia ligue ya kuchambanaa!!basii sawaa tuseme michambo inaruhusiwa!hadi na wasukuma nao kwel?aah!hapa kuna tatizo la kimfumo
Tunapo mjadili Mchungaji tusisahau kuwa, amepitia vitabu vingi vya Mungu. Nadhani msimamo wake unatokana kuofia kugeuka jiwe la chumvi Kama ilivyotokea kwa mke wa Ruti.
Wasio na Imani ya kweli ndo hao Jana waliikataa Sayansi na Leo wanaubiri Sayansi katika kolona.

Mama yopo sawa kwakuwa hakutumia kauli za kubeza Sayansi wakati ule. Wengine ni bendera fuata upepo na ni wa kuwaogopa Kama ukoma
 
I

v kwel kiuhalisia hili suala la kuchanja ambalo ni hiari na watu washaelewa somo lilikuwa ni la kutumia nguvu kiasi hiki kuzid haya matozo ya zakayo kila kukichaa?ningemuheshimu sanaa huyu anaejiita mchungaji endapo angetoa msimamo wake kuhusu hizi tozoo,sina uhakika sanaa kama wana kawe wamemtuma akakemee chanjo wkt wenyew wana matatizo chungu nzima
 
Tambua ya kuwa yeye pia anatoza ushuru waumini.
Hawezi guswa na iloo
 
Huwa nasoma post zako sana ila sijawahi ona hata moja tu yenye mashiko. Zote ni uharo mtupu.
Ndo maana nataka ubadilishe hapo juu kumuita mchungaji,n mchumia tumbo tu huyo alieamua kuwalevya wananjii kwa kujifika uaskofu fake
 
Gwajima askofu kwa tabia zake za uongo sitashangaa akifanya huo mchezo, yule ni msanii tu anaecheza na upepo kuwakamata wasiojua kufikiria vizuri, akiwaambia Corona haiji wanamshangilia, ikija anawadanganya na kingine sichanjwi wanamshangilia tena.
Mzee wa ufufuko feki
 
Back
Top Bottom