Mufindi, Iringa
Jumapili jana 22-Agosti-2021 Askofu Gwajima aliweka bayana maelezo ya hoja zake kuhusu chanjo, na kuwataka waziri na naibu wake wenye dhamana wajibu hoja hizi kwa hoja zenye nguvu.
Akifafanua, askofu alionyesha kwamba mawaziri hao huko nyuma walizunguka kwenye vyombo vya habari wakieleza mashaka waliyonayo kwenye chanjo na kuhamasisha watanzania kujifukiza na kutumia miti-shamba kukabiliana na UVIKO-19.
Askofu Gwajima aliweka bayana zaidi kwa kuonyesha clip ya naibu waziri wa afya Dr. Mollel akifafanua kwenye runinga madhara ya muda mfupi na muda mrefu ya chanjo na kwamba chanjo hiyo inaweza kuathiri utu wa mtu, clip ambayo imezunguka sana kwenye mitandao ya kijamii.
Askofu pia alionyesha waziwazi ukosefu wa weledi wa waziri Dorothy katika kufafanua mambo, akisema waziri ameamuru majeshi yote [ yaani jeshi la magereza, polisi, jeshi la wananchi, takukuru n.k] yamkamate askofu Gwajima wakati hana mamlaka ya kuagiza majeshi hayo. Hiyo mamlaka anayo raisi.
Kabla ya kumaliza kufafanua askofu aliomba muongozo kutoka kwa baba yake Mzee Mathias Gwajima ambaye ni mkwe wa waziri wa afya. Mzee Mathias Gwajima alionyeshwa kusikitishwa na huyo mkwewe na kuamuru asitishe kutumia jina la Gwajima.
Baadae Maulidi Kitenge alipost kwenye ukurasa wake wa Facebook picha ya mzee Stiven Gwajima anayedaiwa kuwa baba mzazi wa mme wa waziri wa afya Methusela Gwajima, kwamba alifariki Septemba 2019.
Ikumbukwe wakati Askofu Gwajima anafafanua alisema baba wadogo wametangulia mbele ya haki, na mkubwa aliyebaki kwenye ukoo ni mzee Mathias Gwajima ambaye ni baba yake.
Wakili Methusela Gwajima, sambamba na post ya Maulidi Kitenge iliyokuwa na lengo la kuonyesha kwamba mkwe halali wa waziri wa afya ni marehemu Stiven Gwajima, alipost picha nyingine mtandaoni akisema huyo marehemu Stiven Gwajima ndo mkwe pekee wa waziri wa afya na hakuna mwingine.
Katika kufuatilia mambo huyu Methusela siku za nyuma aliibuka na kumtetea Paul Makonda wakati wa sekeseke ya madawa ya kulevya na kwamba alikuwa sawa kumtuhumu askofu Gwajima na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Haikuishia hapo, wakili huyu ambaye ni mme wa waziri wa afya baada ya kaka yake askofu Gwajima kugombea ubunge jimbo la Kawe naye alichukua fomu ya kugombea, akapita pita kwa wajumbe akisema yeye ndo Gwajima halisi "original" lakini hakuambulia chochote.
Methusela huyu ndiye aliyeongelewa na mke wake waziri wa afya kwamba ametest mitambo baada ya waziri kuchanja.
Kweli ukistaajabu ya Dorothy ya kucheza kiduku na kuamrisha majeshi yote; utayaona ya mme wake Methusela kumkana baba yake Mathias Gwajima.
Kwa akili za kawaida Methusela ilimbidi acheze vizuri na brand ya Gwajima ambayo askofu ameitengeneza, ili na yeye mambo yake yamwendee vizuri; lakini inaonekana anamhujumu kaka yake askofu Gwajima.
Makonda aliyekuwa anamtetea amepotea kwenye medani za siasa na uongozi sawa na maneno ya Askofu Gwajima; Methusela ameshindwa kuusoma mchezo??
Tulizoea kusema "kwako mwl Kashasha" buriani mchambuzi huyu wa soka...
Tungetamani kujua hii ngoma itaishia wapi; lakini askofu Gwajima amesema amefunga mjadala wa mambo ya chanjo; ili kumpa raisi nafasi ya kujenga nchi.
Kisimbo
Mwandishi wa Kujitegemea - Iringa.