FMES, hiyo CV haithibitishi lo lote kuhusu uraia wake au wa baba yake iwe wa Tanzania au la.
Jenerali Ulimwengu aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya, Mjumbe wa NEC, Kamanda wa Vijana mkoa, na vyeo vingi na bado hakuweza kuthibitisha uraia wake. Huyu asili yake Rwanda.
Madam Madeleine Castico aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu (CCM) Visiwani, Mjumbe wa CC na NEC, Naibu Waziri, naye pia hakuweza kuthibitisha uraia wake. Huyu asili yake Msumbiji.
Bandora (kama sijakosea jina) wa Mambo ya Ndani aliwahi kuwa balozi wa Tz nje, career diplomat na bado alikinyanyua na kwenda kushika uzito Rwanda chini ya Kagame, na kututhibitishia kuwa hakuwa raia wa Tz.
Hiyo ya Mzee Mukasa kuwa Afisa Afya (which could be anything from sanitation officer, meat inspector, etc) siyo CV nzito kabisa ya kuthibitisha u-raia. Hata Chavda ana CV nzito kuliko hiyo (access hadi ikulu) na siyo raia.
Nimeona pia umeepuka katika bandiko lako (copied from
UPL-Homepage) kuonyesha kasoro kwa nini jina la Rwegasira halipo katika historia yake, lakini ghafla ni muhimu baada ya kupitishwa kuwa mgombea! Kama halikuwa muhimu kabla katika historia ya family kwanini liwe muhimu sasa?