Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

CHADEMA wameishiwa, hawana jipya. Huwezi kusema mtu siyo mtanzania kwa kutegemea mouth talk.
Mukasa ana doccs zote zinazoonyesha kuwa yeye ni mtanzania.Passport yake ya Tanzania, living certificates zake zote za O-level na A-Level zimeandikwa yeye ni mtanzania.
CHADEMA wanapoteza muda ambao wangeutumia kujiimarisha vijijini. Hivi vi-political technicalities havitawapeleka popote.
 
Mkuu FME, wamshangaa huyo kwani RA mbona amefika hapo alipo uraia wake je? Tanzania haijaanza kuliwa leo hasa na wageni toka nchi jirani hao ndo kabisaa!

- Mkuu wangu slow down, sheria zetu za uraia zinasemaje nataka tu kujaribu ku-entertain hii idea ya baba yake kuwa foreigner kama incase ingekua kweli?

FMEs!
 
- Sasa baba yake alifikiaje kufanya kazi kwenye serikali yetu mpaka kuwa ofisa wa juu huko wilayani na mkoani bila kua raia wetu? It does not add up!
Respect.
FMEs!

Mkuu FMEs, unamkumbuka Omari Juma aliyewahi kuwa katibu Mkuu wa FAT enzi za Said El Maamry ? Wagombea walikuwa wanachujwa kikwelikweli enzi hizo lakini aliweza kupita kwenye vikao vyote husika vilivyoshirikisha viongozi wa serikali na CCM. Nakumbuka mshtuko wa serikali na CCM siku ilipogundulika kuwa si raia - kwa aibu alipewa masaa kuondoka nchini.
 
Kipindi cha Nyerere swali la uraia halikuwa swala Kubwa kama ilivyo sasa, Watanzania wengi tumeshaamka na tunajivunia Uraia wetu, haikuwa hivi miaka ya zamani.

Nazani kwa mtu kama Mkasa amabaye historia yake iko wazi ni rahisi kumkubali kama Mtanzania bila kinyongo chochote, Kwa kweli mchango wake katika Idara ya Afya ni mkubwa sana tatizo sheria zetu za sasa za uhamiaji na Uraia ndio mbovu.

Swala la jina sio tatizo kwasababu tukianza kuanagalia Majina , Hata kina Mzee Lusinde na Jamii yake tungesema tuwarudishe Congo, kwasababu kina Lusinde ni jamii ya congo, Tatizo lililopo hatujaweza kuipitia sheria ya Uhamiaji tena na kuweza kuweka bayana vipengele vya kisheria ambavyo havina tija kwa Taifa. Kwa maoni yangu ,tukibadili sheria zetu kwenda kwenye Uraia wa kuzaliwa itatusaidia sana kutatua matatizo mengi kama haya na kuachana na huu utaratibu wa kutegemea Uraia wa baba.
 
- Mkuu hebu fafanua hapo kidogo, eti Lusinde ni watu wa Congo? Kwa vipi yaani?

Respect.

FMEs!
 
- Huyu mgombea either ni mbongo au sio, lakini so far kwa niliyoyasoma tayari sioni anything cha kunifanya niamini kwamba huyu sio mbongo, hivi kweli tukifuatilia baba za viongozi wetu walipozaliwa nani atabaki kwenye uongozi?

FMEs!

Uraia wa wazazi ndio unategemea uraia wa watoto. Kama baba yake Oscar alikuwa ni raia wa Tanganyika (kabla ya Muungano) au ni raia wa Tanzania basi uraia wa Oscar hauna mashaka hata kidogo.

Uraia hautegemei mtu amesoma wapi, amesomea nini au amefanya kazi kwenye idara gani. Hautegemei kama huyo mtu alikuwa ni mwaminifu kwa chama au serikali. Unategemea kanuni nyepesi tu.

Ni vizuri pia kuangalia uraia wa viongozi wetu ili tusije kuamka siku moja tukajikuta tunaongozwa na mgeni. Ndio maana wenzetu wa Marekani wao kwenye nafasi ya Urais hawana utata wameweka kabisa kuwa ni raia wa kuzaliwa (yaani hata raia wa kuhamia hawezi kuwa rais!).

Hilo ni kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa kuja kuongozwa na mtu ambaye siyo raia hasa wa nchi hiyo.

Kwa kadiri unavyofahamu baba yake Oscar alizaliwa wapi Tanzania/Tanganyika?
 
- Mkuu hebu fafanua hapo kidogo, eti Lusinde ni watu wa Congo? Kwa vipi yaani?

Respect.

FMEs!

Samahani kama nimekugusa, But the origin ya Hilo Jina ni Congo Mzee. So when walihamia Tanganyika , I dont know but if we want to pick people names by their origin I think kama ulivyosema hapo nyuma hatutakuwa na Viongozi.
 
- Eti wakuu hii ni CV ya mtu asiyekua raia wa Tanzania? Yaani mzazi wake alifikia mpaka kuwa ofisa wa serikali yetu huku akiwa sio raia wetu? Na huyu kijana yote haya ameyafanya huku akiwa sio raia wetu?

I am missing something or what?

Respect.

FMEs!

FMES, hiyo CV haithibitishi lo lote kuhusu uraia wake au wa baba yake iwe wa Tanzania au la.
Jenerali Ulimwengu aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya, Mjumbe wa NEC, Kamanda wa Vijana mkoa, na vyeo vingi na bado hakuweza kuthibitisha uraia wake. Huyu asili yake Rwanda.

Madam Madeleine Castico aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu (CCM) Visiwani, Mjumbe wa CC na NEC, Naibu Waziri, naye pia hakuweza kuthibitisha uraia wake. Huyu asili yake Msumbiji.

Bandora (kama sijakosea jina) wa Mambo ya Ndani aliwahi kuwa balozi wa Tz nje, career diplomat na bado alikinyanyua na kwenda kushika uzito Rwanda chini ya Kagame, na kututhibitishia kuwa hakuwa raia wa Tz.

Hiyo ya Mzee Mukasa kuwa Afisa Afya (which could be anything from sanitation officer, meat inspector, etc) siyo CV nzito kabisa ya kuthibitisha u-raia. Hata Chavda ana CV nzito kuliko hiyo (access hadi ikulu) na siyo raia.

Nimeona pia umeepuka katika bandiko lako (copied from UPL-Homepage) kuonyesha kasoro kwa nini jina la Rwegasira halipo katika historia yake, lakini ghafla ni muhimu baada ya kupitishwa kuwa mgombea! Kama halikuwa muhimu kabla katika historia ya family kwanini liwe muhimu sasa?
 
Mkuu FMEs, unamkumbuka Omari Juma aliyewahi kuwa katibu Mkuu wa FAT enzi za Said El Maamry ? Wagombea walikuwa wanachujwa kikwelikweli enzi hizo lakini aliweza kupita kwenye vikao vyote husika vilivyoshirikisha viongozi wa serikali na CCM. Nakumbuka mshtuko wa serikali na CCM siku ilipogundulika kuwa si raia - kwa aibu alipewa masaa kuondoka nchini.

- Sawa sawa, lakini wekeni more info basi, maana binafsi ninazoziona so far bado ninaziona kuwa ni too strong kwa huyu kijana kuwa mgeni na sio raia, binafsi nimeishi Bunazi yaani Kagera Sugar pale sio rahisi kujua raia na asiye raia ni nani, kuanzia majina, mpaka tabia lakini kwa baba yake huyu Mukasa mpaka kufikia kua ofisa mkubwa serikalini na hata siku moja haikutokea malalamiko kwamba huenda ni foreigner ninashindwa kuamini!

- Anyways, leteni dataz zaidi wakuu, ili tuachane na speculations maana so ndicho kinachofanyika ni speculations tu kwa sababu ya jina lake tu!

Respect.

FMEs!
 
ALIKOTOKA

Mukasa aliyezaliwa Julai 1970, ni mtoto wa tano kati ya 10 katika familia ya Mzee William Mukasa na Mama Apolonia Mukasa.

Sawa

Alizaliwa katika kijiji cha Rukaragata

Hapa kuna walakini maana Mzee Mukassa amehamia Rukaragata baada ya Kustaafu Hospitali Teule ya Biharamulo. Na baada ya Kuhamia huko hatujawahi kupeleka hongera kwa Mama Apolonia kwa kujifungua, I mean hakuzaa tena.

Na isingekuwa rahisi kwa Mzee Msomi, mweledi juu ya masula ya afya kuzaa at the age of 55 or above.

Kuhusu jina Rwegasira; labda wanajaribu kumsogeza Oscar kwa wahaya maana hili jina haliko kabisa kwenye orodha ya majina ya Kisubi (wenyeji wa B'mulo). Ingekuwa enzi za Marehemu Kabuye (1985 against Maghufuli) angepiga kampeni ya " Abasubi twemanye" (wasubi tujijue).

Katika decade hii Rwegasira ni ukoo unaojidhatiti zaidi maeneo ya Misenyi, kati ya Kanyigo na mtukula (boarder to Uganda)
 
- Mkuu wangu slow down, sheria zetu za uraia zinasemaje nataka tu kujaribu ku-entertain hii idea ya baba yake kuwa foreigner kama incase ingekua kweli?

FMEs!

Mkuu FMES,

Hata kama babake ni Mtanzania bado kijana uraia wake unaweza kuwa na matata hasa yale yatokanayo na kuukana uraia mwingine ufikishapo miaka 18.

Chukulia mfano mdogo; naweza hisi wewe uko USA. Ukiwa na mtoto ambaye kwa kuzaliwa tu USA anakuwa ni Mmarekani. Ukienda TZ baadaye hata kama huyo mtoto hukuwahi kumchukulia huo uraia wa USA. Ni kwamba ikifika miaka 18 lazima aukane huo uraia wa USA hata kama hakuwahi kuwa na passport yake au nini.

Mfano mwingine ni wale watoto ambao walizaliwa UK miaka ya kabla ya 83 na wazazi Watanzania ambao hawakuwa raia wa UK (kwa mfano walikuwa wanafunzi). Huyo mtoto kwa kuzaliwa UK tu tayari alikuwa ni raia wa UK, sasa akienda TZ baadaye anagombea ubunge, kuna jamaa anaweza kusema wewe sio raia kwasababu hakuukana uraia ambao si ajabu hata hakujua anao.

Hapo ndipo wajanja wengi wanapatumia kukwamisha wengine. Nafikiri hiyo sheria ni mbovu na labda ingewabana wale ambao wanakuwa wametumia haki za ule uraia mwingine na sio mtu ambaye hata si ajabu hajui kwamba alikuwa na haki ya uraia mwingine.
 
Samahani kama nimekugusa, But the origin ya Hilo Jina ni Congo Mzee. So when walihamia Tanganyika , I dont know but if we want to pick people names by their origin I think kama ulivyosema hapo nyuma hatutakuwa na Viongozi.

- Naona nitakuwa nimekugusa wewe maana mpaka umeomba samahani bila sababu, duh! kama unamuongelea Job Lusinde I am sorry hana anything to do na Congo, sio yeye wala babu zake absolutely nothing! ingawa pia nimekusikia sana.

Respect.

FMEs!
 
FMES, hiyo CV haithibitishi lo lote kuhusu uraia wake au wa baba yake iwe wa Tanzania au la.
Jenerali Ulimwengu aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya, Mjumbe wa NEC, Kamanda wa Vijana mkoa, na vyeo vingi na bado hakuweza kuthibitisha uraia wake. Huyu asili yake Rwanda.

Madam Madeleine Castico aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu (CCM) Visiwani, Mjumbe wa CC na NEC, Naibu Waziri, naye pia hakuweza kuthibitisha uraia wake. Huyu asili yake Msumbiji.

Bandora (kama sijakosea jina) wa Mambo ya Ndani aliwahi kuwa balozi wa Tz nje, career diplomat na bado alikinyanyua na kwenda kushika uzito Rwanda chini ya Kagame, na kututhibitishia kuwa hakuwa raia wa Tz.

Hiyo ya Mzee Mukasa kuwa Afisa Afya (which could be anything from sanitation officer, meat inspector, etc) siyo CV nzito kabisa ya kuthibitisha u-raia. Hata Chavda ana CV nzito kuliko hiyo (access hadi ikulu) na siyo raia.

Nimeona pia umeepuka katika bandiko lako (copied from UPL-Homepage) kuonyesha kasoro kwa nini jina la Rwegasira halipo katika historia yake, lakini ghafla ni muhimu baada ya kupitishwa kuwa mgombea! Kama halikuwa muhimu kabla katika historia ya family kwanini liwe muhimu sasa?

- Mkuu heshima mbele sana, unasema haya tu yanatosha kumuhumu huyu mgombea kua sio raia wetu?

Respect.

FMEs!
 
ALIKOTOKA

Sawa

Hapa kuna walakini maana Mzee Mukassa amehamia Rukaragata baada ya Kustaafu Hospitali Teule ya Biharamulo. Na baada ya Kuhamia huko hatujawahi kupeleka hongera kwa Mama Apolonia kwa kujifungua, I mean hakuzaa tena.

Na isingekuwa rahisi kwa Mzee Msomi, mweledi juu ya masula ya afya kuzaa at the age of 55 or above.

Kuhusu jina Rwegasira; labda wanajaribu kumsogeza Oscar kwa wahaya maana hili jina haliko kabisa kwenye orodha ya majina ya Kisubi (wenyeji wa B'mulo). Ingekuwa enzi za Marehemu Kabuye (1985 against Maghufuli) angepiga kampeni ya " Abasubi twemanye" (wasubi tujijue).

Katika decade hii Rwegasira ni ukoo unaojidhatiti zaidi maeneo ya Misenyi, kati ya Kanyigo na mtukula (boarder to Uganda)

- Mkuu hukuwepo wakati mgombea anazaliwa, umemjua ukubwani sasa unajuaje ya huko nyuma? Au ulikwepo alipozaliwa?

FMEs!
 
Kwa kadiri unavyofahamu baba yake Oscar alizaliwa wapi Tanzania/Tanganyika?

- Mimi sijui baba yake wala yeye mwenyewe amezaliwa wapi, lakini ninaamini nilichokisoma so far, naamini sheria ya kugombea ubunge iko wazi kama inahitaji kuhakikishiwa alipozaliwa baba wa mgombea, basi huyu bwana atakuwa amejaza, sasa tutafute hizo facts tujadili hili tukiwa na facts, leteni facts wakuu, maana so far tunaongea speculations anayejua baba yake alipozaliwa aseme basi au?

- Ninajadili hii ishu na openmind, kwamba anything is possible, lakini facts kwanza sijaona za kuni-convince kwamba jamaa sio raia!

FMEs!
 
Mkuu hukuwepo wakati mgombea anazaliwa, umemjua ukubwani sasa unajuaje ya huko nyuma? Au ulikwepo alipozaliwa?

Heshima mkuu FMES,
Nikweli sikuwepo pale alipozaliwa, na hata kama ningekuwepo nisingeweza kuelewa nini kilikuwa kinatokea na kukiweka kwenye kumbukumbu maana nilikuwa kichanga kama yeye. Lakini pia sijasema kazaliwa Uganda (Rejea post yangu ya kwanza kwenye huu mjadala) Ninachojaribu kuthibitisha ni uasili wa familia ya Mukassa ambayo ndiyo chimbuko la Oscar, iwapo tu alizaliwa na Wazazi na si kijiji, mji, wilaya wala nchi.

Asante Mkulu.
 
- Mimi sijui baba yake wala yeye mwenyewe amezaliwa wapi, lakini ninaamini nilichokisoma so far, naamini sheria ya kugombea ubunge iko wazi kama inahitaji kuhakikishiwa alipozaliwa baba wa mgombea, basi huyu bwana atakuwa amejaza, sasa tutafute hizo facts tujadili hili tukiwa na facts, leteni facts wakuu, maana so far tunaongea speculations anayejua baba yake alipozaliwa aseme basi au?

- Ninajadili hii ishu na openmind, kwamba anything is possible, lakini facts kwanza sijaona za kuni-convince kwamba jamaa sio raia!

FMEs!

Nakubaliana na wewe. Hata mimi sijaona sababu ya kushtusha isipokuwa ilipodaiwa na watu wa Chadema kuwa baba yake Oscar hakuwa mtanzania. Hivyo, kiukweli kabisa siamini kama Oscar kama Oscar ana kosa lolote la yeye kutokuwa raia isipokuwa aidha kwa kutokujua au kwa wazazi kutozingatia kuwa mtoto wao alitakiwa aukane uraia wa wazazi wake alipofikisha miaka 18.

Hivyo, kama ilivyokuwa kwa Jenerali au wengine Oscar anaweza kujikuta ni majeruhi wa kutozingatia sheria. Yawezekana muda wote huu yeye amekuwa akijitambua na kutenda kama Mtanzania. Hivyo, endapo ataenguliwa kwa kweli itamuumiza sana.

Ndiyo maana swali la msingi haliko kwa Oscar bali kwa wazazi wake. Uraia wa Oscar unategemea uraia wa wazazi wake. Kama wazazi walikuwa ni Watanzania/Watanganyika wakati Oscar anazaliwa basi Oscar ana uraia wa Tanzania na kesi kwishnei! Lakini, kama wazazi wake hawakuwa Watanzania au Watanganyika basi Oscar ana kazi kweli. Ila anachoweza kufanya ni kujitoa kwenye kinyang'anyiro, kuomba uraia na mwakani kugombea tena.
 
Hapa kuna walakini maana Mzee Mukassa amehamia Rukaragata baada ya Kustaafu Hospitali Teule ya Biharamulo. Na baada ya Kuhamia huko hatujawahi kupeleka hongera kwa Mama Apolonia kwa kujifungua, I mean hakuzaa tena. Na isingekuwa rahisi kwa Mzee Msomi, mweledi juu ya masula ya afya kuzaa at the age of 55 or above.

- Mkuu samahani kwa kukukwaza tatizo langu ni haya maneno hapo juu, ninayaona ni unfair kwa Oscar, kwa sababu hukuwepo akizaliwa sasa hujui alizaliwa wapi, huenda alizaliwa hapo wakahama na wakarudi baada ya ku-retire!

Respect.

FMEs!
 
Shukrani kwa elimu maana mmepiga makonde from the fore to the rear, left right, up and down.

Asiyeelewa nani CCM wanaweza kuwa wameshikwa pabaya this time? Ndio itakuwa demokrasia yenyewe.
 
Back
Top Bottom