Biharamulo: Picha ya mtoto akisomea kwenye taa za barabarani

Biharamulo: Picha ya mtoto akisomea kwenye taa za barabarani

Huko kuna kaya umeme haujafika, kibatali kinawashwa wakati wa kula tu, ukipata mwanga kama huo inabidi akasome ili asipoteze muda,
Haujafika vipi wakati hapo inaonekana twn kabisa mana yake hakai mbali na hapo
 
Umetia chumvi nyingi sana Mimi nimeenda bush ndani ndani huko hakuna umeme Ila wakiuza mazao yao wananunua Solar sio wajinga kiasi hicho, na Solar wanazotumia zina Mwanga tu km huu wa TANESCO

Unaamini kila kaya ni wakulima? Uliwahi kufika vijiji kama Njelenje huko mbeya ukaona kama kaya zote zina sola?
 
Unaamini kila kaya ni wakulima? Uliwahi kufika vijiji kama Njelenje huko mbeya ukaona kama kaya zote zina sola?
Hao elimu ya Solar itakua haijawafikia au wanaongozwa na Viongozi mizigo wasiojua kutatua changamoto za wananchi wao,
 
Afadhali huyo enzi hizo watu walisomea mbalamwezi, Yani mbalamwezi ikitoka ndo msuli isipotoka ujue umekwisha, usiulize kipindi cha giza watu walisoma vipi.
 
Umeme kufika katika kijiji au mji haimaanishi kila kaya au nyumba imefanikiwa kuvuta huo umeme
Unataka Serikali ikufungie umeme bila wewe kuomba ? Au umemaanisha nini kwa maelezo yako hayo ?
 
BBi
Picha inasambaa kama moto wa kifuu Africa na duniani ikimuonesha mtoto mmoja mpenda shule akipigia msuli kwenye taa za barabarani hivi majuzi huku akiwa amevalia tisheti ya timu ya taifa ya Tanzania (taifa stars).

Barabara hiyo ambayo haiko busy sana imewekewa taa za barabarani hivi karibuni.

USSR View attachment 2580948

Sent using Jamii Forums mobile app
Biharamulo wadau..
 
Back
Top Bottom