Uchaguzi 2020 Biharamulo - Rusahunga Dkt. Magufuli aikacha Ngara, aelekea Kigoma

Uchaguzi 2020 Biharamulo - Rusahunga Dkt. Magufuli aikacha Ngara, aelekea Kigoma

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Baada ya kufuatilia kampeni za jiwe na kutambua kuwa baada ya Bukoba alielekea Biharamulo, ilitegemewa asingeacha kwenda Ngara ili pia aione barabara ile pendwa ya Rusahunga - Rusumo.

Binafsi kwa makusudi mazima ku share uzoefu nikajiongeza chap chap ili nisisikie tu tokea TBC 1 bali nikamshudie macho kwa macho atakuwa na nini cha kusema popote katika barabara hii. Nikitegemea kuleta mrejesho huru usioegemea vilivyo kwenye matakwa ya Dr. Ryoba. Ikumbukwe kuwa maafisa vipenyo wako kila mahali, nani ajuaye?

Kama mbayuwayu vile, mwamba huyu kufika rusahunga kutokea Biharamulo akala kushoto na magari yake mia kidogo kuelekea Nyakanazi, uelekeo kigoma!

Itoshe kusema, mwamba barabara hii anaijua sana na kimsingi kwa makusudi mazima kaamua kulala mbele! Hana majibu. Barabara hii inamvua nguo vilivyo!

Kingine zaidi ya ukweli huo, pamoja na kuwa nilipanga kuwa mitaa ya hii barabara ya rusahunga - Ngara kabla sana ya mwamba huyu kufika rusahunga, tukaishia kupigwa pini kama yalivyo wakuta wengine kupisha msafara wa jiwe yapata 30km tokea Nyakanazi (junction) atakayopita akielekea Kigoma, hali akiwa hata Biharamulo hajaondoka!

Tumekaa barabarani zaidi ya masaa 3 kwenye sehemu marked X (Nyantakara) 30km kutoka Nyakanazi kusubiri jiwe apite Nyakanazi aelekee kwa raha zake Kigoma kutokea Biharamulo:

IMG_20200917_145856_519.jpg


Lusahunga - Muzani ni kuelekea rusumo. Nyakanazi - kakonko ni kuelekea Kigoma. Nyakanazi - Biharamulo ni 50km. Nyantakara - Nyakanazi ni kama 30km.

Tokea 0600 hadi 0930 yaliporuhusiwa magari kutoka Nyantakara, ni wazi kuwa tumempisha apite Nyakanazi mwamba huyu, kabla hata hajaamka kutokea Biharamulo.

Huyu ndiye mwali wetu anayetegemea kura zetu, ili akipita tumpishe tukiwa standstill 30km away kutoka kwenye junction atakayopita.

Amazing!

Hapa chini ni baadhi ya magari yaliyopigwa pini pamoja nasi leo, kumpisha jiwe tukiwa tumesimana nyantakara:

IMG_20200917_135735_442.jpg


IMG_20200917_135714_082.jpg


Maendeleo hayana chama:

Barabara ya Rusahunga Rusumo mtaji kwa wagombea

Ninawasilisha.
 
Mbona barabara nzuri. Unalalamika nn

Ramani umeiona? Pia kumeelezwa:

"Lusahunga - Muzani ni kuelekea rusumo. Nyakanazi - kakonko ni kuelekea Kigoma. Nyakanazi - Biharamulo ni 50km."

Yote ni mahaba tu? Ama kweli mapenzi upofu!

Amekula left. Hadi kufunga safari kuja huku safari binafsi unadhani ni lelemama?

Barabara ya Rusahunga Rusumo mtaji kwa wagombea

Picha ni nyantakara kuliko X kwenye ramani. Magari yalikopigwa stop.

Barabara inayopigiwa kelele unakula right ukitokea Biharamulo ili uelekee rusumo.

Pia kupo hivi:

Ukarabati kichekesho Rusahunga - Rusumo
 
Mgombea wa ccm pale ngara ameshashinda anasubiri kuapishwa tu so kwenda kule ni kupoteza muda tu chama kwa sasa kimefokasi kwenye maeneo yenye upinzani zaidi

Siyo kuwa huku zile nyimbo za kuwa tumejenga flyover, tumenunua madege, tunajenga daraja la busisi, tunajenga airports zikiwamo za Chatto na msalato, nk haziimbiki kabisa?

Anaimba je huku?

Ukarabati kichekesho Rusahunga - Rusumo

Naamini mgombea kipenzi cha wengi hata kacha kuja huku:

Lissu tembelea Rusahunga - Rusumo haraka iwezekanavyo
 
Lissu ni package toshelezi kabisa kuiongoza hii nchi.

Jiwe ni msanii sana. Nalimfungia safari japo kumwona atakavyojikanyaga:

1. Oooh flyover
2. Oooh SGR
3. Oooh daraja la busisi
4. Oooh tumejenga mabarabara
5. Oooh miundo mbinu
6. Oooh zahanati
7. Nk.

Mbona ghafla kama mbayuwayu?

Si huwa anasimamishwa Kula mahindi? Kanusa upepo mbaya kaamua kula Kona.

Haahaaahaaa.

Unbelievable!

Lissu apange kuja huku. Kimsingi wamevaa Makoti ya suti bila suruali:

Lissu tembelea Rusahunga - Rusumo haraka iwezekanavyo
 
Back
Top Bottom