Bikra ya Mwanamke: Kwanini Lawama Zinaishia Kwa Mwanamke Pekee?

Bikra ya Mwanamke: Kwanini Lawama Zinaishia Kwa Mwanamke Pekee?

Yaan Wew swal lako ni moja tu
Kwanini utongoze?

😂😂😂😂😂
Angalia kwanza mada yangu comment zangu kisha za kwako kaa chini tafakari bila presha halafu jilinganishe

Hilo swali umeshindwa kulijibu ndio maana siwezi kuendelea mbele kwa kuruka step sasa kama umeshindwa inaamaana hatua ya awali nimekutoa TKO
 
Kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, licha ya kupewa ushauri na wazazi, walezi na jamii kuhusu madhara ya kuanza ngono katika umri mdogo, lakini bado wanashawishika.

Swali langu ni hili: Je, ushawishi wa wanaume una nguvu zaidi kuliko malezi, ushauri wa wazazi na walezi?
Kabla ya hapo wanakuaga wabishi sana. Wazazi wanapata shida mno akishapata mtu wa kumpa vichips huko ndio kabisa yani.
 
Chizi tu huyo achana naye. Tangu lini feminist akawa desperate na bikira? Wapo wanawake wameolewa multiple times hao wanaume waliangalia vigezo gani? Mtoa mada bikira walishamchomoa kwa chips mayai sasa kila mwanaume anayempata kigezo ni bikira ndio maana anatoa milio na kupanic hovyo!
Huoni aibu kuendelea kujidhalilisha kwa kuainika akili yako ndogo kiasi hiki?

Ningekua wewe ningenyamanza

Eti kila mwanaume naempata kigezo ni bikra 😅
unachekesha
 
Huoni aibu kuendelea kujidhalilisha kwa kuainika akili yako ndogo kiasi hiki?

Ningekua wewe ningenyamanza

Eti kila mwanaume naempata kigezo ni bikra 😅
unachekesha
Sasa watu wakidai bikira wewe inakuuma nini?
 
Hiyo ni nadra, na umeangalia upande mmoja tu wa hoja. Sisi tunachosema ni kwamba kama watu wawili wameamua kuingia kwenye mahusiano ya kingono kwa hiari yao, basi wawe tayari pia kuwajibika kwa maamuzi yao. Ndiyo maana wengine tunasema aliyetoa bikra ndiye aoane naye, ili kuepusha usumbufu wa baadaye wa kulinganisha mwenza wa sasa na ex au kuishi na kumbukumbu za mahusiano yaliyopita.
 
Umekwepa swali "nani atakubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia?" Ukiambiwa uoe bikira maana yake umuoe kwanza ndipo uchunguze kama anayo au la? Kitu gani kimekushinda kujibu hapo?

sijalikwepa nimelijibu labda tu kama haujanielewa, wewe unajoongelea wewe kama wewe mimi naongelea nchi kama jamii, na kama nchi hapo hakuna mshindi, kwani wanaume hawaoi anayedhibiwa siyo mwanamke kama wengi wenu mnavyodhania bali ni jamii na nchi nzima na ndiyo maana jamii ambayo inajitambua haiwawachii wanawake peke yao bali jukumu ni la wote na wote wanaungana pmj kujaribu kutatua tatizo lkn tanzagiza watu kama wewe mnaamini kwamba kama usipooa au kuanzisha familia basi unamkomoa mwanamke, la hasha, its more complicated than that kwani familia ndiyo inayojenga nchi hivyo kama wewe hauwezi kuona kwa sababu hakuna bikra haumuadhibu yoyote isipokuwa wewe mwenyewe pia na nchi nzima na siyo mwanamke tu kama wengi wenu mnavyodhania ...
 
Kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, licha ya kupewa ushauri na wazazi, walezi na jamii kuhusu madhara ya kuanza ngono katika umri mdogo, lakini bado wanashawishika.
Wanaingia kwenye wakiwa wadogo sio?
Haya wanaingia kwenye mahusiano na akina nani?

Swali langu ni hili: Je, ushawishi wa wanaume una nguvu zaidi kuliko malezi, ushauri wa wazazi na walezi?
Ushawishi wa mwanaume una nguvu ndio kwa sababu anatumia uzoefu wake
Malezi ya watoto pia yana nguvu
Lakini malezi ni pamoja na huyo mwanaume
 
Sasa watu wakidai bikira wewe inakuuma nini?
Umeona imeniuma wapi au nawakumbusha kua nyie hiyo bikra mnayotafuta
Hamstahili maana nyie ni wachafu tu

Mwanamke bikra anastahili mwanaume asiemjua Mwanamke
 
Hiyo ni nadra, na umeangalia upande mmoja tu wa hoja. Sisi tunachosema ni kwamba kama watu wawili wameamua kuingia kwenye mahusiano ya kingono kwa hiari yao, basi wawe tayari pia kuwajibika kwa maamuzi yao. Ndiyo maana wengine tunasema aliyetoa bikra ndiye aoane naye, ili kuepusha usumbufu wa baadaye wa kulinganisha mwenza wa sasa na ex au kuishi na kumbukumbu za mahusiano yaliyopita.
Ilibidi useme hivi tangu mwanzo sio kukimbilia kulaumu Mwanamke

Tena hii hoja yako inafaa kwa binti wa age ya 18+

Lakini chini ya hapo inafaa mwanaume awajibishwe bila huruma
 
Suala la mwanamke kuhukumiwa vikali anapopoteza bikra (au kufanya mapenzi) ikilinganishwa na mwanaume ambaye mara nyingi haonekani kama amefanya kosa kubwa, linatokana na mifumo ya kijamii, kitamaduni, na kihistoria. Hali hii kitaalamu inajulikana kama "Double Standards" (Viwango Viwili vya Maadili).
Zifuatazo ni sababu kuu zinazochangia mtazamo huu katika jamii nyingi:

1. Mifumo Dume na Umiliki (Patriarchy) linasababishwa na Mwanamke kama Thamani: Kihistoria, katika jamii nyingi za kitamaduni, bikra ya mwanamke ilichukuliwa kama "mali" au "alama ya usafi" inayomilikiwa na familia yake (wazazi) na baadaye mume wake.

sababu nyingine ni Heshima ya Familia: Msichana kuolewa akiwa bikra kuliletea familia heshima kubwa na hata kuongeza thamani ya mahari. Mwanaume hakuwa na kigezo hiki cha kimaumbile kilichofungamanishwa na thamani ya familia yake.

Mtazamo wa Kibiolojia na Kudhibiti Uzao Uthibitisho wa Mtoto: Kabla ya kuwepo kwa vipimo vya kisayansi kama DNA, njia pekee ya mwanaume kuwa na uhakika kuwa mtoto ni wake ilikuwa ni kuoa mwanamke ambaye hakuwa amewahi kukutana kimwili na mwanaume mwingine (bikra) na kuhakikisha anabaki mwaminifu.

Unyanyapaa wa Mimba: Mwanamke akifanya mapenzi na kupata mimba nje ya ndoa, jambo hilo linaonekana wazi kwa kila mtu (ushahidi wa kibayolojia), wakati mwanaume anaweza kufanya mapenzi na kusiwe na ushahidi wa haraka wa kimaumbile unaoonekana kwenye mwili wake.

3. Mafundisho ya Kidini na Kimila , hapa utaona Tafsiri ya Maadili: Ingawa dini kuu (kama Ukristo na Uislamu) zinakataza ngono nje ya ndoa kwa wote (mwanaume na mwanamke), jamii mara nyingi imekuwa ikichuja mafundisho haya na kuweka uzito mkubwa zaidi kwa mwanamke.

Malezi ya Wasichana: Tangu utotoni, malezi ya mtoto wa kike yamejaa mafundisho mengi ya kujilinda na kulinda "ustara" wake, wakati mtoto wa kiume mara nyingi anaachiwa uhuru mkubwa zaidi, jambo linalofanya makosa yake kuchukuliwa kwa wepesi.

Sifa dhidi ya Aibu (Social Validation)Ushujaa wa Kiume: Katika tamaduni nyingi zilizopotoka, mwanaume anayeshiriki ngono na wanawake wengi mara nyingi husifiwa kama "mjanja" au "mwanaume kamili" (playboy). Unyanyapaa wa Kike: Kinyume chake, mwanamke anayefanya jambo lile lile au anayepoteza bikra yake nje ya utaratibu uliowekwa huhukumiwa kama "mnyonge", "asiye na adabu", au mwenye tabia mbaya.

​
Jamii imekariri ujinga yaani mwanamke anahukumiwa kwa kutotunza bikra

Huku mwanaume akisifiwa kwa kulala na wanawake wengi

Huu si ni ujinga mkuu?
 
Umeona imeniuma wapi au nawakumbusha kua nyie hiyo bikra mnayotafuta
Hamstahili maana nyie ni wachafu tu

Mwanamke bikra anastahili mwanaume asiemjua Mwanamke
Naishia hapa naona unanipumzikia tu! nikimquote mtu mwingine we potezea tu
 
Kwanza, una ushahidi gani kwamba wanaume huwa hatuwakosoi wanaume wenzetu wanaoshiriki katika kuwatoa mabinti bikra, hasa wale wanaowashawishi wasichana wadogo kingono? Huwezi kuhitimisha kwamba wanaume hawazungumzii suala hilo kwa sababu tu wewe hujaona mijadala hiyo.

Nakumbuka hata hapa JamiiForums, kwenye comments za baadhi ya mijadala, kulikuwa na watu waliowashauri wanaume wenzao wasiwaharibu mabinti ambao hawana mpango wa kuwaoa. Nakumbuka hoja hiyo ilijadiliwa, ingawa siwezi kukumbuka uzi husika. Kwa hiyo, si sahihi kudhani kwamba wanaume hawakemeani kwa sababu tu hukuuona mjadala huo.

Pili, kwa nini tunapozungumzia mahusiano ya kingono, tunachukulia kwamba kila mara mwanaume ndiye anayemshawishi mwanamke au binti? Vipi kuhusu baadhi ya wasichana wanaovutiwa na wanaume wenye uwezo wa kifedha, wanaotamani maisha mepesi kwa sababu ya changamoto za kiuchumi, au wanaoingia kwenye mahusiano kwa maamuzi yao wenyewe? Je, katika kila hali hiyo, tutasema mwanaume ndiye aliyemshawishi?

Ni muhimu kutofautisha kati ya watu wazima wanaofanya maamuzi kwa hiari yao na mazingira ambayo msichana mdogo anadanganywa, anashinikizwa au anatumika kingono na mtu mzima. Hayo ni mambo mawili tofauti, na mtu mzima anapaswa kuwajibika anapomdhulumu au kumtumia mtoto.

Hoja yangu si kwamba wanaume hawana wajibu, bali ni kwamba hatupaswi kuangalia upande mmoja tu wa jambo. Kama tunataka kuzungumzia suala la bikra, mahusiano na ndoa, tuzungumzie pia wajibu wa wanaume, maamuzi ya wanawake, mazingira yanayochangia maamuzi hayo na viwango vinavyotumika kuwahukumu wote wawili.
 
Mpaka hapa nimehitimisha wewe ni mdogo sana kicwani asante kwa kushiriki
Ndio maana nasema ww ni mtupu japo kuwa unajitia ujuaji na kwa ujuaji huu huko kuolewa utakusikia kwenye bomba tu.
Kabla ya kubisha unatakiwa kujiuliza ni kwanini Mungu kamuumba mwanamke na bikra wakati mwanaume hakumpa hiyo bikra nijibu kwanza hilo swali.

Mwili wa mwanamke ni kitu chenye thamani kubwa sana na ndiyo maana sisi waislam huwa tunahimiza mwanamke kujistiri ili mwili huo usionekane hovyovyo tu,mwanamke ukishindwa kutunza mwili wako automatic unakuwa umepoteza thamani yako hata kama una pesa na ww ni msomi kiasi gani.
,Thamani ya mwanamke ipo kwenye mwili wake na ndio maana umeubwa ukiwa mlaini nzuri, unao vutia na kutamnisha.
Na ndio maana mwanamke akisha fikisha umri wa miaka 50 ni ngumu sana kuolewa achana na kutongozwa tu kwa sababu muonekano wake hauvutii tena.
Naww mwanaume ukishindwa kutimiza majukumu yako ndani ya nyumba unakuwa umepoteza thamani yako kama mwanaume.
 
Wanaingia kwenye wakiwa wadogo sio?
Haya wanaingia kwenye mahusiano na akina nani?

Ushawishi wa mwanaume una nguvu ndio kwa sababu anatumia uzoefu wake
Malezi ya watoto pia yana nguvu
Lakini malezi ni pamoja na huyo mwanaume
Sawa, nimekupata. 😂 Lakini hapo ndipo ninapotaka unithibitishie hoja yako. Unaposema ushawishi wa mwanaume una nguvu zaidi kuliko malezi, una ushahidi gani wa kuthibitisha kauli hiyo? Je, unamaanisha kila msichana anayeingia kwenye mahusiano ya kingono akiwa mdogo ameshawishiwa na mwanaume, au unazungumzia baadhi ya matukio maalumu?

Kwa sababu kusema mwanaume anatumia uzoefu wake kumshawishi msichana hakuthibitishi moja kwa moja kwamba ushawishi wake una nguvu kuliko malezi ya wazazi na walezi. Hapo bado unahitaji kueleza msingi wa hitimisho lako.

Vipi kuhusu baadhi ya wasichana wanaoingia kwenye mahusiano kwa maamuzi yao wenyewe, au wanaovutiwa na uwezo wa kifedha wa wanaume na maisha wanayoamini watayapata kupitia mahusiano hayo? Je, katika kila mazingira hayo tutasema mwanaume ndiye aliyewashawishi?

Mimi sikatai kwamba kuna wanaume wanaowadanganya, kuwashawishi au kuwatumia wasichana, hasa walio wadogo. Hilo lipo na ni jambo linalopaswa kukemewa. Lakini kuwepo kwa wanaume wanaowashawishi wasichana hakuthibitishi kwamba ushawishi wa wanaume una nguvu zaidi kuliko malezi, wala kwamba kila msichana aliyeingia kwenye mahusiano ya kingono alishawishiwa.

Kwa hiyo, kabla hatujafanya hitimisho la jumla, naomba uthibitishe msingi wa kauli yako: una ushahidi gani kwamba ushawishi wa mwanaume una nguvu zaidi kuliko malezi ya wazazi na walezi? 😂
 
Ndio maana nasema ww ni mtupu japo kuwa unajitia ujuaji na kwa ujuaji huu huko kuolewa utakusikia kwenye bomba tu.
Kabla ya kubisha unatakiwa kujiuliza ni kwanini Mungu kamuumba mwanamke na bikra wakati mwanaume hakumpa hiyo bikra nijibu kwanza hilo swali.

Mwili wa mwanamke ni kitu chenye thamani kubwa sana na ndiyo maana sisi waislam huwa tunahimiza mwanamke kujistiri ili mwili huo usionekane hovyovyo tu,mwanamke ukishindwa kutunza mwili wako automatic unakuwa umepoteza thamani yako hata kama una pesa na ww ni msomi kiasi gani.
,Thamani ya mwanamke ipo kwenye mwili wake na ndio maana umeubwa ukiwa mlaini nzuri, unao vutia na kutamnisha.
Na ndio maana mwanamke akisha fikisha umri wa miaka 50 ni ngumu sana kuolewa achana na kutongozwa tu kwa sababu muonekano wake hauvutii tena.
Naww mwanaume ukishindwa kutimiza majukumu yako ndani ya nyumba unakuwa umepoteza thamani yako kama mwanaume.
Huenda kweli mimi ni mjuaji na ni kwa sababu najua so hilo halifichi kiwango chako kidogo cha reasoning iliyonayo
Na umeshindwa kabisa kuficha upumbavu ulionao

Sasa rudi juu katizame ulivyokua una m quote cocastic

Utagundua kiwango chako

Asante kwa kushiriki
 
Ya kwamba unajua kuliko mungu aliye kupa bikra wakati kaka yako hajampa hiyo bikra?
Na kwa ujuaji wako utaliwa sana na kuachwa mwisho wa siku hasira unakuja kuzimalizia humu kwa kuwapandishia visukari wanaume.
 
Back
Top Bottom