Bikra ya Mwanamke: Kwanini Lawama Zinaishia Kwa Mwanamke Pekee?

Bikra ya Mwanamke: Kwanini Lawama Zinaishia Kwa Mwanamke Pekee?

Mwanaume atalaumiwa na mwanamke atalaumiwa sababu ya kitu kimoja akili, ila atakaye laumiwa sana yule anaye imiliki sababu kapewa akili na utashi.
Wote wanaweza kulaumiwa tena lawama zaidi ni kwa mwanaume mtu mzima ku mrubuni mtoto tena unakuta wa shule ya msingi

Hivi hapo unataka umbebeshe lawama gani huyo mtoto?
 
Mtoa mada kakusifia kwa huu upumbavu nani atakubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia? Ukiambiwa uoe bikira maana yake umuoe kwanza ndipo uchunguze kama anayo au la?

bado hauelewi na ndiyo maana nasema ni kupoteza muda kujadiliana na watanzagiza anything complex, swali kwako labda, wewe unataka kuoa bikra sawa, lkn nani anacontrol kama mwanaume ni bikra pia i.e anasubiri mpaka wakti wa ndoa? na kama mwanaume "hawezi" kusubiri ina maana ana sex na wanawake ambao hajaoana nao, sasa hiyo bkra itatokea wapi kama kila mwanaume ana-sex hovyo na wanawake wa kwenye hiyo hiyo jamii?

i mean, ni both ways ukitaka mwanamke awe bikra basi kama jamii pia mkubaliane wanaume pia wawe bikra, inawezekana jamii za Christian wali-practice hii sana tu inaitwa abstinence, kwamba wote wawili (mwanamke na mwanume) wanasubiri mpaka siku ya ndoa, lkn tanzagiza ni kinyume chake mwanaume anataka na kutegemea mwanamke "ajitunze" akisubiri huku mwanaume ana free ride kuishi atakavyo kuwa na multiple sex partners, hilo haliwezekani ...
 
Ameongea fact amenyooka kama rula wela makasiriko pembeni ujenge hoja mbali na hapo utaonekana kituko katikati ya watu waliostarabika
Nimemuuliza huyo inaonekana ni mwanaume mwenzangu we wadau wakikuquote unapanick!
 
Wote wanaweza kulaumiwa tena lawama zaidi ni kwa mwanaume mtu mzima ku mrubuni mtoto tena unakuta wa shule ya msingi

Hivi hapo unataka umbebeshe lawama gani huyo mtoto?
Usitafute excuse kutaka kuhalalisha jambo, kila mtu kwa nafasi yake awajibike mzazi awajibike kwenye malezi na mtoto mwenye hiyo tunu ndio anatakiwa yeye kwa akili aliyopewa aitumie kwenye kujizuia mpaka ndoa.
 
Kukomaa kifikra...!!??
Umemshikia bunduki ili akubali..? Au kakubali kwa utashi na kutaka kwake.

Mkuu naelewa sana unachokisema
Kwanini analaumiwa binti mdogo wa umri asieweza kuachambua mambo kwa mapana

Ila anaacwa mwanaume mtu mzima timamu huku akikingiwa kifua kwamba hakumlazimisha binti

Nyie wanaume hamuwezi kukubali kua nyie ni waharibifu wa watoto wadogo?

Under age hawawezi kutoana wao kwa wao? mbona una under estimate mambo mengi kwenye hoja zako? Halafu wa kiume anaweza asiwe na nia ya kumuacha huyo binti aliyemtoa bikra ila binti ndo akamkataa kwa tamaa zake baadae. You should consider all the possibilities unapojadili mada ya aina hii hata kama ww ni feminist.
 
bado hauelewi na ndiyo maana nasema ni kupoteza muda kujadiliana na watanzagiza anything complex, swali kwako labda, wewe unataka kuoa bikra sawa, lkn nani anacontrol kama mwanaume ni bikra pia i.e anasubiri mpaka wakti wa ndoa? na kama mwanaume "hawezi" kusubiri ina maana ana sex na wanawake ambao hajaoana nao, sasa hiyo bkra itattokea wapi kama kila mwanaume ana-sex hobvyo na wanawake wa kwenye hiyo hiyo jamii?

i mean ni both ways ukitaka mwanamke awe bikra bsaikama jamii pia mkubaliane wanaume pia wawe bokra, inawezekana in Christianity ina itwa abstinence, kwamba wote wawili mwanamke na mwanume wanasubiri mpoaka siku ya ndoa ....
Umekwepa swali "nani atakubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia?" Ukiambiwa uoe bikira maana yake umuoe kwanza ndipo uchunguze kama anayo au la? Kitu gani kimekushinda kujibu hapo?
 
Una uwezo mdogo wa kufikiri japo kuwa unajifanya mjuaji.
Mwanaume ana vichache vya kupoteza kwenye ngono hali ya kuwa mwanamke anavyo vingi vya kupoteza.
Na ndio maana nasema kuwa itakuwa mpuuzi ukiacha mlango wazi ukitegemea eti wezi watajizuia kukuibia.
Mwanamke ndo mlango wa zinaa hivyo ili zinaa ifanyike ni razima mwanamke akubali.
Na ndio maana hata ww hujalala na wote walio kutongoza bali umelala na ulio wakubalia kulala nao Ina maana hata hao ulio lala nao ungetaka usingelala nao.
Linapo kuja kwenye suala la ngono faida kubwa ipo upande wa mwanaume hali ya kuwa hasara kubwa Iko upande wa mwanamke.
Mwanaume akilala na ww akakutoa bikra yeye anakuwa hajapoteza chochote ila ww unakuwa umepoteza bikra yako.
Au ukipata mimba mwanaume anakuwa hajapoteza chochote ila ww itakuwa umepoteza vingi kwa sababu hiyo mimba ndo utahangaika nayo miezi 9 na leba utaenda ww na hata ikiwezekana hiyo mtoto utahangaika naye ww wakati huo uliye fanya naye uzinzi yupo anaponda raha.
Katika hali kama hiyo usitegemee mwanaume atajali chochote kuhusu hilo kwa sababu athari yake kwake ni mdogo.
Ww mwenyewe mwenye mwili hujajua thamani ya mwili wako mpaka ukaamuwa kuugawa kwa mtu aufanye anacho taka alafu utegemee mwanaume mlio kutana ukubwa authamini mwili wako?
Mimi au wewe ndiye una ukingo wa kufikiria??
 
Umepima thamani ya mwanamke kwa kupoteza bikra yake wewe thamani yako tunaipima vipi ?
Thamani ya mwanaume inapimwa kwa mfuko wake na uwezo wako wa kutimiza majukumu,lakini thamani ya mwanamke Ina pimwa kwa mwili wake.
 
Nimemuuliza huyo inaonekana ni mwanaume mwenzangu we wadau wakikuquote unapanick!
Wala sipanic mi nimenyooka issue mnataka kubembelezwa

Ukweli siku zote hua mchungu endapo wanaume wote mkifunga zipu zenu na kudhibiti tamaa zenu

Bikra zitakua za ku mwaga
Ila kwa tabia zenu za kurubuni mpaka watoto wa shule acheni kulalama ni matokeo ya metendo yenu
 
Thamani ya mwanaume inapimwa kwa mfuko wake na uwezo wako wa kutimiza majukumu,lakini thamani ya mwanamke Ina pimwa kwa mwili wake.
Mpaka hapa nimehitimisha wewe ni mdogo sana kicwani asante kwa kushiriki
 
WANAUME, NAWAITA NJOOENI KWENYE JAMVI

ANGALIZO: Hapa ukija, njoo na hoja, usije na hisia zako

UTANGULIZI :Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema mwanamke asiye na bikra hastahili kuolewa hastahili kutolewa mahari, abebwe mzobe mzobe mpaka ndoani

Ila nina swali moja kwa hawa wanaume wenye mtazamo huu: Kwani nani anayeondoa bikra ya mwanamke?

Si mwanaume naye anashiriki katika tendo hilo?

Sasa kwanini baadhi yenu mna nguvu nyingi za kuwananga wanawake wasio na bikra, lakini hamna nguvu hizo hizo za kuzungumzia wajibu wa wanaume wanaowashawishi na kuwatumia wasichana wadogo kingono?

Nasema hivyo kwa sababu kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, hawajakomaa vya kutosha kiakili na kihisia
Baadhi yao hudanganywa, hushawishiwa kwa ahadi mbalimbali au hutumiwa na watu wazima wanaotambua vizuri wanachokifanya

Mwisho hujikuta wamepoteza usichana wao

Cha kushangaza ni kwamba, mwanaume anaweza kushiriki katika mazingira yaliyosababisha mwanamke kupoteza bikra halafu baadaye akageuka na kumdharau mwanamke huyo kwa sababu hiyohiyo

Yaani wewe mwanaume ambae hukujitunza ambae unajua kila sample ya kei za wanawake
Unapata wapi nguvu ya kusema nataka mwanamke bikra?

Kwa usafi upi hasa ulionao?
Hao uliwachezea unataka nani ale makombo yako wewe unatafuta fresh?

Nimeingia mtandaoni kutafuta hali ya ukatili kingono kwa wasichani wenye umri mdogo

Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa Tanzania wa mwaka 2024 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana (VACS) asilimia 8.4 ya wanawake waliohojiwa wenye umri wa miaka 18–24 waliripoti kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18

Huu ni utafiti tu ambao wanawake wengine huogopa kufunguka
Lakini naamini wapo wengi zaidi na tunaona kesi nyingi hata hazipelekwi kwenye madawati huishia kumalizwa kwa ngazi ya familia

Wote tunajua haya mambo yapo tena hufanywa na watu wakaribu sana kwenye familia wale wa kuaminiwa na sio watu tu ni Wanaume wenzenu au hata nyinyi wenyewe 📌


Naomba nieleweke sio kwamba wanaume wote wako hivi. La hasha!

Kuna wanaume wanaoheshimu wanawake, wanaolinda watoto na wanaopinga kabisa vitendo hivi


Hoja yangu ni kwa wale wanaume wanaotaka mwanamke awe bikra wakati wa ndoa, lakini hawataki kuzungumzia wajibu wa mwanaume katika kulinda heshima na usalama wa wasichana

Hakuna bikra itatoka bila mwanaume au tuseme baiskeli?

Wanaume kwanini msianze kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kufunga zipu zenu na kuacha kurubuni wasichana kwenye umri mdogo?

Hivi hamuoni kua nyie ndio chanzo kikubwa?

Mwisho; Kama bikra ni kigezo cha thamani ya mwanamke, je thamani ya mwanaume anayeshiriki katika tendo hilo inapimwaje?

Kama mwanamke anatakiwa kuwajibika kwa historia yake ya kimapenzi, je, mwanaume naye hapaswi kuwajibika kwa matendo yake?

Na kama kweli tunataka kupunguza tatizo hili, kwanini tusianze kwa kuhamasisha heshima, uwajibikaji, kutowadanganya wasichana na kutowatumia watoto kingono?

MWISHO WA SIKU, SI UNAWEZA KUMDHARAU MTU KWA JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE ULICHANGIA KULITOKEA?

ShesRise_1 ✋️
Suala la mwanamke kuhukumiwa vikali anapopoteza bikra (au kufanya mapenzi) ikilinganishwa na mwanaume ambaye mara nyingi haonekani kama amefanya kosa kubwa, linatokana na mifumo ya kijamii, kitamaduni, na kihistoria. Hali hii kitaalamu inajulikana kama "Double Standards" (Viwango Viwili vya Maadili).
Zifuatazo ni sababu kuu zinazochangia mtazamo huu katika jamii nyingi:

1. Mifumo Dume na Umiliki (Patriarchy) linasababishwa na Mwanamke kama Thamani: Kihistoria, katika jamii nyingi za kitamaduni, bikra ya mwanamke ilichukuliwa kama "mali" au "alama ya usafi" inayomilikiwa na familia yake (wazazi) na baadaye mume wake.

sababu nyingine ni Heshima ya Familia: Msichana kuolewa akiwa bikra kuliletea familia heshima kubwa na hata kuongeza thamani ya mahari. Mwanaume hakuwa na kigezo hiki cha kimaumbile kilichofungamanishwa na thamani ya familia yake.

Mtazamo wa Kibiolojia na Kudhibiti Uzao Uthibitisho wa Mtoto: Kabla ya kuwepo kwa vipimo vya kisayansi kama DNA, njia pekee ya mwanaume kuwa na uhakika kuwa mtoto ni wake ilikuwa ni kuoa mwanamke ambaye hakuwa amewahi kukutana kimwili na mwanaume mwingine (bikra) na kuhakikisha anabaki mwaminifu.

Unyanyapaa wa Mimba:
Mwanamke akifanya mapenzi na kupata mimba nje ya ndoa, jambo hilo linaonekana wazi kwa kila mtu (ushahidi wa kibayolojia), wakati mwanaume anaweza kufanya mapenzi na kusiwe na ushahidi wa haraka wa kimaumbile unaoonekana kwenye mwili wake.

3. Mafundisho ya Kidini na Kimila , hapa utaona Tafsiri ya Maadili: Ingawa dini kuu (kama Ukristo na Uislamu) zinakataza ngono nje ya ndoa kwa wote (mwanaume na mwanamke), jamii mara nyingi imekuwa ikichuja mafundisho haya na kuweka uzito mkubwa zaidi kwa mwanamke.

Malezi ya Wasichana:
Tangu utotoni, malezi ya mtoto wa kike yamejaa mafundisho mengi ya kujilinda na kulinda "ustara" wake, wakati mtoto wa kiume mara nyingi anaachiwa uhuru mkubwa zaidi, jambo linalofanya makosa yake kuchukuliwa kwa wepesi.

Sifa dhidi ya Aibu (Social Validation)Ushujaa wa Kiume: Katika tamaduni nyingi zilizopotoka, mwanaume anayeshiriki ngono na wanawake wengi mara nyingi husifiwa kama "mjanja" au "mwanaume kamili" (playboy). Unyanyapaa wa Kike: Kinyume chake, mwanamke anayefanya jambo lile lile au anayepoteza bikra yake nje ya utaratibu uliowekwa huhukumiwa kama "mnyonge", "asiye na adabu", au mwenye tabia mbaya.

​
 
Wala sipanic mi nimenyooka issue mnataka kubembelezwa

Ukweli siku zote hua mchungu endapo wanaume wote mkifunga zipu zenu na kudhibiti tamaa zenu

Bikra zitakua za ku mwaga
Ila kwa tabia zenu za kurubuni mpaka watoto wa shule acheni kulalama ni matokeo ya metendo yenu
Yaan Wew swal lako ni moja tu
Kwanini utongoze?

😂😂😂😂😂
 
Kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, licha ya kupewa ushauri na wazazi, walezi na jamii kuhusu madhara ya kuanza ngono katika umri mdogo, lakini bado wanashawishika.


Swali langu ni hili: Je, ushawishi wa wanaume una nguvu zaidi kuliko malezi, ushauri wa wazazi na walezi?
 
Under age hawawezi kutoana wao kwa wao? mbona una under estimate mambo mengi kwenye hoja zako? Halafu wa kiume anaweza asiwe na nia ya kumuacha huyo binti aliyemtoa bikra ila binti ndo akamkataa kwa tamaa zake baadae. You should consider all the possibilities unapojadili mada ya aina hii hata kama ww ni feminist.
Chizi tu huyo achana naye. Tangu lini feminist akawa desperate na bikira? Wapo wanawake wameolewa multiple times hao wanaume waliangalia vigezo gani? Mtoa mada bikira walishamchomoa kwa chips mayai sasa kila mwanaume anayempata kigezo ni bikira ndio maana anatoa milio na kupanic hovyo!
 
Back
Top Bottom