Bikra ya Mwanamke: Kwanini Lawama Zinaishia Kwa Mwanamke Pekee?

Bikra ya Mwanamke: Kwanini Lawama Zinaishia Kwa Mwanamke Pekee?

Sasa unavyosema mimi ninavyo wachokonoa.....? Uliniona wapi na fanya hivyo?
Nimesema kwa sababu naona unashadadia wanaume wanaofanya hayo
Hii methali unaielewa vipi? Hasiye funzwa na ........... hufumzwa na.............
Akiwemo mtoto wako
Husiwaache waliwengu wamfunze mwanao. Umepewa kazi ya kulea lea mwanao, mkuze kimwili,kiroho na kiakili. Ili kesho akili imuongoze aje kufanya maamui juu ya mwili wake na maisha yake.
Haya
Waharibifu mbona wapo wengi mnazungumzia wanaume? Mbona siku hizi kuna trend ambayo nayo inakuwa ya wanawake kuwarubuni watoto wadogo wa kiume au mtoto wa kiume anasikia utamu aharibiwi maisha.
Hawa tutawaongelea siku nyingine hakuna tabu
 
Nimesema kwa sababu naona unashadadia wanaume wanaofanya hayo

Akiwemo mtoto wako

Haya

Hawa tutawaongelea siku nyingine hakuna tabu
Timiza wajibu wako kwa mwanao, dunia haijawahi kuwa na huruma kwa wazembe walio shindwa kuwalea watoto zao.
 
WANAUME, NAWAITA NJOOENI KWENYE JAMVI

ANGALIZO: Hapa ukija, njoo na hoja, usije na hisia zako

UTANGULIZI :Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema mwanamke asiye na bikra hastahili kuolewa hastahili kutolewa mahari, abebwe mzobe mzobe mpaka ndoani

Ila nina swali moja kwa hawa wanaume wenye mtazamo huu: Kwani nani anayeondoa bikra ya mwanamke?

Si mwanaume naye anashiriki katika tendo hilo?

Sasa kwanini baadhi yenu mna nguvu nyingi za kuwananga wanawake wasio na bikra, lakini hamna nguvu hizo hizo za kuzungumzia wajibu wa wanaume wanaowashawishi na kuwatumia wasichana wadogo kingono?

Nasema hivyo kwa sababu kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, hawajakomaa vya kutosha kiakili na kihisia
Baadhi yao hudanganywa, hushawishiwa kwa ahadi mbalimbali au hutumiwa na watu wazima wanaotambua vizuri wanachokifanya

Mwisho hujikuta wamepoteza usichana wao

Cha kushangaza ni kwamba, mwanaume anaweza kushiriki katika mazingira yaliyosababisha mwanamke kupoteza bikra halafu baadaye akageuka na kumdharau mwanamke huyo kwa sababu hiyohiyo

Yaani wewe mwanaume ambae hukujitunza ambae unajua kila sample ya kei za wanawake
Unapata wapi nguvu ya kusema nataka mwanamke bikra?

Kwa usafi upi hasa ulionao?
Hao uliwachezea unataka nani ale makombo yako wewe unatafuta fresh?

Nimeingia mtandaoni kutafuta hali ya ukatili kingono kwa wasichani wenye umri mdogo

Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa Tanzania wa mwaka 2024 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana (VACS) asilimia 8.4 ya wanawake waliohojiwa wenye umri wa miaka 18–24 waliripoti kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18

Huu ni utafiti tu ambao wanawake wengine huogopa kufunguka
Lakini naamini wapo wengi zaidi na tunaona kesi nyingi hata hazipelekwi kwenye madawati huishia kumalizwa kwa ngazi ya familia

Wote tunajua haya mambo yapo tena hufanywa na watu wakaribu sana kwenye familia wale wa kuaminiwa na sio watu tu ni Wanaume wenzenu au hata nyinyi wenyewe 📌

Naomba nieleweke sio kwamba wanaume wote wako hivi. La hasha!

Kuna wanaume wanaoheshimu wanawake, wanaolinda watoto na wanaopinga kabisa vitendo hivi

Hoja yangu ni kwa wale wanaume wanaotaka mwanamke awe bikra wakati wa ndoa, lakini hawataki kuzungumzia wajibu wa mwanaume katika kulinda heshima na usalama wa wasichana

Hakuna bikra itatoka bila mwanaume au tuseme baiskeli?

Wanaume kwanini msianze kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kufunga zipu zenu na kuacha kurubuni wasichana kwenye umri mdogo?

Hivi hamuoni kua nyie ndio chanzo kikubwa?

Mwisho; Kama bikra ni kigezo cha thamani ya mwanamke, je thamani ya mwanaume anayeshiriki katika tendo hilo inapimwaje?

Kama mwanamke anatakiwa kuwajibika kwa historia yake ya kimapenzi, je, mwanaume naye hapaswi kuwajibika kwa matendo yake?

Na kama kweli tunataka kupunguza tatizo hili, kwanini tusianze kwa kuhamasisha heshima, uwajibikaji, kutowadanganya wasichana na kutowatumia watoto kingono?

MWISHO WA SIKU, SI UNAWEZA KUMDHARAU MTU KWA JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE ULICHANGIA KULITOKEA?

ShesRise_1 ✋️
1793113816738.png
 
Bikira inaweza kuondolewa kwa Mchezo wa Kike wa Dama..Muhusika anakuwa hana huo ufahamu..Siku ya Ku du Nyoka anazama Mazima ...Wote Wana kuwa confused
 
Nimeona wengi hawajamuelewa mleta mada,

Issue ni kwamba,kwa kawaida,Mwanamke anatolewa bikra yake na mwanaume,haijalishi walipatana au hawakupatana mpaka ikapelekea huyo mwanamke kupoteza hiyo bikra yake,kwa lugha nyepesi hapa ni kwamba,bikra hiyo imepotea kwa ushirikiano kati ya mwanamke na mwanaume,

Hoja ya mleta mada anauliza kwamba,sasa kwanini lawama ziende kwa mwanamke peke yake?
Nafikiri mjadala upo kwenye hiyo hoja.

Mleta mada kuna sehemu tayari nilishamfafanulia ilo suala. Tuseme tu amechagua kutoelewa. Nilimwambia kwamba kiasili wanaume na wanawake hatuhukumiwi kwa vigezo vinavyofanana kwenye kila kitu.

Vipaumbele vya mwanaume ni tofauti na mwanamke. Saikolojia ya mwanaume ni tofauti na mwanamke. Biological clock ya mwanamke ni tofauti na mwanaume n.k

Sasa hapo kwenye kujitunza nature imechagua kumuhukumu mwanamke, kama ambavyo kuna masuala ambayo anahukumiwa mwanaume lakini mwanamke haguswi mfano umasikini. Mwanamke masikini anaweza kupendwa, kuthaminiwa na akaingia kwenye ndoa akiwa jobless lakini haiwezekani kuwa hivyo kwa mwanaume.

Wanawake sio wajinga wanaelewa hilo suala vizuri kabisa, sema wanachokifanya ni kujaribu kukwepa uwajibikaji tu. Ndio maana hiyo usawa wa kijinsia kwenye historia ya mahusiano mengi wanaupigania hapa, hawawezi kuupigania kwenye kulipa bill wakati na wao wamepewa fursa zote kama mwanaume
 
Waeza kuta wengi wao hawajui kwamba mama zao waliolewa wakiwa sio bikra ila ujuaji na upumbavu wao wanatukana wasio bikra. Tena kama walieza fika mpaka chuo kimasomo

Kama kuna kosa lilifanywa na baba angu haimaanishi kwamba mimi natakiwa kulirudia. Kama kuna kosa lilifanywa na mama angu haimaanishi mimi natakiwa kuoa mwanamke akiefanya kosa kama la mama angu
 
ShesRise_1 hiyo ni nature ndio imeamua hivyo. Tahamani ya mwanaume ipo kwenye mali, thamani ya mwanamke ipo kwenye kujitunza. Nature ina patterns zake ambazo haziitambui feminism. Ni kweli nature inaweza kuwa katili lakini ndio nature hiyo hauwezi kuoingana nayo.

Kwahiyo ambae thamani yake ipo kwenye mali, atafute mali na akikishe amezipata bila kisingizio. Ambae thamani yake ipo kwenye kujitunza, ajitunze na akikishe anaolewa akiwa bikira bila kisingizio
 
Kama kuna kosa lilifanywa na baba angu haimaanishi kwamba mimi natakiwa kulirudia. Kama kuna kosa lilifanywa na mama angu haimaanishi mimi natakiwa kuoa mwanamke akiefanya kosa kama la mama angu
Una pointi, ila litazame kwa dunia ya sasa, mtoto wa kike ana vunja ungo akiwa masomoni na suala la ndoa, serikali inapinga na ni kosa kutembea na binti chini ya miaka 18. Katika kipindi chote hicho mpaka anamaliza sekondari kashakua mtu mzima na pengine ana ndoto za kwenda chuo kikuu, huo mda kwa kujilinda na dunia ya mapenzi hataweza vipi? miaka 20 na zaidi bila kufanya mapenzi. Tafakari
 
Kwa point yako hii wanaume wanapewaje lawama kama mtoa mada anavyojaribu kumbebesha mwanaume mzigo kwa maamuzi ya mwanamke kuhusu mwili wake mwenyewe?
 
Bikira inaweza kuondolewa kwa Mchezo wa Kike wa Dama..Muhusika anakuwa hana huo ufahamu..Siku ya Ku du Nyoka anazama Mazima ...Wote Wana kuwa confused
Kumbe sikujua hili
Kwahiyo huyu nae atalaumiwa pia hakujitunza
 
Mleta mada kuna sehemu tayari nilishamfafanulia ilo suala. Tuseme tu amechagua kutoelewa. Nilimwambia kwamba kiasili wanaume na wanawake hatuhukumiwi kwa vigezo vinavyofanana kwenye kila kitu.

Vipaumbele vya mwanaume ni tofauti na mwanamke. Saikolojia ya mwanaume ni tofauti na mwanamke. Biological clock ya mwanamke ni tofauti na mwanaume n.k

Sasa hapo kwenye kujitunza nature imechagua kumuhukumu mwanamke, kama ambavyo kuna masuala ambayo anahukumiwa mwanaume lakini mwanamke haguswi mfano umasikini. Mwanamke masikini anaweza kupendwa, kuthaminiwa na akaingia kwenye ndoa akiwa jobless lakini haiwezekani kuwa hivyo kwa mwanaume.

Wanawake sio wajinga wanaelewa hilo suala vizuri kabisa, sema wanachokifanya ni kujaribu kukwepa uwajibikaji tu. Ndio maana hiyo usawa wa kijinsia kwenye historia ya mahusiano mengi wanaupigania hapa, hawawezi kuupigania kwenye kulipa bill wakati na wao wamepewa fursa zote kama mwanaume
Hakuna nature hapo sema tu umwinyi wa wanaume wa kiafrica tena baadhi yenu
 
ShesRise_1 hiyo ni nature ndio imeamua hivyo. Tahamani ya mwanaume ipo kwenye mali, thamani ya mwanamke ipo kwenye kujitunza. Nature ina patterns zake ambazo haziitambui feminism. Ni kweli nature inaweza kuwa katili lakini ndio nature hiyo hauwezi kuoingana nayo.

Kwahiyo ambae thamani yake ipo kwenye mali, atafute mali na akikishe amezipata bila kisingizio. Ambae thamani yake ipo kwenye kujitunza, ajitunze na akikishe anaolewa akiwa bikira bila kisingizio
Ujue tunashindwa kuelewana wapi kaka ? Ni baadhi yenu wanaume kuacha kuongelea uharibifu mnaoufanya kwa kisingizio cha nature hakuna nature inayokutuma uka mbikiri mtoto wa under 15 hiyo nature ipo kwenye akili yako pengine
 
Back
Top Bottom