Bila kusema ukweli kuhusu 2020 uchaguzi wa 2025 wengi watasusia

Bila kusema ukweli kuhusu 2020 uchaguzi wa 2025 wengi watasusia

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Nimeona leo kwenye mkutano wa TDC wadau wengi wa vyama na haki. Haya yote ya vikosi kazi vyote havitasaiia chochote kama wadau watafukia yaliyopita bila kuongelea uchaguzi wa 2020.

1. Inabidi yote mabaya yaliyotokea yasemwe na wadau wote kwa uwazi
2. Inabidi wadau wote wakubaliane kurekebisha yale mabaya yaliyotokea

Hii njia ya kikosi kazi ili tu Raisi awe na kitu cha kusema kwamba haya ni makubaliano ya pamoja haitawezekana kwa wananchi. Watanzania wengi wanajua mambo na tofauti ya ukweli na uongo. Hichi kikosi kazi cha sasa hivi ni kama kupoteza muda mpaka pale kwa ujumla pande zote zikakubali makosa kwanza kabla ya kwenda mbele na chaguzi zijazo

Chadema walisusia na kuwaambia Watanzania wasiende kwenye chaguzi tutaona watu wengi hawataona sababu ya kwenda kwenye chaguzi na hili sio nzuri kwa taifa. Raisi Samia kama anafikiria hivi vikosi kazi vitatosha ni lazima ajue bila Chadema upinzani hasa kwa Tanzania Bara ni bure tu. Hapa tunaongelea wadau wasio pungua 35% sasa kama hii ni ndogo na ni ya kuuza waenendelee na maigizo lakini kama kuna nia njema ya marekebisho Rais Samia anza na kubadilisha watu wote waliofanya haya mabaya mfano Tume imepataje barua za wabunge wa viti maalumu kama Chadema wanasema hawajaandika?

Je nani kaandika hiyo barua na kachukuliwa hatua gani? au kama ni chadema wana danganya toeni ushahidi.... wananchi wanaangalia vitu kama hivi sio vikosi kazi vya watu ambao hawafahamiki.

Kuna tofauti na vyeo na watu mfano Ndugai alikuwa na cheo hakuwa na watu na ndiyo maana leo kapotea!

Chadema tuwapende au tusiwapende wana watu tena wengi sana na ni lazima wawe kwenye meza bila hivyo Raisi unapoteza muda
 
Kumbe bado kuna watu wana mpango wa kupiga kura?

Hongera kwao.
 
Serikali ya ccm haisafishiki wakubali waanze moja.

Maridhiano lazima yaanze kutambua nini tatizo.
 

Ahsante kwa bandiko zuri mengi yalitokea ndio sababu hata mitandao ilizimwa siku 6.

Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini chochote kuhusu "uchafuzi mkuu" ule ,

Naona hii TCD sio platform huru bali ni state owned propaganda machinery kama ilivyokua magazeti ya Tanzanite na Jamvi la habari yaliyokua yakitumiwa na Cyprian Musiba, naona Mr Zitto ndio tarumbeta la awamu ya 6 hii kwa namna siwezi kuikubali na ukweli humuweka mtu huru.
 
Kama kuna chama kingine chochote hakichukui ruzuku naomba mnitajie hapa🤔
 
Back
Top Bottom