Bila kutaja miaka yako, tuambie una umri gani

Bila kutaja miaka yako, tuambie una umri gani

Mimi wakati Simba inamchakaza Zamalek nilikuwa form 2
Hapo ndo ulipoanzia kuipenda Simba siyo? au ilikuwa kabla ya hapo?

Mimi nilianza kuipenda Simba SC ile nilipopata akili tu na kukuta Mzee wangu amegoma kunywea chai kwenye vikombe vya plastic vya njano au kijani, akivinasibisha na Uyanga Yanga.
 
Nilikua mtoto enzi za marehem Max na zembwela bado wapo mizengwe

Jumamosi ni siku ya kuangalia ITV maigizo ya kina mzee pwagu, mlopelo na mzee muhogo mchungu.

Nikiwa darasa la nne ilikua nikitoka madrasa asubuhi saa 5 nyumbani nakuta dada zangu wanaangalia marudio ya Jumba la dhahabu ya jini kabula na Basupa channel ya TVT siku hizi TBC

Mziki uliokua una trend ni ule
Hei Hei aloo maaa[emoji445]
Laiti ingekua unanioonaaaa[emoji445]
Vile kila time nakondaa nawazaa[emoji445] Kama kukupata tawezaa[emoji445]
 
Nilizaliwa miaka mitatu baadae Baba wa taifa mwl JK nyerere akafariki[emoji17]
 
Wakati hiyo tamthilia inaonyeshwa kwa mara ya kwanza ITV mimi nipo darasa la pili
images (10).jpeg.jpg
 
Nimetumia mafuta ya Rays both colors Red, Yellow, Green n colourless, nimetumia Sabuni Mbuni....nimekunywa juice ya kuwekwa kwenye chupa za soda with yellow colors na chupa zaoshwa tena....nimekula mihogo ya mwamba mmoja anaitwa KaziBure hapo Makumbusho....nimecheza mpira hapo Makumbusho Stand, kulikuwa na Kinyozi wa kutumia kitana hapo Makumbusho chini ya mwembe....nimeangalia Sana movie hapo Makumbusho ofisi za Thithiem.

Mzee Hashimu Rungwe ndo Car dealer at his best hapo Makumbusho...alikuwa na mtoto mkali balaa....gari zake nyingi za kimarekani ZILIKUWA kwenye showroom zake 😂

What else aaah ok nimelipa nauli sh 50...
Funny thing niliokota remote universal nilizima Sana TV za jirani 😂😂
 
Enzi zetu unapika ugali jiwe ila unakula mvuke nchi imetoka mbali hii jamani vijana vijiweni wanakwambia vita ije tuu tuwekane sawa nawachoora kwa mbali halafu nacheka sana kwa dharau
 
Back
Top Bottom