Bila kutaja miaka yako, tuambie una umri gani

Bila kutaja miaka yako, tuambie una umri gani

Disko toto , wavulana tunalipa 300 tshs, wasichana bure.

Wakubwa (me) 1000 wanawake bure
 
Ulanzi (mtogwa) ilikuwa ndio soda kwani ilihifadhiwa kwenye chupa za soda... tulinunua kwa senti....kamwene nyelaga...
 
Dah!!! Ila maisha bwana!!. Mtu kala chips za 250 halafu anakwambia enzi hizo. Acha nipite tu maana naweza onekana muongo.
 
Nimemaliza chuo kipindi maji ya bakhersa ya viroba almaarufu maji ya kandoro ndio yamepigwa marufuku. Nimeyanywa sana yale maji yalikua yanauzwa Tsh 50 nadhani. Wakati naanza chuo nauli ya daladala ilikua Tsh 150
 
Miaka sita baada ya kumaliza la saba watoto wa shule (msingi na sekondari) wakaambiwa Kama sare ya shule imekwisha wavae 'madurufu' (kitambaa kwa wakati ule kilitumika Kama sanda) pia viatu tulivaa katambuga maana tuliambiwa Kuna kufunga mikanda miezi 18 ikapita basi wengi tuligeuka wamasai na watani zangu wagogo na viatu vyetu tunakatiza mitaa ya posta na hakuna anayekushangaa, Moro Shoes ikatuokoa. Ahsante Mzee Ruksa ukatuokoa.
 
Niliandikishwa darasa la kwanza shule ya serikali kwa ada ya 2,400 hizo mia nne zilikua ni kwa ajili ya nembo unapewa nembo mbili hiyo 2,000 sijui ilikuwa ni ya nini

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom