Quran huwezi ielewa kwa kusoma Aya moja tu. Lazima uangalie Aya zilizotangulia na zinazofuatia zinazungumzia maudhui gani! Kwa mfano ukisoma ukisoma Aya ya 4 ya sura ya 107/ suuratil maauun. Allaah anasema:
فويل للمصلين.
(Adhabu kali itawapata wenye kuswali)
Unaweza elewa kuwa kuswali ni dhambi na wanaoswali wataadhibiwa na Allaah siku ya kiyama.
Na mtu anaweza tetea hoja hii kwa kusema kwamba Aya Iko wazi kwamba ADHABU KALI ITAWAPATA WENYE KUSWALI au OLE WAO WENYE KUSWALI!.
Lakini ukiunganisha Aya hiyo na Aya inayofuata
الذين هم عن صلاتهم ساهون
"Wale ambao wanazipuuza swala zao ndio utagundua kwamba makusudio ya walengwa katika aya ya nne ni kundi maalumu ya watu wanaoswali bila kuchunga tarafibu za swala kama alovyoelekeza Mtume صلى الله عليه وسلم.
Sasa wewe unapong'ang'ania Aya moja bila kuangalia Aya zilizotangulia ni dalili ya ulimbukeni na uzumbukuku wa kujitia ujuaji wa mambo usiyoyajua!