GE2025 Bila Tundu Lissu Kuachiliwa na CHADEMA Kuruhusiwa, uhalali wa Rais Samia Suluhu utahojiwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,256
Reaction score
44,597
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kesi za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria.

Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
 
Huwezi kuhalalisha haramu.
Ninavyofahamu CDM hawapo tayari kuingia kwenye uchaguzi na kiongozi wao ameenda mbali na kutaka kuukwamisha uchaguzi na kwa kinywa chake akikiri kuwa mhaini.
Mzee Mwanakijiji unataka kuweka precedence kwamba nchii hii uchaguzi maana yake ni ushiriki wa Chadema tu??

By the way Sidhani kama kuna Utawala haujawahi kuhojiwa au kutiliwa mashaka au kushutumiwa.kwa kuwa hii ni haki ya msingi ya kikatiba.
Haiwezekani kusimamisha uchaguzi kwa maoni na maslahi ya Tundu lissu halafu ukaacha matamanio ya watanzania zaidi ya milioni 60.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kisa za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria. Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
Duuuuu hivi upo mkuuu?? Basiii sawaaa
 
TAL angegombea vipi wakati aliweka msimamo wa no reform no election? Hata angelikuwa hajafungwa asingegombea maana huo ndio msimamo wa chama na ndio maana CDM hakuna mgombea yoyote mpaka sasa si rais, ubunge wala udiwani. Kesi aliyo nayo haina mahusiano na chadema kutoshiriki uchaguzi, waliamua kwa hiari ya kutoshiriki na ndio ikasababisha mgawanyiko kati yao na kuzaa G55, hujayaona hayo?
 
Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kisa za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar
Natamani wanangu wasisome, taaluma ya sheria imevuliwa nguo kabisa na kuonekana ni taaluma ya kipumbavu kuwahi kuwepo duniani. Unamuangalia yule wakili wa serikali na jinsi hakimu anavyojipa u_serious fake unaishia kusema "masaburi" yao hawa.
 
Ni lini walijali uhalali au kuogopa kuhojiwa (na nani wa kuwahoji)? Ukitaka Precedence ya wasivyojali kawaulize CUF kule Zanzibar na Matokeo ambayo kila mtu alikuwa anajua kwamba ni Maalim ndio alikuwa Anashinda....: Mambo yatabadilika huko Mbeleni sana na hata CCM kuja kivingine ila kwa sasa bado wapo wapo Sana...
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kisa za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria. Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
Siyo kwamba Rais Samia anaweza kushinda uchaguzi ujao.

Ni kwamba, Rais Samia atashinda uchaguzi ujao.

That’s a foregone conclusion.

Everything is stacked in their favor right now.
 
(external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa)
Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa Polisi na wenzake wamemwambia kuwa ENDAPO Lissu atagombea na chama chake kushiriki uchaguzi basi POLISI hata wakiiba kura na kuwa-harass kiasi gani wapinzani bado CCM hawataweza kutoboa. Kwahio, the only option ni kuhakikisha kuwa CHADEMA inadhibitiwa iwe kihalali au kipumbavu (kama ilivyo sasa)
 
Umepiga kwenye mshono, CCM kwa ujumla.wao wate wanamwogopa TAL Ni ukweli mtupu Lissu akisimama na Samia, aisee mama za kinzazibari ataambulia manyoya tu mwisho.wa siku. TAL ataachiwa miezi kadhaa baada ya Samia kuapishwa, ataachiwa huru baada ya mchakato wa Katiba mpya kuanza.
 
..Na wakimuachilia TAL wakati wa mchakato wa Katiba umeanza bado atakuwa na sauti kubwa na ata influence mchakato mzima.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenmkongwe ye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kisa za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria.

Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
Mkongwe wa jf. Huwa tunawamiss sana. Kama wao ndani ya chama hawajiamini kiasi cha kupindusha kanuni zao unadhani wataruhusu mropokaji Lisu aingie barabarani? Kumuachia Lisu aingie barabarani na huo mgawanyiko wa ndani ya chama mama hatafika hata misa ya kwanza. Nionavyo mimi Lisu ataachiwa pale baada ya mama na genge lake kujihakikishia kiti. Hiyo ni baada ya oktoba 29 na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom