GE2025 Bila Tundu Lissu Kuachiliwa na CHADEMA Kuruhusiwa, uhalali wa Rais Samia Suluhu utahojiwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kuna watu walitakiwa kuishia kuwa walinzi,msekretary, wafagia ofisi, walitakiwa kuwa wauza genge, au wasimamizi wa maghala ya nafaka.

Ila kwasababu watu wenye Hekima walichagua kukaa kimya na kupuuza sampuli hii ya watu wa kawaida kabisa kupenyezwa na kupewa mamlaka kubwa ,leo tunavuna matokeo ya kuzembea.

Mkulima asipokuwa mkali na shamba lake na kucheza na nyani ,watamaliza mazao yote na yeye ndie atabeba hasara.

Watolewe. Hakuna namna.
 
Mkubwa heshima yako umemaliza hapa uhalali watakosa ila TAL ndio game changer wa hizi siasa tumelishwa sana viini macho kwenye siasa za upinzani kwa muda wote kumbe tawala ndio wana rule kote kote nakuamua nani akae wapi ila ile January 21 ndio zilipozaliwa siasa za upinzani tunaelekea pazuri
 
Mzee Mwanakijiji na wengine wenye mawazo kama yako, mwaka huu 2025 HAKUNA UCHAGUZI MKUU unless electoral reforms zimefanyika. Maana yangu ni kuwa, hata kama reforms zikifanyika, then, kwa mwaka huu 2025 ni ngumu kufanyika uchaguzi...!!

Lakini lililo kubwa zaidi, Bi Samia Suluhu Hassan (mwanamke na Mzanzibari toka taifa la ZANZIBAR) HAWEZI KUWA RAIS WA TANGANYIKA tena iwe mwaka huu, au 2026 au wakati mwingine wowote ujao...!

Msitishwe na maandalizi yoyote ya hiki kinachoitwa "Uchaguzi mkuu 2025...."

Na msitishwe na kuaminishwa na mbwembwe zozote zinazoendelea sasa kufanyika kuchagiza tendo hili haramu ambalo Mungu hataliruuhusu kufanyika tena...

Chukua na amini hii👉🏻👉🏻: Kila kitu kitazimika ghafla kama kibatari kilichokuwa ktk chumba tulivu lakini upepo mkuu ukavuma kutoka kusikojulikana na kukizimisha kibatari hicho fyuuuu...!!
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kisa za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria.

Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
THE FALL OF CCM 1995-2025.✍️📌
 
Huwezi kuhalalisha haramu.
Ninavyofahamu CDM hawapo tayari kuingia kwenye uchaguzi na kiongozi wao ameenda mbali na kutaka kuukwamisha uchaguzi na kwa kinywa chake akikiri kuwa mhaini.
Mzee Mwanakijiji unataka kuweka precedence kwamba nchii uchaguzi maana yake ni ushiriki wa Chadema tu??
Mkurupuko ukisikia neno chadema tu kunyeleo kinapwita
Hujaelewa.
Kuna uhaini unaofanywa na mtu mmoja? Yaani mtu apange uhaini dar mbele ya media aachwe akalale kwake regeta atoke tegeta akakamatiwe mbinga?
 
Utahojiwa na nani, TEC?!!! Hao inafahamika mbona kuwa hawamtaki.
 
Hao CHADEMA wako kama kambale, Bwawa likikauka hupotea mvua zikinyesha Hawa hapa. Amini amini nawambia makomredi kesho Tundu atoke harafu watu watangaziwe atakuwa uwanja wa taifa, uwanja utajaaa , Yaani tumemkuza mno tume mpa promo ndani na nje ya nchi
 
Mkurupuko ukisikia neno chadema tu kunyeleo kinapwita
Hujaelewa.
Kuna uhaini unaofanywa na mtu mmoja? Yaani mtu apange uhaini dar mbele ya media aachwe akalale kwake regeta atoke tegeta akakamatiwe mbinga?
Nilishawahi kutoa mifano ya watu waliohukumiwa kwa uhaini wenyewe...acha mihemko.
By the way kesi inaendelea na mahakama itatoa majibu uoga wa nini?
 
Huwezi kuhalalisha haramu.
Ninavyofahamu CDM hawapo tayari kuingia kwenye uchaguzi na kiongozi wao ameenda mbali na kutaka kuukwamisha uchaguzi na kwa kinywa chake akikiri kuwa mhaini.
Mzee Mwanakijiji unataka kuweka precedence kwamba nchii uchaguzi maana yake ni ushiriki wa Chadema tu??
Unaweza kumtafutia Lissu Kesi nyingine lakini siyo Uhaini, hajawahi kuwepo Mhaini mmoja tu (Fanya kuuliza uelimishwe)

Kingine ni hiki, Bila Chadema hakuna uchaguzi.
 
TAL angegombea vipi wakati aliweka msimamo wa no reform no election? Hata angelikuwa hajafungwa asingegombea maana huo ndio msimamo wa chama na ndio maana CDM hakuna mgombea yoyote mpaka sasa si rais, ubunge wala udiwani. Kesi aliyo nayo haina mahusiano na chadema kutoshiriki uchaguzi, waliamua kwa hiari ya kutoshiriki na ndio ikasababisha mgawanyiko kati yao na kuzaa G55, hujayaona hayo?
Kwani ukisema no reform No Election ndio unatakiwa upewe kesi ya uhaini? Uzuie mikutano ya kisiasa ya chadema? Hivi ushindani hapo utatoka wapi? Watanzania tunafanywa wajinga sana Mimi ni CCM lakini siasa za kijinga namna hii siziungi mkono.
 
Back
Top Bottom