GE2025 Bila Tundu Lissu Kuachiliwa na CHADEMA Kuruhusiwa, uhalali wa Rais Samia Suluhu utahojiwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kisa za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria.

Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
Atakae chaguliwa atakua rais wa 10% ya watz achana afrika na Dunia, hivi chwa wanaelewa hili kweli au wapo tu kama mazombi kwamba October wanatiki, ila watatikiwa pia asema Bwana
 
Kwakweli Walifanya kosa kubwa la kimkakati. Hawakujua haya
 
Si itajulikana ndio maana tunayo mahakama.
Mnataka tuwe na Taifa ambalo mtu akiamka asubuhi anaweza kuzua taharuki na kutokana na umaarufu wake aachwe tu.
Presumably ametenda kosa na ni lazima mahakama ihusike kuthibitisha au vinginevyo.
Ukitaka kuruka agana na nyonga...waswahili husema.
Wakati annanzisha harakati za kuupinga uchaguzi lazima alikuwa na Uelewa kuwa haitakuwa rahisi ,CCM au Serikali isingeweza kukubali na ni lazima ingemdhibiti...sasa plan B yake kichwani ilikuwa ni hii ya kutaka sympathy??
Kuhusu vyama vidogo kuingia kwenye uchaguzi ni haki yao na tukumbuke hata chadema ilikuwa ndogo sana for the past 20 years...na ilikuzwa na sisi wananchi baada ya kuiona CCM ikitaka kutekwa au kuacha njia yake..
Chadema pia ilikuzwa na itashushwa na wananchi walewale...na hapa sababu ni moja tu ...kutaka madaraka kwa njia ya ukorofi itakayoliacha taifa katika mgawanyiko.
Ilikuwepo NCCR ya Mrema
Ilikuwepo CUF ya Maalim
Ilikuwepo Chadema ya Mbowe
Sasa inaanza ACT ya Zitto na Chauma ya Salum Mwalimu.
Kamwe tusitake kuitisha mifumo ya kidemokrasia kwa mgongo wa Taasisi moja.
UPINZANI WA KWELI UTATOKA NDANI YA CCM ...Iliwahi kusemwa lakini bado sana kwa kuwa CCM imeendelea kuicheza karata yake vyema hadi sasa.
CCM inautambua mtandao wa kimaslahi sio leo tu bali toka enzi za Nyerere na kwa miaka yote imeendelea kuudhibiti bila kuyumbisha Taifa.

..Ccm ndio wanaozua taharuki kwa kudai kuna uhaini wakati hakuna.

..tusipoteze muda na rasilimali za mahakama kwa mambo ya kijinga.

..haiwezekani watu wafungue kesi kwa sababu wamezidiwa hoja na wanajisikia kuwatesa wapinzani wao.
 
Kwa mazingira ya sasa hata ashindane na Nani, ‘atashinda’ tu.

Hivyo, kwa mazingira ya sasa, hakuna maana yoyote ile kushiriki katika uchaguzi wowote ule.
Endeleeni kugoma kushiriki msubiri nyakati zijazo. Tanzania haijawahi kuamini kwenye kikundi flani ndio kisikilizwe wao tu kuliko wengine. Haiwezekani.
 
..Ccm ndio wanaozua taharuki kwa kudai kuna uhaini wakati hakuna.

..tusipoteze muda na rasilimali za mahakama kwa mambo ya kijinga.

..haiwezekani watu wafungue kesi kwa sababu wamezidiwa hoja na wanajisikia kuwatesa wapinzani wao.
Kesi imefunguliwa kwa sababu kuna mtanzania mwenzetu anataka kupoka haki yetu ya kupiga kura.
Inakuwaje utake kuzuia uchaguzi wakati tupo tunaohitaji kupiga au kupigiwa kura?Is this democracy?
 
Huwezi kuhalalisha haramu.
Ninavyofahamu CDM hawapo tayari kuingia kwenye uchaguzi na kiongozi wao ameenda mbali na kutaka kuukwamisha uchaguzi na kwa kinywa chake akikiri kuwa mhaini.
Mzee Mwanakijiji unataka kuweka precedence kwamba nchii hii uchaguzi maana yake ni ushiriki wa Chadema tu??

By the way Sidhani kama kuna Utawala haujawahi kuhojiwa au kutiliwa mashaka au kushutumiwa.kwa kuwa hii ni haki ya msingi ya kikatiba.
Haiwezekani kusimamisha uchaguzi kwa maoni na maslahi ya Tundu lissu halafu ukaacha matamanio ya watanzania zaidi ya milioni 60.

Acha lutopoka!!

Matamanio ya wananchi milioni 60 ni kutaka nvhi iendeshwe na mahulumati?

Sema wewe na mashetani wenzako wachache ndio mlioridhia uchaguzi bandia, lakini watanzania walio wengi hawana muda wa kwenda kubariki udhulumaji wa haki.

Kwa uchaguzi huu, Samia hata atatangazwe ameshinda kwa 200%, atabakia kuwa ni kiongozi haramu mbele ya wananchi walio wengi, na yeye atajua kuwa anawaongoza wasiomtaka.

Wengi tulimwunga mkono na kumsigia Rais Samia alivyouanza uongozi, lakini namna alivyoendelea, amekuwa sumu kwa Watanganyika walio wengi.
 
Siyo kwamba Rais Samia anaweza kushinda uchaguzi ujao.

Ni kwamba, Rais Samia atashinda uchaguzi ujao.

That’s a foregone conclusion.

Everything is stacked in their favor right now.
hata ingekuwa wewe ungeshinda bondia mwenzako umemfunga na kamba miguu na mikono na umemfunga kitambaa cheusi usoni ni kwanini usishinde!
 
Natamani wanangu wasisome, taaluma ya sheria imevuliwa nguo kabisa na kuonekana ni taaluma ya kipumbavu kuwahi kuwepo duniani. Unamuangalia yule wakili wa serikali na jinsi hakimu anavyojipa u_serious fake unaishia kusema "masaburi" yao hawa.
Hii ni kwa Tanzania tu,Sheria haina maana tena ,sheria inafanya kazi kwa watu wanaowataka wao tu ,nje ya Tanzania sidhani kama wanasheria wanaweza kusimama na kujisifu kwa taaluma hiyo, ni aibu kwa kweli
 
Huwezi kuhalalisha haramu.
Ninavyofahamu CDM hawapo tayari kuingia kwenye uchaguzi na kiongozi wao ameenda mbali na kutaka kuukwamisha uchaguzi na kwa kinywa chake akikiri kuwa mhaini.
Mzee Mwanakijiji unataka kuweka precedence kwamba nchii hii uchaguzi maana yake ni ushiriki wa Chadema tu??

By the way Sidhani kama kuna Utawala haujawahi kuhojiwa au kutiliwa mashaka au kushutumiwa.kwa kuwa hii ni haki ya msingi ya kikatiba.
Haiwezekani kusimamisha uchaguzi kwa maoni na maslahi ya Tundu lissu halafu ukaacha matamanio ya watanzania zaidi ya milioni 60.
Hata bwege ana akili lakini si kwa ubwege huu
 
Acha lutopoka!!

Matamanio ya wananchi milioni 60 ni kutaka nvhi iendeshwe na mahulumati?

Sema wewe na mashetani wenzako wachache ndio mlioridhia uchaguzi bandia, lakini watanzania walio wengi hawana muda wa kwenda kubariki udhulumaji wa haki.

Kwa uchaguzi huu, Samia hata atatangazwe ameshinda kwa 200%, atabakia kuwa ni kiongozi haramu mbele ya wananchi walio wengi, na yeye atajua kuwa anawaongoza wasiomtaka.

Wengi tulimwunga mkono na kumsigia Rais Samia alivyouanza uongozi, lakini namna alivyoendelea, amekuwa sumu kwa Watanganyika walio wengi.
Watanzania wengi wanathamini kuwa na kitambulisho cha mpiga kura na pia wanajua umuhimu wa kuliga kura.
Pengine zipo fursa zutakazopatikana hapo mbeleni kwa wale walioshiriki kupiga kura je upo tayari kuzikosa?
By the way lawama dhidi ya CCM,Uchaguzi ,Tume ya uchaguzi n.k hazitoisha lakini malalamiko yote yenye mantiki huwa yanafanyiwa kazi na ushahidi upo.Bahati nzuri
wakati Nyerere ,Mwinyi,Mkapa,Kikwete ,Magufuli na Sasa samia wakishutumiwa nimekuwepo kwa hiyo sio jambo jipya na haiwezekani kiongozi au mfumo wa uongozi ukakaa bila shutuma.Hata Yesu alishutumiwa.
 
Huwezi kuhalalisha haramu.
Ninavyofahamu CDM hawapo tayari kuingia kwenye uchaguzi na kiongozi wao ameenda mbali na kutaka kuukwamisha uchaguzi na kwa kinywa chake akikiri kuwa mhaini.
Mzee Mwanakijiji unataka kuweka precedence kwamba nchii hii uchaguzi maana yake ni ushiriki wa Chadema tu??

By the way Sidhani kama kuna Utawala haujawahi kuhojiwa au kutiliwa mashaka au kushutumiwa.kwa kuwa hii ni haki ya msingi ya kikatiba.
Haiwezekani kusimamisha uchaguzi kwa maoni na maslahi ya Tundu lissu halafu ukaacha matamanio ya watanzania zaidi ya milioni 60.
Kwa hiyo kitendo cha Tundu Lissu kuwataka mfanye mabadiliko ya msingi kwenye tume na pia wasimamizi wa uchaguzi ili uwe huru na wa haki, ndiyo uhaini!

Matamanio ya wananchi walio wengi ni kuona kura zao zinaheshimiwa! Na siyo watu wanapiga kura, halafu wasimamizi na tume wanabadilisha matokeo kwa maslahi ya chama tawala!

Na nawaambia kama mtaendelea na huu upuuzi wenu; watu wengi wenye akili timamu hawatakuja washiriki kwenye haya maigizo yenu. Wananchi tulio wengi tuna imani na Lissu kuliko mnavyofikiri. Na hata mumshirikie kwa miaka mingapi! Siku akitoka tu, tutaendelea kumuunga mkono! Na nyinyi mtaishia kuchezea kodi za wananchi ili tu kulazimisha kupendwa.
 
2020 aligombea kupitia katiba na miongozo ambayo haikuwa imeboreshwa.Aliangukia pua na hakufikia alichokifikia Lowassa.
Nini kinakupa hope ya yeye kushindwa mwaka huu ambapo mazingira yameboreshwa?
By the way unatarajia wasimamizi watoke wapi na wateuliwe na nani ili wawe huru kama unavyofikiri?
Nani awezaye kuwa "huru" mbele ya Dola?unaanzaje kufikiri uhuru huo ambao hata USA haupo??
 
Kesi imefunguliwa kwa sababu kuna mtanzania mwenzetu anataka kupoka haki yetu ya kupiga kura.
Inakuwaje utake kuzuia uchaguzi wakati tupo tunaohitaji kupiga au kupigiwa kura?Is this democracy?

..Tundu Lissu anataka mabadiliko yatakayohakikisha uchaguzi huru, wa haki, na uwazi. Mtu wa aina hiyo hana nia mbaya na nchi yetu.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kisa za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria.

Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
Mzee leo umeongea kwa uchungu sana
 
Back
Top Bottom