Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
BILA UZALENDO HATA TUJENGE HOSPITALI AU SHULE KILA KATA, BADO NI BURE.
Anaandika, Robert Heriel
Kukosa miundombinu ya Huduma za kijamii ni tatizo lakini kukosa uadilifu na Uzalendo ni janga kubwa katika mataifa yetu ya Afrika. Nchi yetu inamatatizo mengi Sana lakini yake makubwa ni matatizo ya kitabia. Nchi inawatu wengi wenye saratani ya kitabia.
Ukitaka kujua Jambo hili, nenda hospitalini leo hii utajionea ninachokieleza, sio wafanyakazi wote wenye saratani hiyo, Ila wengi wa watumishi wa umma sio waadilifu na Uzalendo kwao ni kipengele.
Watu hawaipendi nchi Yao.
Watu hawapendani wao Kwa wao.
Watu hawapendi Rasilimali za nchi Yao.
Watu ni wabinafsi kupitiliza!
Ukienda kuhudumiwa, Jambo la Kwanza atakalofikiri Mtoa Huduma ni kuhakikisha anaku-undermine Kwa namna ambayo kivyovyote atahakikisha uwe Duni kwake. Inashangaza na kusikitisha Mno. Jambo hilo analifanya ili kujiwekea ulinzi na kutafuta umuogope ili kuficha udhaifu wake(kama upo). Kisha kunyong'onyeza kujiamini kwako ili ushindwe kupigania Haki zako. Upumbavu tuu!
Na Kwa vile watanzania wengi hawajiamini wamejikuta katika mkondo wenye kina kirefu cha kuonewa na watumishi washenzi wasiowaadilifu. Wamegeuka wanyonge.
Ukichunguza Foleni na misongamano katika mahospitalini mengi sio Kwa sababu Watu ni wengi kupita Kiasi au sio Kwa sababu madaktari au watumishi waliopo NI wachache! Nop! Bali Kwa Asilimia kubwa ni inasababishwa na Watumishi hao kutokuwa waadilifu, hawaanzi kazi Kwa muda, kazi kujizungusha zungusha kijinga, kupiga umbeya umbeya ofisini, unakuta Mtumishi mmoja anamkuta mwenzake anafanya kazi, lenyewe linakuja n Stori za kijinga, hapo zitapotea dakika tano, upuuzi tuu!
Kutoheshimu Watu kunafanya watumishi wa umma kuwanyanyasa Wateja wao. MTU anapokuja ofisini kwako elewa kuwa anashida na hajaja kupoteza muda hapo. Mheshimu. Sio utumie shida zake kumkandamiza. Hizo ni dharau na ushenzi.
Hata kama MTU anamuonekano usiovutia, hata kama MTU ni fukara na Maskini, naheshimu, mhudumie Kwa Moyo wote Kwa sababu ndio kazi uliyoisomea.
Sio ukituona Sisi wavaa Suti au wenye mionekano inayovutia ndio unaleta shobo za kijinga. Huo ni ushenzi.
Kozi karibu zote mmefundishwa Saikolojia ili muweze kuwahudumia Watu vizuri. Kwa nini usivae kiatu cha mteja wako? Vile unavyotaka kufanyiwa basi fanyia wengine vivyohivyo.
Taifa linaweza kuwa na wasomi wengi na miundombinu mingi lakini kama Watu wake wakawa na tabia za kishenzi basi ni Sawa na Bure.
Moja ya Ishara kuwa MTU Fulani sio muadilifu na sio mzalendo ni kupenda na kutanguliza Pesa kuliko UTU. Kuwadharau Watu Kwa mionekano Yao na hadhi zao badala ya kudharau na kuchukia Matendo maovu na Mabaya.
Vijana, mkitaka mfurahie Elimu yenu, kazi zenu basi Taikon nawausia muwe waadilifu. Muwe wazalendo, wapendeni watanzania wenzenu muwapo kwenye Maeneo ya Kazi zenu. Kutokusoma kwao, umaskini wao hauna mahusiano yoyote na huduma mtakayowapa. Acheni kutaka kuogopwa(kulazimisha kuheshimiwa).
Hamkusoma ili muwaonee wasiosoma,
Hamkuumbwa na mvuto ili muwanyanyase wasio na mvuto,
Hamkupata kazi ili muwatese makapuku, fukara na watu chokambaya.
Yaani kitoto kikishafika chuo kinabadilika na kujiona kana kwamba hakistahili kuishi na watu wasiosoma. Eleweni kuwa Sisi ni taifa moja, wapo watakaobahatika kusoma iwe Kwa bahati au juhudi zao, na wapo ambao hawata bahatika kusoma iwe kwa uzembe au vyovyote.
Hallelujah!
Ijumaa Kareem. Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam