Bila Waajemi kuingilia kati, leo hii Syria, Lebanon, Palestina yote na sehemu kubwa ya Misri zingekuwa zimechukuliwa kwa nguvu na Israel

Bila Waajemi kuingilia kati, leo hii Syria, Lebanon, Palestina yote na sehemu kubwa ya Misri zingekuwa zimechukuliwa kwa nguvu na Israel

Kwan wanaotawala Israel ni hao Ashkenazi peke yao chief. Hawa kina marehem Simon Peres Izak Rabin walikuwa Ashkenazi. Kwanini mna ugonjwa uzungufobia.
Nimegoogle Simon peres kazaliwa Poland, unataka kusema nini? Wayahudi wa Poland sio Ashkenazi? Izak Rabin nae Kazaliwa Jerusalem ila wazazi wake ni Migrants toka Ulaya ukimuangalia tu Mzungu. Leta Ushahidi hao ni wayahudi wa Middle East.
 
Hiv wewe unafaham gorilla war ni sawa na vita vya jeshi na jeshi sio. Hao Hamas wangekuwa wanavaa gwanda za jeshi wanakutana live ndio ungeuona mziki. Hata hivyo hao Israel wamejizuia sana maana wangekuwa wanasema waue live hakuna binadamu angebaki hapo Gaza. Hata ukiangalia video za wanajesh wa Hamas wamevaa kiraia wamejificha kwenye makaz ya watu. By the way ushawasikia Hamas wakitangaza wanajesh wao mpaka sasa wamekufa wangap. Ugenius ni pamoja na kuchukua eneo Katikati ya mataifa zaid ya kumi na wote wakakaa sio ishu lelemama kama unavyofikir.
Muajemi peke yake kapeleka vijana wake wakaizunguke Israel inayolindwa na mataifa zaidi ya 10 ya magharibi. Anashambulia Israeli kwa namna anavyojisikia mbele ya mitambo ya kuzuia makombora ya magharibi, na bado anafanikiwa kufikia lengo lake.

Muisrael akishirikiana na magharibi wamejaribu na wao kupambana na muajemi pekee kwa kumuundia vikundi vidogo vidogo pamoja na jeshi la Marekani pale Iraq. Lakini leo hii kwa umoja wao wote wanaomba poo.

Marekani anatafuta njia ya kuikimbia Iraq. Cha kushukuru ni kwa vile Israel haikupeana mpaka na Iran, maana leo hii hao wayahudi wangerudi tena kukimbilia huko huko Ulaya walipotokea. Jamaa hawanaga mzaha kabisa. Muulize Trump alitaka kuwatishia nyau kwa kutuma vijidege visivyo na ruban vikakusanye taarifa za kijasusi, jamaa wakaviunguza vyote na kumpa onyo kuwa chochote kitachosogelea eneo lake kitaunguzwa.

Mpaka Trump anaondoka hakuwahi tena kurudia mzaha ule 😂😂😂
 
Nimegoogle Simon peres kazaliwa Poland, unataka kusema nini? Wayahudi wa Poland sio Ashkenazi? Izak Rabin nae Kazaliwa Jerusalem ila wazazi wake ni Migrants toka Ulaya ukimuangalia tu Mzungu. Leta Ushahidi hao ni wayahudi wa Middle East.
Ushahidi hana yeye anachopambania ni mistari inayosema ukiinariki israel hata katika mambo ya kipuuzi na wewe utabarikiwa.

Watu wa aina hii hata ikitokea vita kati ya Tanzania na Israel wao watakuwa upande wa Israel kuuwa watanzania wenzao.
 
Kuvuka mipaka ya kimataifa kwenda west bank kujenga katika ardhi wanayoambiwa sio yao ndo kujilinda?

Israel ukiiangalia kiramani ni kwamba imeshachukua eneo kubwa la ardhi ya wapalestina. Sasa kuvuka tena kwenda kujenga katika ardhi ya watu ambao mmeshawanyang'anya maeneo yao kitambo nako ni kujilinda? Au mnataka waende wapi na wamezaliwa pale na kukulia pale?

West bank huko wananchi wanaonyang'anywa majumba na viwanja vyao wakiingia barabarani kuandamana ili kuonesha dunia kile kinachoendelea huko Israel inatuma askari na jeshi lenye masilaha makubwa makubwa kupambana na wanyonge wanaoandamana wakiwa na mawe au fimbo. Tena wengi ni vijana wadogo, kina mama na hawa watoto.

Matokeo yake askari wanatumia nguvu kubwa kuzima maandamano kwa kuuwa, kujeruhi, kukamata watu na kwenda kuwafunga bila kuwafungulia kesi nk. Hivi hapa Tanzania watu wakinyimwa uhuru wa kuandamana kutoa ya moyoni wewe utajisikiaje?

Lakini pia serikali ikitumia askari, jeshi lenye silaha za moto kupambana na waandamaji waliobeba mawe na fimbo pia utajisikiaje? Au kwako kunya anye kuku tu, lakini akinya bata eti kaharisha?

Ulikuwepo enzi za mauaji ya Akwilini alieuwawa katika maandamano?
Anachofanya Israeli ni kuchukua ardhi yake aliyoporwa tangu enzi za mababu.
 
Sasa kwanini Sayansi inaonesha Mpalestina wa Leo ndio ana Dna ya Saudi na Suleiman na Yesu? Na hao Mnaowaita wayahudi Dna zao ni sawa na W Ukraine na wengine wa Ulaya Mashariki?

Yaani Yesu aje hilo eneo watu wabadili Dini waweza wakristo, wakae hapo maelfu ya Miaka Leo wanauliwa hao watu na kupotezwa kabisa Duniani huamini kama hao ni wayahudi wa Kale, Ila Wazungu ambao they have Nothing to do With Mashariki ya Kati unaamini ni Wayahudi?
Point yako nini hasa? Kwamba wale magaidi ya Palestine Ndio wayahudi
 
Muajemi peke yake kapeleka vijana wake wakaizunguke Israel inayolindwa na mataifa zaidi ya 10 ya magharibi. Anashambulia Israeli kwa namna anavyojisikia mbele ya mitambo ya kuzuia makombora ya magharibi, na bado anafanikiwa kufikia lengo lake.

Muisrael akishirikiana na magharibi wamejaribu na wao kupambana na muajemi pekee kwa kumuundia vikundi vidogo vidogo pamoja na jeshi la Marekani pale Iraq. Lakini leo hii kwa umoja wao wote wanaomba poo.

Marekani anatafuta njia ya kuikimbia Iraq. Cha kushukuru ni kwa vile Israel haikupeana mpaka na Iran, maana leo hii hao wayahudi wangerudi tena kukimbilia huko huko Ulaya walipotokea. Jamaa hawanaga mzaha kabisa. Muulize Trump alitaka kuwatishia nyau kwa kutuma vijidege visivyo na ruban vikakusanye taarifa za kijasusi, jamaa wakaviunguza vyote na kumpa onyo kuwa chochote kitachosogelea eneo lake kitaunguzwa.

Mpaka Trump anaondoka hakuwahi tena kurudia mzaha ule 😂😂😂
Nilikuwa nakutafuta kumbe chuki za kidini ndio zinakupelekesha. Nilifikir ulikuwa huru kuhusu hoja chief pole. Ndio Dunia hiyo mkuu
 
Point yako nini hasa? Kwamba wale magaidi ya Palestine Ndio wayahudi
1. Sio magaidi ni watu wanaotetea Nchi yao kihalali

2. Yes wao ndio wayahudi Kama ilivyokua proved na Sayansi Kuna studies mbalimbali zimefanyika Havard universities na wanasayansi mbalimbali duniani na studies zote matokeo ni yale yale Dna za Wayahudi wa Zamani ndio hizo hizo Dna za Wapalestina wa Sasa.

View: https://twitter.com/MiroCyo/status/1712258026881921287
 
Huyo kijana mimi nilipogundua kuwa ni mjinga, basi nikamuacha tu abaki na ujinga wake.
Mwenye akili ni wewe mwanaume mzima unajadili ya watu wasiokutambua wakat nchi yako ni majalala. Ungetumia akili kidogo kubadili mawazo ya vijana wenzio we muda wote unajadili watu wapigana paipu huko hiyo ndio akili. Hii ndio miafrica sishangai. Hapo Congo au Darfur Sudan wanakouawa kila siku huna cha kujadili ila wameguswa hao wachumba umeona ndio hoja. Amka Mzee hutambuliwa nao acha kujipendekeza mtoto wa kiume. Waache wauane atakaebaki ndio achukue nchi
 
Nilikuwa nakutafuta kumbe chuki za kidini ndio zinakupelekesha. Nilifikir ulikuwa huru kuhusu hoja chief pole. Ndio Dunia hiyo mkuu
Ukiona mtu anajadili jambo kwa kutanguliza kutaja neno dini hata pale anaejadiliana nae hajalitaja hilo neno ujue huyo mtu ameathiriwa kwa kiwango kikubwa na udini. Hapa ndio kunanifanya nimuelewe vizuri raisi wa China aliezungumzia watu kama wewe ambae ni mpogoro wa ifakara huko unatoka mishipa kutetea watu wasiokujua kwa sababu ya hisia za kidini.

Unaweza kuniambia ni wapi nilipotaja dini ya mtu?

Au umejuaje kama mimi nazungumzia habari za dini na wakati mimi nimetaja nchi?

Mwl Nyerere ashasema mtu anaejadili jambo kwa kutumia kigezo cha dini huyo ujue ameishiwa hoja. Hivyo wewe umeishiwa hoja. Umeshindwa kuwatetea wayahudi kwa utetezi wenye kueleweka umeamua kuja na habari za dini ili kunitoa kwenye point. Kumbe wewe ni kijana wa ovyo kabisa. Ndomaana raisi wa China kakupiga dongo
 
Attachments

  • 13820411_474e176b5f9b4f73a0efd5c863b1537b_jpeg9007ab240faecd3b84b2d425535ccbd1.jpeg
    13820411_474e176b5f9b4f73a0efd5c863b1537b_jpeg9007ab240faecd3b84b2d425535ccbd1.jpeg
    67.3 KB · Views: 2
1. Sio magaidi ni watu wanaotetea Nchi yao kihalali

2. Yes wao ndio wayahudi Kama ilivyokua proved na Sayansi Kuna studies mbalimbali zimefanyika Havard universities na wanasayansi mbalimbali duniani na studies zote matokeo ni yale yale Dna za Wayahudi wa Zamani ndio hizo hizo Dna za Wapalestina wa Sasa.

View: https://twitter.com/MiroCyo/status/1712258026881921287

Huyo hawezi kukuelewa. Yeye ashaaminishwa kuwa myahudi lazima awe mzungu tu 😂😂
 
Mwenye akili ni wewe mwanaume mzima unajadili ya watu wasiokutambua wakat nchi yako ni majalala. Ungetumia akili kidogo kubadili mawazo ya vijana wenzio we muda wote unajadili watu wapigana paipu huko hiyo ndio akili. Hii ndio miafrica sishangai. Hapo Congo au Darfur Sudan wanakouawa kila siku huna cha kujadili ila wameguswa hao wachumba umeona ndio hoja. Amka Mzee hutambuliwa nao acha kujipendekeza mtoto wa kiume. Waache wauane atakaebaki ndio achukue nchi
Kweli chizi sio lazima atembee uchi. Hata kuandika ujinga na pumba nao ni uchizi vilevile. Wewe umejuaje kuwa huwa siandiki hayo yanayotokea Congo na nchi zingine?

Inamaana unataka kila nitakaloandika nije nikwambie kuwa leo nimeandika mada inayohusu Congo, kesho nikwambie nimeandika mada inayohusu Kenya, Sudan nk?

Hata hivyo sio lazima niandike kile unachotaka wewe niandike. Hizo habari za Congo unazosema mbona wewe mwenyewe hukuwahi kuziandika? Kwani wewe sio mwafrika?

Pia sikukulazimisha kuchangia mada yangu, wewe kwa vile hauwezi kuandika mada inayohusu congo, cameron nk, ungetafuta watu wanaoweza kuandika mada ya nchi hizo ili uchangie.

Kijana wa hovyo sijapata kuona hapa JF.
 
I'm sure umekimbilia ku comment bila kusoma thread yote ili kujua kilichoandikwa.
Kwamba nilichokiandika kipo nje Mada?.
Ngoja nirudie tena,"

Let say hii abracadabra uliyoyiandika hapa ni kweli, kuna shida gani Israel kuichukua Misri?.
Ama zama za mwenye nguvu kuchukua chochote zimeshaisha?.
Wao walitumia nguvu kuua wenyeji wa Africa ya kaskazini, why dunia iwaonee huruma wao?*.
 
wenyeji wa africa kaskazini ulikusudia nani ? Mfaransa na Algeria au Mtaliana na Libya ??
 
Ndio nimeamka sorry kwa kuchelewa kukujibu. Iko hiv for reasons kuna vitu vinafanyika kwasababu maalumu kwenye nchi au maeneo tofauti. Nitakupa mfano. Kule kwetu Kilimanjaro kwa mfano miaka ya nyuma ya Nyerere watoto walikuwa hawafaulu mitihan ila walikuwa wanachaguliwa. Yaan mnakuta mmefaulu 30 wanachaguliwa hapo 2 tu. Hiyo nafasi nyingine anapewa watoto mikoa mingine kwa maelezo tuliyopewa na wazee so wazee wengi walikuwa wananunua majina ya watu hasa mikoa mingine ili tu kuwasidia watoto wao kusoma. So serikali ya TZ imefanya huo mchezo live miaka kipind hicho kwa kigezo kwamba hawa wameshasoma wengine nao wasome. Ni kama Mh. magufuli alivyosema wachagga hatupeliki kitu subiri na wenzenu wapate. Na wala hakuna anaelaumu unajua kwasababu gani. Watu washajua ishu hapa ni kujitafuta ukiwa na hela ndio nguvu yako. Ukienda hapo kenya mjaluo ni ndoto kupewa nchi na Nigeria kwa mfano ni ndoto waigbo kupewa nchi. Fuatilia kwanini hajawah kutokea mkuu wa jeshi mchagga au mchagga akitaka urais propaganda zinakuwa nyingi. Serikali inakuwa na sababu zao. Na hizo Mambo zipo dunia nzima Obama mpaka anakuwa rais haikuwa simpo. Ukienda Israel kwenyewe kuna raia waarabu wapalestina. Na kwa utaratibu kila raia wa Israel anatakiwa aingie jeshin na ukishakuwa mjeshi unatakiwa kumiliki silaha. Lakin hawa jamaa wakipewa silaha wote kiusalama pia ni shida pia so wanapewa wachache wengi wanabaniwa. . So kuna kaugumu kwao kupewa silaha pia. So mi sishangai hawa Jews falasha kupunguzwa uzazi labda ongezeko lao kwa mwaka na ardhi ya nchi ni ndogo nk huwez kujua. Ni kama mchina alivyozuia watu wa mjin kuwa na watoto wengi akaruhusu wa kijijin kuwa na wawili by then. Ni sababu za kiusalama zaid sometimes. Shida yetu ni kukariri kosa analofanya mzungu akifanya mwafrica haliwi kosa ni kawaida. Tumekuwa na hofu ya kizungu sana badala ya kujijengea mfumo wa kushindana ulimwengun tumebaki watu wa kuonyesha madhaifu kwa kulalamika tu. Cku zote ukiona mtu hasa mwanaume analalamika jua ni mdhaifu sana. Hii ni dunia ya ushindan nenda front kama unataka kujulikana na kusikika
Kukaa na kuongea au kuchati hakujawah kuleta mabadiliko popote Mzee. Mbona watu wa far east hakuna mwenye muda wa kujadili huu ujinga tumebaki Sisi black kujichelewesha kuongelea ya watu wakat muda hakuna tuna matatizo mengi kuliko huu upuuz unaoendelea hapo middle east. Tumesahau kuwa hapo watu wanapigania ardhi na hiongezeki wenzetu kwasasa hasa wachina wanapenyeza raia wao Africa nzima sasa hiv Mungu akitujalia miaka 40 ijayo wanatutawala tena kutokea ndani. Na hii ni kwasababu hatujui tunataka nini tunafikir kuna watu mahali wanatuonea huruma au wanatupenda ur wrong guys. Mi nafikir ni muda wa kutafakar kwanini Africa tunadharauliwa. Ni kwasababu hatujitafuti tunajishughukisha na ya watu. Niko muda mji mmoja china unaitwa fujiang. Huku ni viwanda tupu. Na wanachotafuta ni soko tu basi. Sasa badala ya watu kutoka kwenda kujitafuta maana Mungu katujalia nchi yetu ipo kwenye engo nzur kibiashara uje ukae na mchina uwe hata agent wa chupi Bongo we ni Iran cjui anapamban upuuz mtupu. Kiufupi hatuna muda wa kupoteza wala huna wa kumlaumu zaid yako. Mwarabu au mzungu akipata we kwake ni choo nothing to them. Ukiona vita popote ni fursa kwa wengine sio ushabiki wa kindez. Mi miaka ya 2012 nimeuza mahind kishenz hapo Juba wakat wanatandikana. mzee nachowaomba pambanen achaneni na biashara za kufuatilia washindan wanaopamban namna ya kuicontrol Dunia. Sisi wala hawatujui. Nimeuza mpunga sana Bujumbura. Na fursa zipo nyingi sana jaman huhitaj kujua kwanini jamii nyingine zinatudharau hii dunia ni kama tuko mbuga za Wanyama. simba ili aishi ni lazima swala wawepo so jitahd ujitafute uwe angalau Chui na wewe uzao wako upate wa kumla aache kulalamika kama wewe.
Humu watu ni anonymous ,unajuaje kuwa huchati na mtu ambaye yuko kwenye biashara/kazi anapambana na maisha kama unavyojinasibu.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Ukiona mtu anajadili jambo kwa kutanguliza kutaja neno dini hata pale anaejadiliana nae hajalitaja hilo neno ujue huyo mtu ameathiriwa kwa kiwango kikubwa na udini. Hapa ndio kunanifanya nimuelewe vizuri raisi wa China aliezungumzia watu kama wewe ambae ni mpogoro wa ifakara huko unatoka mishipa kutetea watu wasiokujua kwa sababu ya hisia za kidini.

Unaweza kuniambia ni wapi nilipotaja dini ya mtu?

Au umejuaje kama mimi nazungumzia habari za dini na wakati mimi nimetaja nchi?

Mwl Nyerere ashasema mtu anaejadili jambo kwa kutumia kigezo cha dini huyo ujue ameishiwa hoja. Hivyo wewe umeishiwa hoja. Umeshindwa kuwatetea wayahudi kwa utetezi wenye kueleweka umeamua kuja na habari za dini ili kunitoa kwenye point. Kumbe wewe ni kijana wa ovyo kabisa. Ndomaana raisi wa China kakupiga dongo
Bro acha makasiriko. Mtoto wa kiume hupaswi kutaja sifa za wanaume wenzio mkuu. Nimekuambia hao watu hawakujui wala hawatakaa wakujue. Watu wenyewe ushasema ni wazungu na waarabu ambao kimsingi ndio walioua na kuwauza Babu zetu. Sasa kama wameshindwa kimaslah wanauana wewe mwafrica unataka nini waache wauawane ni zamu yao kuonja mateso we zungumzia shida ya nchi yako. Mbona hilo liko kirahc sana. Hupaswi kushobokea wanaume Mzee we leta mipango ya hela. Watakuheshimu ukiwa na hela au ubunifu zaid sana we ni kima kwao. Daah cjui nizungumze lugha gan uelewe mkuu. Tunashida nyingi mno hatuna Muda wa kupoteza chief. Na hatuna wa kumlaumu zaid ya kuchelewa kuchukua hatua. Cjui Israel cjui Palestine cjui iran cjui marekan mzee huna utakachopata zaid ya kujilisha upepo halafu baadae unakuja kuwaachia watoto laana kwa kutokukutunza. Ngoja nikupe mfano kidogo labda utanielewa. Unajua Nyerere vita zake zote alizokuwa anapiganisha Africa zilikuwa humanity war. Tumepata nini zaid ya kizazi chake kusifiwa na wengi walishakufa. Sasa kipo kizazi Ukienda South leo hakijui na wala hakitaki kujua hizo Mambo kila cku wanawatimua vijana wetu mitaan na kuwaua. Vita ni biashara mzee tena ya kiume kabisa. Nyerere alivyoteka wale wanajeshi wa libya pale Uganda Gadafi alitaka kumpa mafuta kwa kipind flan kama mabadilishano Mzee akakataa. Na tumetoka vitan tukiwa majalala. Sasa hizo Mambo ni ujinga ishu ni hela na ikiwezekana peleka watoto wakasome huko dunian watuibie teknolijia sio cjui waarabu Israel cjui mzungu cjui iran seriously. Hiv tuko humu humu dunian au tuko likizo. Achaneni na story za kushobokea hawa weupe wametutesa sana ni zamu Yao kuumia. Kama pale Ukraine. Hivyo hivyo.
 
Kwamba nilichokiandika kipo nje Mada?.
Ngoja nirudie tena,"

Let say hii abracadabra uliyoyiandika hapa ni kweli, kuna shida gani Israel kuichukua Misri?.
Ama zama za mwenye nguvu kuchukua chochote zimeshaisha?.
Wao walitumia nguvu kuua wenyeji wa Africa ya kaskazini, why dunia iwaonee huruma wao?*.
Kuuwa hata wakoloni waliwauwa babu zetu kina chief Mkwawa, chief Mirambo, Kijekitile na wengine wengi alafu baada ya kuwauwa wengine wakaondoka na vichwa vyao. Na bado watu weusi, au waafrika waliendelea kuwaamini wakoloni na kuzifuata dini zao walizotuletea ili zitupumbaze.

Mada inazungumzia jinsi waajemi walivyozima njama za baadhi ya mataifa ikiwemo Misri kuchukuliwa. So swala la hao wamisri kuuwa waafrika au wazungu kuuwa babu zetu kina chief Mirambo, Mkwawa nk halikuwa kwenye mada.
 
Humu watu ni anonymous ,unajuaje kuwa huchati na mtu ambaye yuko kwenye biashara/kazi anapambana na maisha kama unavyojinasibu.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
Kupambana na kuwaelimisha wenzio kuhusu yaliyopo na yajayo ni muhim Zaid. Angekuwa anatuletea hiz story kama story za kwenye kahawa kijiwen sawa ila kupoteza nguvu kubwa kuwajadili maadui wetu Mambo yao ni uzwazwa tu.
 
Back
Top Bottom