Kuvuka mipaka ya kimataifa kwenda west bank kujenga katika ardhi wanayoambiwa sio yao ndo kujilinda?
Israel ukiiangalia kiramani ni kwamba imeshachukua eneo kubwa la ardhi ya wapalestina. Sasa kuvuka tena kwenda kujenga katika ardhi ya watu ambao mmeshawanyang'anya maeneo yao kitambo nako ni kujilinda? Au mnataka waende wapi na wamezaliwa pale na kukulia pale?
West bank huko wananchi wanaonyang'anywa majumba na viwanja vyao wakiingia barabarani kuandamana ili kuonesha dunia kile kinachoendelea huko Israel inatuma askari na jeshi lenye masilaha makubwa makubwa kupambana na wanyonge wanaoandamana wakiwa na mawe au fimbo. Tena wengi ni vijana wadogo, kina mama na hawa watoto.
Matokeo yake askari wanatumia nguvu kubwa kuzima maandamano kwa kuuwa, kujeruhi, kukamata watu na kwenda kuwafunga bila kuwafungulia kesi nk. Hivi hapa Tanzania watu wakinyimwa uhuru wa kuandamana kutoa ya moyoni wewe utajisikiaje?
Lakini pia serikali ikitumia askari, jeshi lenye silaha za moto kupambana na waandamaji waliobeba mawe na fimbo pia utajisikiaje? Au kwako kunya anye kuku tu, lakini akinya bata eti kaharisha?
Ulikuwepo enzi za mauaji ya Akwilini alieuwawa katika maandamano?