Bila Waajemi kuingilia kati, leo hii Syria, Lebanon, Palestina yote na sehemu kubwa ya Misri zingekuwa zimechukuliwa kwa nguvu na Israel

Kwan wanaotawala Israel ni hao Ashkenazi peke yao chief. Hawa kina marehem Simon Peres Izak Rabin walikuwa Ashkenazi. Kwanini mna ugonjwa uzungufobia.
Nimegoogle Simon peres kazaliwa Poland, unataka kusema nini? Wayahudi wa Poland sio Ashkenazi? Izak Rabin nae Kazaliwa Jerusalem ila wazazi wake ni Migrants toka Ulaya ukimuangalia tu Mzungu. Leta Ushahidi hao ni wayahudi wa Middle East.
 
Muajemi peke yake kapeleka vijana wake wakaizunguke Israel inayolindwa na mataifa zaidi ya 10 ya magharibi. Anashambulia Israeli kwa namna anavyojisikia mbele ya mitambo ya kuzuia makombora ya magharibi, na bado anafanikiwa kufikia lengo lake.

Muisrael akishirikiana na magharibi wamejaribu na wao kupambana na muajemi pekee kwa kumuundia vikundi vidogo vidogo pamoja na jeshi la Marekani pale Iraq. Lakini leo hii kwa umoja wao wote wanaomba poo.

Marekani anatafuta njia ya kuikimbia Iraq. Cha kushukuru ni kwa vile Israel haikupeana mpaka na Iran, maana leo hii hao wayahudi wangerudi tena kukimbilia huko huko Ulaya walipotokea. Jamaa hawanaga mzaha kabisa. Muulize Trump alitaka kuwatishia nyau kwa kutuma vijidege visivyo na ruban vikakusanye taarifa za kijasusi, jamaa wakaviunguza vyote na kumpa onyo kuwa chochote kitachosogelea eneo lake kitaunguzwa.

Mpaka Trump anaondoka hakuwahi tena kurudia mzaha ule 😂😂😂
 
Nimegoogle Simon peres kazaliwa Poland, unataka kusema nini? Wayahudi wa Poland sio Ashkenazi? Izak Rabin nae Kazaliwa Jerusalem ila wazazi wake ni Migrants toka Ulaya ukimuangalia tu Mzungu. Leta Ushahidi hao ni wayahudi wa Middle East.
Ushahidi hana yeye anachopambania ni mistari inayosema ukiinariki israel hata katika mambo ya kipuuzi na wewe utabarikiwa.

Watu wa aina hii hata ikitokea vita kati ya Tanzania na Israel wao watakuwa upande wa Israel kuuwa watanzania wenzao.
 
Anachofanya Israeli ni kuchukua ardhi yake aliyoporwa tangu enzi za mababu.
 
Point yako nini hasa? Kwamba wale magaidi ya Palestine Ndio wayahudi
 
Nilikuwa nakutafuta kumbe chuki za kidini ndio zinakupelekesha. Nilifikir ulikuwa huru kuhusu hoja chief pole. Ndio Dunia hiyo mkuu
 
Point yako nini hasa? Kwamba wale magaidi ya Palestine Ndio wayahudi
1. Sio magaidi ni watu wanaotetea Nchi yao kihalali

2. Yes wao ndio wayahudi Kama ilivyokua proved na Sayansi Kuna studies mbalimbali zimefanyika Havard universities na wanasayansi mbalimbali duniani na studies zote matokeo ni yale yale Dna za Wayahudi wa Zamani ndio hizo hizo Dna za Wapalestina wa Sasa.


View: https://twitter.com/MiroCyo/status/1712258026881921287
 
Huyo kijana mimi nilipogundua kuwa ni mjinga, basi nikamuacha tu abaki na ujinga wake.
Mwenye akili ni wewe mwanaume mzima unajadili ya watu wasiokutambua wakat nchi yako ni majalala. Ungetumia akili kidogo kubadili mawazo ya vijana wenzio we muda wote unajadili watu wapigana paipu huko hiyo ndio akili. Hii ndio miafrica sishangai. Hapo Congo au Darfur Sudan wanakouawa kila siku huna cha kujadili ila wameguswa hao wachumba umeona ndio hoja. Amka Mzee hutambuliwa nao acha kujipendekeza mtoto wa kiume. Waache wauane atakaebaki ndio achukue nchi
 
Nilikuwa nakutafuta kumbe chuki za kidini ndio zinakupelekesha. Nilifikir ulikuwa huru kuhusu hoja chief pole. Ndio Dunia hiyo mkuu
Ukiona mtu anajadili jambo kwa kutanguliza kutaja neno dini hata pale anaejadiliana nae hajalitaja hilo neno ujue huyo mtu ameathiriwa kwa kiwango kikubwa na udini. Hapa ndio kunanifanya nimuelewe vizuri raisi wa China aliezungumzia watu kama wewe ambae ni mpogoro wa ifakara huko unatoka mishipa kutetea watu wasiokujua kwa sababu ya hisia za kidini.

Unaweza kuniambia ni wapi nilipotaja dini ya mtu?

Au umejuaje kama mimi nazungumzia habari za dini na wakati mimi nimetaja nchi?

Mwl Nyerere ashasema mtu anaejadili jambo kwa kutumia kigezo cha dini huyo ujue ameishiwa hoja. Hivyo wewe umeishiwa hoja. Umeshindwa kuwatetea wayahudi kwa utetezi wenye kueleweka umeamua kuja na habari za dini ili kunitoa kwenye point. Kumbe wewe ni kijana wa ovyo kabisa. Ndomaana raisi wa China kakupiga dongo
 

Attachments

  • 13820411_474e176b5f9b4f73a0efd5c863b1537b_jpeg9007ab240faecd3b84b2d425535ccbd1.jpeg
    67.3 KB · Views: 2
Huyo hawezi kukuelewa. Yeye ashaaminishwa kuwa myahudi lazima awe mzungu tu 😂😂
 
Kweli chizi sio lazima atembee uchi. Hata kuandika ujinga na pumba nao ni uchizi vilevile. Wewe umejuaje kuwa huwa siandiki hayo yanayotokea Congo na nchi zingine?

Inamaana unataka kila nitakaloandika nije nikwambie kuwa leo nimeandika mada inayohusu Congo, kesho nikwambie nimeandika mada inayohusu Kenya, Sudan nk?

Hata hivyo sio lazima niandike kile unachotaka wewe niandike. Hizo habari za Congo unazosema mbona wewe mwenyewe hukuwahi kuziandika? Kwani wewe sio mwafrika?

Pia sikukulazimisha kuchangia mada yangu, wewe kwa vile hauwezi kuandika mada inayohusu congo, cameron nk, ungetafuta watu wanaoweza kuandika mada ya nchi hizo ili uchangie.

Kijana wa hovyo sijapata kuona hapa JF.
 
I'm sure umekimbilia ku comment bila kusoma thread yote ili kujua kilichoandikwa.
Kwamba nilichokiandika kipo nje Mada?.
Ngoja nirudie tena,"

Let say hii abracadabra uliyoyiandika hapa ni kweli, kuna shida gani Israel kuichukua Misri?.
Ama zama za mwenye nguvu kuchukua chochote zimeshaisha?.
Wao walitumia nguvu kuua wenyeji wa Africa ya kaskazini, why dunia iwaonee huruma wao?*.
 
wenyeji wa africa kaskazini ulikusudia nani ? Mfaransa na Algeria au Mtaliana na Libya ??
 
Humu watu ni anonymous ,unajuaje kuwa huchati na mtu ambaye yuko kwenye biashara/kazi anapambana na maisha kama unavyojinasibu.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Bro acha makasiriko. Mtoto wa kiume hupaswi kutaja sifa za wanaume wenzio mkuu. Nimekuambia hao watu hawakujui wala hawatakaa wakujue. Watu wenyewe ushasema ni wazungu na waarabu ambao kimsingi ndio walioua na kuwauza Babu zetu. Sasa kama wameshindwa kimaslah wanauana wewe mwafrica unataka nini waache wauawane ni zamu yao kuonja mateso we zungumzia shida ya nchi yako. Mbona hilo liko kirahc sana. Hupaswi kushobokea wanaume Mzee we leta mipango ya hela. Watakuheshimu ukiwa na hela au ubunifu zaid sana we ni kima kwao. Daah cjui nizungumze lugha gan uelewe mkuu. Tunashida nyingi mno hatuna Muda wa kupoteza chief. Na hatuna wa kumlaumu zaid ya kuchelewa kuchukua hatua. Cjui Israel cjui Palestine cjui iran cjui marekan mzee huna utakachopata zaid ya kujilisha upepo halafu baadae unakuja kuwaachia watoto laana kwa kutokukutunza. Ngoja nikupe mfano kidogo labda utanielewa. Unajua Nyerere vita zake zote alizokuwa anapiganisha Africa zilikuwa humanity war. Tumepata nini zaid ya kizazi chake kusifiwa na wengi walishakufa. Sasa kipo kizazi Ukienda South leo hakijui na wala hakitaki kujua hizo Mambo kila cku wanawatimua vijana wetu mitaan na kuwaua. Vita ni biashara mzee tena ya kiume kabisa. Nyerere alivyoteka wale wanajeshi wa libya pale Uganda Gadafi alitaka kumpa mafuta kwa kipind flan kama mabadilishano Mzee akakataa. Na tumetoka vitan tukiwa majalala. Sasa hizo Mambo ni ujinga ishu ni hela na ikiwezekana peleka watoto wakasome huko dunian watuibie teknolijia sio cjui waarabu Israel cjui mzungu cjui iran seriously. Hiv tuko humu humu dunian au tuko likizo. Achaneni na story za kushobokea hawa weupe wametutesa sana ni zamu Yao kuumia. Kama pale Ukraine. Hivyo hivyo.
 
Kuuwa hata wakoloni waliwauwa babu zetu kina chief Mkwawa, chief Mirambo, Kijekitile na wengine wengi alafu baada ya kuwauwa wengine wakaondoka na vichwa vyao. Na bado watu weusi, au waafrika waliendelea kuwaamini wakoloni na kuzifuata dini zao walizotuletea ili zitupumbaze.

Mada inazungumzia jinsi waajemi walivyozima njama za baadhi ya mataifa ikiwemo Misri kuchukuliwa. So swala la hao wamisri kuuwa waafrika au wazungu kuuwa babu zetu kina chief Mirambo, Mkwawa nk halikuwa kwenye mada.
 
Humu watu ni anonymous ,unajuaje kuwa huchati na mtu ambaye yuko kwenye biashara/kazi anapambana na maisha kama unavyojinasibu.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
Kupambana na kuwaelimisha wenzio kuhusu yaliyopo na yajayo ni muhim Zaid. Angekuwa anatuletea hiz story kama story za kwenye kahawa kijiwen sawa ila kupoteza nguvu kubwa kuwajadili maadui wetu Mambo yao ni uzwazwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…