Bila Waajemi kuingilia kati, leo hii Syria, Lebanon, Palestina yote na sehemu kubwa ya Misri zingekuwa zimechukuliwa kwa nguvu na Israel

Acha uongo Israel alirudisha sinai lakin alikua ameshaichukua
 
Kama wale ni wazungu halisi then wayahudi wenye ardhi yao wako wapi!
Wewe jamaa ni muungwana sana na mara nyingi huwa unafikiri kabla ya kuandika. Hauna mihemko kama baadhi ya wachangiaji wengine wa pande zote mbili yani wakristo na waislamu. Ndomaana toka mwanzo tunajadiliana vizuri. Anyway acha nijibu ulichouliza.

Wayahudi original wapo hapo mashariki ya kati toka miaka hiyo kabla ya 1948. Na wapo katika nchi nyingi tu. Wapo Lebanon, Syria, Misri, Palestina nk. Na walikuwa wanaishi kama wanavyoishi watu wengine, hakuna kubaguliwa wala kuteswa. Wayahudi waleteswa ulaya kama baadhi ya story zinavyosema lakini wa hapo mashariki ya kati hawakuteswa. Inasemekana hata kipindi cha Ottoman empire wao walikuwa na haki sawa na raia wengine kama ilivyo leo Tanzania. Muhindi, mwaarabu, mnyamwezi, mzaramo, mgogo nk wote wana haki sawa, japo maendeleo yanaweza kutofautiana kulingana na upeo wa kabila au jamii husika.

Sasa wazungu haswa waingereza walipogundua kwamba kuna miaka fulani ikifika itabidi watoe uhuru kwa zile nchi wanazotawala moja wapo ikiwa Tanganyika. Ndo wakaanza kutafuta mbinu ambayo itawasaidia kuendelea kunyonya nchi zingine hata baada ya kuzipa uhuru ili kuendesha uchumi wa nchi zao. Waingereza au wazungu waligundua kwamba mashariki ya kati kuna rasilimali nyingi kama vile gesi, mafuta nk. Hivyo ili kuzipata hizo inabidi watafute mbinu mbadala ya kuzifikia. Waliona wakisema watumie njia ya mikataba ya kawaida pekee hawatoweza kupata faida wanayoikusudia. Hivyo ni kutafuta njia ya kuzishika hizo nchi ili iwe rahisi wao kuzipata hizo rasilimali za mafuta, gesi nk bila gharama.

Sasa ili waweze kuingia huko inabidi watafute watu ambao watawatumia kama ngao yao bila wao kuonekana kuwa wapo nyuma ya ngao hiyo. Ndo wakaanza kukusanya wale wayahudi waliokuwa Ulaya ambao historia inasema walikuwa bado ni wanyonge tu hadi kufikia hatua ya kuuwawa kama kuku na Hitler.

Sasa kwa vile wayahudi walisambaa sehemu nyingi ikawa ngumu kujua kuwa huyo ni myahudi original au mzungu kutokana na wengine kuchanga mbegu na wazungu. Yani baba myahudi, baba mzungu, lakini vile vile wana sera inayosema myahudi anaweza kuwa yeyote yule, ndo maana leo kuna mpaka waethiopia kabisa weusi wenzetu lakini ni wayahudi, hivyo wazungu nao wakatumia hicho kigezo kuwa hata ukiwa mzungu pia unaweza kuwa myahudi. Waingereza wakapenyeza wapelelezi wao, askari wao, halikadhalika na Mmarekani na yeye hakutaka kuwa nyuma na yeye akapachika wa kwake na kwenda kuwachomeka huko.

Kwahiyo sera ikawa wale waliotokea Ulaya ndio wanatakiwa waongoze nchi kutokana na elimu yao utaalam wao walioupata kutoka Ulaya nk. Hapo ndo wazungu pia walipopenyeza watu wao katika mifumo ya nchi kwa kisingizio cha elimu ili kukamilisha mission waliokuwa nayo pale Mashariki ya kati. Wayahudi original ambao mpaka leo wapo, hawana usemi wowote kwani ni kama vile wamekaliwa kooni na wale waliotoka nje ambao hela zikiingia za misaada zinaangukia katika mikono yao (wazungu) hivyo wazawa hawana la kufanya as long wanaishi vizuri wanakula na kufanya vibarua vidogo vidogo vya kuwaingizia hela ya kula nk.

Hiyo ndio hali halisi pale Mashariki ya kati.
 
Miaka 3000 ulikuwepo? Au ndo story za kwenye vitabu?
 
Hao unaowaita wazungu wakipimwa DNA na hao wayahudi wa middle east zinaendani
Hivi huko shuleni huwaga mnasomea nini

Wayahudi wameisha ulaya zaidi ya miaka 1500 ila hawakubadilisha tamaduni zao ndo maana hata hitler alipotaka kuwaua ilikua rahisi kuwatambua
 
Israeli ni dola huru na inatambulika kimataifa na pia ina haki ya kujilinda
Kuvuka mipaka ya kimataifa kwenda west bank kujenga katika ardhi wanayoambiwa sio yao ndo kujilinda?

Israel ukiiangalia kiramani ni kwamba imeshachukua eneo kubwa la ardhi ya wapalestina. Sasa kuvuka tena kwenda kujenga katika ardhi ya watu ambao mmeshawanyang'anya maeneo yao kitambo nako ni kujilinda? Au mnataka waende wapi na wamezaliwa pale na kukulia pale?

West bank huko wananchi wanaonyang'anywa majumba na viwanja vyao wakiingia barabarani kuandamana ili kuonesha dunia kile kinachoendelea huko Israel inatuma askari na jeshi lenye masilaha makubwa makubwa kupambana na wanyonge wanaoandamana wakiwa na mawe au fimbo. Tena wengi ni vijana wadogo, kina mama na hawa watoto.

Matokeo yake askari wanatumia nguvu kubwa kuzima maandamano kwa kuuwa, kujeruhi, kukamata watu na kwenda kuwafunga bila kuwafungulia kesi nk. Hivi hapa Tanzania watu wakinyimwa uhuru wa kuandamana kutoa ya moyoni wewe utajisikiaje?

Lakini pia serikali ikitumia askari, jeshi lenye silaha za moto kupambana na waandamaji waliobeba mawe na fimbo pia utajisikiaje? Au kwako kunya anye kuku tu, lakini akinya bata eti kaharisha?

Ulikuwepo enzi za mauaji ya Akwilini alieuwawa katika maandamano?
 
Naam umempa ukweli wake.
 
Acha uongo Israel alirudisha sinai lakin alikua ameshaichukua
Soma vizuri alichoandika jamaa. Punguza kwanza muhemko. Wayahudi wa kizungu huwa hawapiti humu kuangalia ulichoandika, so usiwe na papara.
 
Wewe ulikuwepo hiyo miaka 1500 unayosema au ulisimuliwa na nabii tito
 
Sasa kwanini Sayansi inaonesha Mpalestina wa Leo ndio ana Dna ya daudi na Suleiman na Yesu? Na hao Mnaowaita wayahudi Dna zao ni sawa na W Ukraine na wengine wa Ulaya Mashariki?

Yaani Yesu aje hilo eneo watu wabadili Dini waweza wakristo, wakae hapo maelfu ya Miaka Leo wanauliwa hao watu na kupotezwa kabisa Duniani huamini kama hao ni wayahudi wa Kale, Ila Wazungu ambao they have Nothing to do With Mashariki ya Kati unaamini ni Wayahudi?
 
Haziendani Dna, Wanaoendana Dna ni Mizrahi na Sepharidic Jews ambao walikua ni wayahudi ila wanaishi jamii moja na waarabu.

Hao wayahudi waliokuja middle East karne iliopita Dna zao hazifanani na watu wa Middle East, kwa Baba Dna ni 0 na kwa mama unaitafut kwa tochi labda 3%, huku Africa Kuna watu Wana Dna ya Kiyahudi kubwa kushinda hio Ashkenazi, ndio maana Dna zinakuwa Banned Israel Kupima.
 
Mbona swali langu lilikuwa rahisi tu mkuu? Israel hiyo ya magenius imefanikiwa kwenye lipi kwa nyanja yeyote kuanzia Uchumi, Michezo na Utamaduni?

Huo U-genius mbona umeshindwa maliza vita au hata kuibeba hiyo Gaza jumla jumla miaka na miaka?
Hiv wewe unafaham gorilla war ni sawa na vita vya jeshi na jeshi sio. Hao Hamas wangekuwa wanavaa gwanda za jeshi wanakutana live ndio ungeuona mziki. Hata hivyo hao Israel wamejizuia sana maana wangekuwa wanasema waue live hakuna binadamu angebaki hapo Gaza. Hata ukiangalia video za wanajesh wa Hamas wamevaa kiraia wamejificha kwenye makaz ya watu. By the way ushawasikia Hamas wakitangaza wanajesh wao mpaka sasa wamekufa wangap. Ugenius ni pamoja na kuchukua eneo Katikati ya mataifa zaid ya kumi na wote wakakaa sio ishu lelemama kama unavyofikir.
 
Kwan wanaotawala Israel ni hao Ashkenazi peke yao chief. Hawa kina marehem Simon Peres Izak Rabin walikuwa Ashkenazi. Kwanini mna ugonjwa uzungufobia.
 
1. Hao Jews wa Iraq na wengine Nchi za Kiarabu unajua Historia yao walifikaje Israel? Ma Zionist walitega mabomu Makazi yao na kuwaua, walisababisha machafuko Mashariki ya Kati yote ili wahamie Israel na wakafanikiwa, hilo ni kujipa Legitimacy na kuidanganya Dunia kwamba hio ni Nchi ya Kiyahudi, ila wanaoongoza hio Nchi yaani Ashkenazi sio wayahudi wa Asili.

2. Weusi Israel wengi hawatakikani huko na wanapewa mpaka vidonge wasizaliane.

3. Jews Wa Iran walikataa kwenda Israel na sababu Iran wapo vizuri Njama za Zionist hazikufika huku.

Soma hapa
 
Huyo kijana mimi nilipogundua kuwa ni mjinga, basi nikamuacha tu abaki na ujinga wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…