Bilionea Mulokozi anunua helikopta binafsi, atua Manyara, Wananchi wafika kumpokea

Bilionea Mulokozi anunua helikopta binafsi, atua Manyara, Wananchi wafika kumpokea

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
366
Reaction score
243

Na Ferdinand Shayo, Manyara.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amenunua ndege binafsi aina ya Helkopta ambapo ametua kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Stedium akiwa ameambatana na familia yake.

Mulokozi anaingia miongoni mwa Watanzania wachache wanaomiliki ndege binafsi ambapo amesema kuwa kampuni yake imekua ikikua siku hadi siku na kuonyesha vitu vya tofauti .

“Hakuna Mtu alitegemea kuwa Manyara kunaweza kuwa na helkopta ni mambo mengi yanaanza, wafanyabiashara wengi wanajifunza, kila mtu anaruhusiwa kumiliki chombo hichi inawezekana” Anaeleza David Mulokozi.
Amesema kuwa ndege hiyo itasaidia katika utoaji wa huduma katika kampuni yake inayojihusisha na uzalishaji wa vinywaji changamshi.

Mulokozi ameiomba serikali ijenge kiwanja cha ndege ili ndege nyingi zaidi ziweze kutua mkoani Manyara .

Kwa upande wao wakazi wa mkoa wa Manyara waliofika na kushuhudia helkopta hiyo ikitua akiwemo Melkiori Enyasi anaelezea furaha yake baada ya kuona ndege binafsi ya kwanza ya mkazi wa mkoa wa Manyara ikitua katika ardhi nyumbani.

Enyasi amempongeza Mulokozi kwa kununua ndege binafsi itakayochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi .

nawaza mtu unawezaje kuwa na furaha huku hela zako unazipata kwa kudhuru watu?

unauza pombe, una kampuni ya kubet...

sawa hulazimishi mtu lakini hivyo vitu unavitengeneza kwa namna inayoleta uraibu ili upate pesa nyingi

na unavitangaza kabisa

hii inakaaje?
 
kwani Kuna tatizo gani mkuu.., kama ulivyosema kuwa hawalazimishwi nadhani labda tujikite kwa wateja zaidi maake angekuwa hapati faida angeachana nayo.....
 
kwani Kuna tatizo gani mkuu.., kama ulivyosema kuwa hawalazimishwi nadhani labda tujikite kwa wateja zaidi maake angekuwa hapati faida angeachana nayo.....
kikawaida tunaambiwa mnywa pombe halazimishwi.

lakini matangazo ya pombe yamezagaa

wanatunga majina mazuri mazuri kama serengeti na rangi rangi zile kuvutia watu

halafu tunajua kabisa pombe inaleta uraibu, huwezi itumia kwa 'kiasi'

huoni siasa hapo?

yaani unamuambia mtu atumie kwa kiasi kitu ambacho kinaathiri mfumo wake wa fahamu na kufanya akose utulivu bila kuwa nacho?

kuna mtu ana maamuzi juu ya mfumo wake wa fahamu?
 
nawaza mtu unawezaje kuwa na furaha huku hela zako unazipata kwa kudhuru watu?

unauza pombe, una kampuni ya kubet...

sawa hulazimishi mtu lakini hivyo vitu unavitengeneza kwa namna inayoleta uraibu ili upate pesa nyingi

na unavitangaza kabisa

hii inakaaje?
Tafuta pesa kwa namna yoyote ilimradi hauvunji sheria. Umaskini mbaya sana
 
Back
Top Bottom