Bilionea Mulokozi anunua helikopta binafsi, atua Manyara, Wananchi wafika kumpokea

Bilionea Mulokozi anunua helikopta binafsi, atua Manyara, Wananchi wafika kumpokea

Halazimishwi mtu, it's possible labda hata mzalishaji akawa hanywi.
mihadarati ikishaingia kwenye mwili wako inasababisha utegemezi

inacheza na neurotransmitters

haulazimishwi lakini ipo wazi kwamba ukianza kutumia kutoka ni ngumu

umeelewa?

sasa huoni hapo kuna mkanganyiko?

sawa hulazimishwi, lakini huhitaji kulazimishwa ili uingie kweye uraibu!
 
nawaza mtu unawezaje kuwa na furaha huku hela zako unazipata kwa kudhuru watu?

unauza pombe, una kampuni ya kubet...

sawa hulazimishi mtu lakini hivyo vitu unavitengeneza kwa namna inayoleta uraibu ili upate pesa nyingi

na unavitangaza kabisa

hii inakaaje?
Oooh kumbe changamshi ndo pombe nilikuwa sijaelewa!
 
nawaza mtu unawezaje kuwa na furaha huku hela zako unazipata kwa kudhuru watu?

unauza pombe, una kampuni ya kubet...

sawa hulazimishi mtu lakini hivyo vitu unavitengeneza kwa namna inayoleta uraibu ili upate pesa nyingi

na unavitangaza kabisa

hii inakaaje?
Hata kanisa katoliti linaruhusu pombe,..........pombe sio haramu,,hii Dunia ukiwa boya utapigwa kama ngoma
 
kikawaida tunaambiwa mnywa pombe halazimishwi.

lakini matangazo ya pombe yamezagaa

wanatunga majina mazuri mazuri kama serengeti na rangi rangi zile kuvutia watu

halafu tunajua kabisa pombe inaleta uraibu, huwezi itumia kwa 'kiasi'

huoni siasa hapo?

yaani unamuambia mtu atumie kwa kiasi kitu ambacho kinaathiri mfumo wake wa fahamu na kufanya akose utulivu bila kuwa nacho?

kuna mtu ana maamuzi juu ya mfumo wake wa fahamu?
Biblia inasema kunywa kwa kiasi,......W.H.O March 2024,walianza kusema pombe kiasi chochote kile ni hatari,------Uislam zaidi ya miaka 1000 ulisema Pombe ni haramu
uislam upo mbele ya muda
 

Na Ferdinand Shayo, Manyara.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amenunua ndege binafsi aina ya Helkopta ambapo ametua kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Stedium akiwa ameambatana na familia yake.

Mulokozi anaingia miongoni mwa Watanzania wachache wanaomiliki ndege binafsi ambapo amesema kuwa kampuni yake imekua ikikua siku hadi siku na kuonyesha vitu vya tofauti .

“Hakuna Mtu alitegemea kuwa Manyara kunaweza kuwa na helkopta ni mambo mengi yanaanza, wafanyabiashara wengi wanajifunza, kila mtu anaruhusiwa kumiliki chombo hichi inawezekana” Anaeleza David Mulokozi.
Amesema kuwa ndege hiyo itasaidia katika utoaji wa huduma katika kampuni yake inayojihusisha na uzalishaji wa vinywaji changamshi.

Mulokozi ameiomba serikali ijenge kiwanja cha ndege ili ndege nyingi zaidi ziweze kutua mkoani Manyara .

Kwa upande wao wakazi wa mkoa wa Manyara waliofika na kushuhudia helkopta hiyo ikitua akiwemo Melkiori Enyasi anaelezea furaha yake baada ya kuona ndege binafsi ya kwanza ya mkazi wa mkoa wa Manyara ikitua katika ardhi nyumbani.

Enyasi amempongeza Mulokozi kwa kununua ndege binafsi itakayochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi .




Myie mna ushamba sana sasa hii nayo ni issue kweli?????????????????????????????????
 
nawaza mtu unawezaje kuwa na furaha huku hela zako unazipata kwa kudhuru watu?

unauza pombe, una kampuni ya kubet...

sawa hulazimishi mtu lakini hivyo vitu unavitengeneza kwa namna inayoleta uraibu ili upate pesa nyingi

na unavitangaza kabisa

hii inakaaje?

Dhambi ziko nyingi kuu.
Yeye amechagua hiyo dhambi.

Wengine wamechagua udhinifu.
Wengine malaya na wauza papuchi.
Wengine wadangaji.
Wengine waongo.
Wengine wezi,majambazi na matapeli.
Wengine wafitini, wanafiki na wambea.
Wengine dhulmati.
Wengine mashoga.

Yeye amechagua hiyo dhambi na ameweza kununua helicopter, haya sasa kazi kwenu wauza papuchi na wadangaji.

Hatupaswi kutenda dhambi bali tunapaswa kuishi vile mwenyezi MUNGU atakavyo.
 
vinywaji changamshi ndo vipi hivyo...?
hebu wekeni picha ya hivyo vinywaji..😅
images.jpeg
mati-strong-coffe-3b.png
 
Back
Top Bottom