Bilionea Mulokozi anunua helikopta binafsi, atua Manyara, Wananchi wafika kumpokea

Pamoja na kulipa kodi ila hela zake zinaonekana
Biashara ndio zinatakuwa ziwe hivyo
Ila kwa Africa ukisaidia tu upinzani basi unamalizwa
Sasa ajichanganye atoe hiyo chopper basi sifa zote zitakuwa hakuna ila ubaya

Helicopter hazina viwanja vya ndege bali ni Heliport hata yeye anaweza kutengeneza kwa vibali vya serikali
Hata akitaka juu ya nyumba
 
Na Ferdinand Shayo, Manyara.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amenunua ndege binafsi aina ya Helkopta ambapo ametua kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Stedium akiwa ameambatana na familia yake.

Mulokozi anaingia miongoni mwa Watanzania wachache wanaomiliki ndege binafsi ambapo amesema kuwa kampuni yake imekua ikikua siku hadi siku na kuonyesha vitu vya tofauti .

“Hakuna Mtu alitegemea kuwa Manyara kunaweza kuwa na helkopta ni mambo mengi yanaanza, wafanyabiashara wengi wanajifunza, kila mtu anaruhusiwa kumiliki chombo hichi inawezekana” Anaeleza David Mulokozi.
Amesema kuwa ndege hiyo itasaidia katika utoaji wa huduma katika kampuni yake inayojihusisha na uzalishaji wa vinywaji changamshi.

Mulokozi ameiomba serikali ijenge kiwanja cha ndege ili ndege nyingi zaidi ziweze kutua mkoani Manyara .

Kwa upande wao wakazi wa mkoa wa Manyara waliofika na kushuhudia helkopta hiyo ikitua akiwemo Melkiori Enyasi anaelezea furaha yake baada ya kuona ndege binafsi ya kwanza ya mkazi wa mkoa wa Manyara ikitua katika ardhi nyumbani.

Enyasi amempongeza Mulokozi kwa kununua ndege binafsi itakayochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi .

Wazee wa ndumba tunaomba ushuhuda tafazali
 
Tunazungumzia pombe kali inayoharibu maini inavyomtajirisha mwamba hadi ananunua helikopta..bado kuna lile jumba lake la mamilioni 300 huko na gari kali
Kila kitu kina madhara yake, hakuna mtu aliyeshikiwa bunduki kununua hizo pombe, kama havunji sheria, biashara yake inaliingiza taifa pato kubwa sana.
 
bilionea mkaanga maini ya vijana , ndio ujue kuwa mipombe inafakamiwa sana yaani jamaa kauza viroba sijui visungura hadi kanunua ndege na wateja wake wakubwa ni hawa hawa maafisa usafirishaji aka bodaboda. Mungu alisaidie sana taifa la Tanzania.
 
nawaza mtu unawezaje kuwa na furaha huku hela zako unazipata kwa kudhuru watu?

unauza pombe, una kampuni ya kubet...

sawa hulazimishi mtu lakini hivyo vitu unavitengeneza kwa namna inayoleta uraibu ili upate pesa nyingi

na unavitangaza kabisa

hii inakaaje?
Biashara ya pombe ndio inayoniweka mjini.
ACHANA NAYO KABISAAA

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
kikawaida tunaambiwa mnywa pombe halazimishwi.

lakini matangazo ya pombe yamezagaa

wanatunga majina mazuri mazuri kama serengeti na rangi rangi zile kuvutia watu

halafu tunajua kabisa pombe inaleta uraibu, huwezi itumia kwa 'kiasi'

huoni siasa hapo?

yaani unamuambia mtu atumie kwa kiasi kitu ambacho kinaathiri mfumo wake wa fahamu na kufanya akose utulivu bila kuwa nacho?

kuna mtu ana maamuzi juu ya mfumo wake wa fahamu?
Aseeh naona kila mmoja afanye kinachompa amani

Ikiwa anaona ni haki yake kufanya hivyo ni vizuri ikiwa sio ni vyema zaidi
Good luck
 
Na Ferdinand Shayo, Manyara.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amenunua ndege binafsi aina ya Helkopta ambapo ametua kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Stedium akiwa ameambatana na familia yake.

Mulokozi anaingia miongoni mwa Watanzania wachache wanaomiliki ndege binafsi ambapo amesema kuwa kampuni yake imekua ikikua siku hadi siku na kuonyesha vitu vya tofauti .

“Hakuna Mtu alitegemea kuwa Manyara kunaweza kuwa na helkopta ni mambo mengi yanaanza, wafanyabiashara wengi wanajifunza, kila mtu anaruhusiwa kumiliki chombo hichi inawezekana” Anaeleza David Mulokozi.
Amesema kuwa ndege hiyo itasaidia katika utoaji wa huduma katika kampuni yake inayojihusisha na uzalishaji wa vinywaji changamshi.

Mulokozi ameiomba serikali ijenge kiwanja cha ndege ili ndege nyingi zaidi ziweze kutua mkoani Manyara .

Kwa upande wao wakazi wa mkoa wa Manyara waliofika na kushuhudia helkopta hiyo ikitua akiwemo Melkiori Enyasi anaelezea furaha yake baada ya kuona ndege binafsi ya kwanza ya mkazi wa mkoa wa Manyara ikitua katika ardhi nyumbani.

Enyasi amempongeza Mulokozi kwa kununua ndege binafsi itakayochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi .

huyu ni muuaji . Watanzania wengi wanakufa kwa kunywa pombe zake za buku 2
 
nawaza mtu unawezaje kuwa na furaha huku hela zako unazipata kwa kudhuru watu?

unauza pombe, una kampuni ya kubet...

sawa hulazimishi mtu lakini hivyo vitu unavitengeneza kwa namna inayoleta uraibu ili upate pesa nyingi

na unavitangaza kabisa

hii inakaaje?
Kilevi chochote kimewekewa tahadhari kwamba kunywa kistaarabu.

Hakuna mtu anaye tengeneza pombe kudhuru watu, Na mamlaka iidhinishe hiyo pombe.

Unaye jidhuru ni wewe mnywaji kwa kutozingatia kiwango sahihi. Au kunywa kupitiliza.
 
kikawaida tunaambiwa mnywa pombe halazimishwi.

lakini matangazo ya pombe yamezagaa

wanatunga majina mazuri mazuri kama serengeti na rangi rangi zile kuvutia watu

halafu tunajua kabisa pombe inaleta uraibu, huwezi itumia kwa 'kiasi'

huoni siasa hapo?

yaani unamuambia mtu atumie kwa kiasi kitu ambacho kinaathiri mfumo wake wa fahamu na kufanya akose utulivu bila kuwa nacho?

kuna mtu ana maamuzi juu ya mfumo wake wa fahamu?
Halazimishwi mtu, it's possible labda hata mzalishaji akawa hanywi.
 
nawaza mtu unawezaje kuwa na furaha huku hela zako unazipata kwa kudhuru watu?

unauza pombe, una kampuni ya kubet...

sawa hulazimishi mtu lakini hivyo vitu unavitengeneza kwa namna inayoleta uraibu ili upate pesa nyingi

na unavitangaza kabisa

hii inakaaje?
Kampuni yake ya kubeti inaitwaje
Nataka kuijua ili tuendelee kumchangiq mwanamanyara mwenzetu kuliko kupunwa na kanji Kila siku
 
Back
Top Bottom