Uchaguzi 2020 Bilionea Nabii Shilla ajitosa kumkabili Lijualikali jimbo la Kilombero kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Bilionea Nabii Shilla ajitosa kumkabili Lijualikali jimbo la Kilombero kupitia CHADEMA

Gwajima, kauli na matendo yake ndio vimemuhukumu.
Kauli na matendo vimemhukumu kiaje?

Nyie si ndio mlisema kuwa utumishi wa Mungu na siasa ni mbali mbali sasa huyo Shilla mbona mnamfagilia au yeye sio Mtumishi wa Mungu
 
Mahaba ya kisiasa yamegandisha fikra za watu!
ukiwa upinzani hata shetani anaitwa malaika!
 
Hivi huyu kijana ni bilionea kweli au a.k.a. tu? Kama ni kweli basi thumb up na apitishwe chap chap, maana kwa ukata wa chama wacha awapelekee hizo hela watengeneza mikakati ya ushindi.😆😆
 
CHADEMA ipo kwenye mioyo ya watu/watz wkt ccm ipo kwenye mioyo ya tume na polisi
 
Bahati mbaya huwezi kukumbatia pesa halafu ukabaki na Yesu, hawa watu wanaonesha jinsi walivyo watafutaji, nawasikitikia sana hao waumini wao, naona msimu wa fursa kwao umewadia.
Hata kamani jambazi,mchawi, mwizi ,kibaka ilimradi anasimama dhidi ya hao wala nyama mi naunga mkono hoja.
 
Huyo Gwajima si mlikuwa mnamtumia kuishambulia CHADEMA?Na hiyo ndio maana halisi ya kuchanganya dini na siasa.
kwa hiyo mtumishi wa Mungu kuishambulia CHADEMA ndio kuchanganya dini na siasa, lakini kuipamba CHADEMA sio kuchanganya dini na siasa?
 
Clip yake nimeiona twitter(Darmpya Blog on twitter), imenifurahisha mno na huyu inaonyesha ni muongeaji mzuri sana.Akiingia Bungeni, itakuwa ni shida(watu wataomba muongozo wa kiti mwanzo, mwisho).

Anakwambia: Akili kichwani, pesa mfukoni, Yesu moyoni.

Msikilizeni hapa kwenye hii clip akihojiwa:



Waliojipa kazi ya kuia CHADEMA wamefeli kwa asilimia 100, kwani watia nia ni wengi nchi nzima akiwemo hyu aliewatosa watu wa chama cha kijani akaona aje ajaribu kugombea kupitia CHADEMA,huku akidai yeye hana njaa.


Hizi njaa hatari sana juzi tu hapa mlikuwa mnamponda Gwajima sasa huyu ni mchungaji wa mbuzi?
 
Huyu hajachanganya dini na siasa wandugu? Mbona naona comment nyingi tofauti na alivyotangaza nia Gwajima? Tuache unafki kwenye nyeusi tuseme nyeusi haijalishi ni upande gan!
Huyu tunajua ni Jambazi kabisa.Hata likisimama jiwe ni bora kuliko Wala nyama
 
We mbwa polepole na genge lake la serikali hii ya kishetani walisemaje kuhusu Lowasa alipokua upinzani? Na sasa wanaseje?

Jiongeze acha utumwa wa fikra mfu za pale lumumba
Matusi na lugha chafu vinachafua moyo na kupunguza uwezo wa akili

Acha jazba rudi kwenye ufahamu wako!
 
kwa hiyo mtumishi wa Mungu kuishambulia CHADEMA ndio kuchanganya dini na siasa, lakini kuipamba CHADEMA sio kuchanganya dini na siasa?
Ndugu embu rekebisha tungo yako/swali lako tata tupime mrejesho. Kwenye neno "dini" ondoa harafu weka neno "ukabila" Ntakusaidia kwa wasio elewa. Tungo yako itasomeka hivi, nakunukuu;-
" kwa hiyo mtumishi wa Mungu kuishambulia CHADEMA ndio kuchanganya ukabila na siasa, lakini kuipamba CHADEMA sio kuchanganya ukabila na siasa? " Hapo vipi. Ni muhimu kuchungulia mwendo wa uvunguni sio juu juu tu kwa atakae jibu utata huu. Wasukuma oyee!
 
Huyo Shilla,Mashimo,Gwajima wote ni matapeli tu ila kupitia mawakala tofauti.
 
Salary Slip,

Sasa huyu ndio sio tapeli ila Gwajima siku hizi tapeli, makamanda bana [emoji1787][emoji1787]

Tofauti ni moja huyu kijana hatagemei sadaka au kuuzia watu vitu kama Gwajima hakuna ushaidi huo. Gwajima anategemea watu wa kanisani kwakwe. Huyu kijana hana hata kanisa maalumu. Pili umri huyu kijana ana miaka 23-25 , tatu haingii kwa kujinufaisha au ukabila kama Gwajima ambaye ameshaitwa mpaka polisi kwasababu ya ukabila. Gwajima anafuata asali mara Chadema na mara CCM. Kawe tutakuwa tumerudi nyuma kumchagua Gwajima badala ya Halima kijana wa Kawe na mpiganaji. Yaani Gwajima mpaka anadanganya kufufua watu!!! Sio kuponya kufufua watu bila ushahidi. Cha mwisho mimi binafsi nimekutana na kuongea na Gwajima biashara hapa US 2018 hana kipaji cha unabii wala nini ni mfanya biashara mzuri na smart sana lakini sio mtu wa dini. Dogo pamoja na utoto anakipaji cha utabiri lakini haina maana hayo mengine ni yake unaweza kuwa na kipaji lakini usiwe mponyaji au muubiri. Hivyo tusilazimishe mtu awe kitu kimoja lakini dogo hategemei waamini wake kama Gwajima
 
Salary Slip,

Sasa huyu ndio sio tapeli ila Gwajima siku hizi tapeli, makamanda bana [emoji1787][emoji1787]
Gwaji boy alijipambanua ana cheo kikubwa kuliko uraisi ,uwaziri na ubunge ;so kugombea vyeo hivyo amejishusha
 
Back
Top Bottom