Bilionea Rostam Aziz amemalizana na Vodacom Tanzania (Auza hisa zote kwa Vodacom SA)

Wakati Vodacom inaingia Tanzania Rostam hakuwa mweka hazina wa Ccm wala kiongozi wa ngazi yeyote wa chama zaidi ya kuwa mbunge.

Wakti huo pia hisa zake zilikuwa chini ya 20% kabla ya kuwashawishi wenzake akina Noni kumuuzia hisa (maarifa ya biashara na kuona mbali). Kipindi hicho hakuna aliyekuwa anadhani biashara ya mitandao ya simu itakuwa kubwa kiasi hicho.

Mwaka 2013 akauza 17.2% ya hisa zake (maarifa ya biashara - biashara iko juu na hisa zina thamani kubwa sana na kusoma nyakati zinazokuja).

Hivi karibuni kauza nusu iliyobaki kwa 220 million Usd (maarifa ya biashara - ukweli kuwa soko la simu limekuwa na linaelekea kuwa gumu sana kwa sababu ya ushindani)

Nina hakika kama angekuwa na hisa za Safaricom Kenya (ambako imedhibiti soko) asingeuza hisa zake.

Tukubali tukatae, jamaa ana maarifa sana ya biashara. Bila kuwa na maarifa ya kutosha hata uwe mweka hazina wa vyama vyote huwezi kufanikiwa kibiashara kiasi hicho.
Unajuaje wewe mgerasi jamaa ana maarifa ya biashara?
 
Hapo Tanzania na Magufuli wetu hatupati kitu, Rostam Aziz ni mkwepa kodi mahiri

Fedha yake haipo Tanzania ; ipo offshore [ Jersey] Matajiri karibuni wote pengine JAH PEOPLE peke yake fedha yao imefichwa nje ya nchi!!! Mo ameficha huko DUBAI na ndio maana family yake imehamia huko; hapa kawabakizia SIMBA SPORTS club!!!
 
View attachment 1214645

Tanzanian Tycoon Rostam Aziz Sells Last Tranche Of Vodacom Shares For $220 Million

Tajiri Kongwe nchini Tanzania Rostam Aziz, Hatimaye amemalizia Ngwe ya Mwisho ya Mauzo fungu la mwisho la Hisa zake za Vodacom Tanzania kwa kuwauzia Vodacom South Africa.

Kwa Mujibu wa report kutoka Citizen newspaper, Aziz ameuza fungu lake la 588 million (Shea) iliyokuwa imebaki Vodacom Tanzania, ambayo ilikuwa ikisimamiwa na Mirambo Holdings, Moja ya kampuni zake za uwekezaji kwendaVodacom South Africa, kwa dili lililokamilishwa kupitia Dar es Salaam Stock Exchange Jumatano iliyopita.

Shea (Shares) hizo zilithaminishwa kwa takribani dola milioni mbili na ishirini $220 wakati wa mauzo. Msemaji wa Vodacom Tanzania hakutaka kutoa ushirikiano wakati alipoombwa kutoa maoni yoyote juu ya hilo.

Dili hilo limekuja karibu Miezi kumi tangu 'Washikadau' (shareholders) wa Dar es Salaam Stock Exchange-kuorodhesha kupitishwa kwa mauzo ya sehemu ya Mirambo Holdings iliyobaki Vodacom Tanzania

Rostam Aziz (55) ndiye aliyewezesha kuingia kwa Vodacom South Africa nchini Tanzania, awali alikuwa akimili wastani wa asilimia ya 35% fungu ndani ya Vodacom Tanzania.

Mwaka 2014, aliuza asilimia 17.2% ya fungu la Vodacom Tanzania iliyokuwa ikimilikiwa na kampuni yake ya binafsi ya uwekezaji Cavalry Holdings, iliyosajiliwa Jersey Island ikiwa na umiliki wa 17.8% ya hisa.

Rostam Aziz, ni bilionea wa kwanza nchini na bado anaongoza kwa biashara. Mbali na kumiliki hisa zake Vodacom Tanzania, amepata utajiri mkubwa kupitia mikataba ya uwekezaji na ujenzi wa Biashara za Mgodi Caspian Mining, Bandari ya Dar es Salaam, Majengo ya Biashara na Makazi nchini na Mashariki ya kati sambamba na uwekezaji kupitia vyombo vya habari nchini Tanzania (Channel Ten/Magic FM/ DTV/CTN/C2C nk).

Mwezi July Mwaka huu alizindua Biashara ya kiwanda cha Ujazaji gesi, Dar es Salaam (Petroleum Gas-LPG) yenye thamani ya dola za kimarekani $65Millioni.
Pia alifaidika sana na EPA.
 
Huyu jamaa ni tajiri namba 1 Tz hakuna ubishi kwenye hilo!!
Nadhani baada ya Vodacom kulazimishwa kuuza hisa zake kwa wananchi nadhani kimepalekea sakata hili.
 
Wale walionunua hisa huko itakuaje
 
Wataalanu wa hisa tusaidieni hisa za Rostam zimeuzika vipi hisa za wengine mbona haziuziki?
 
Kuna jamaa yangu alinunua hisa za vodacom kipindi wanauza mwaka juzi anasema hazijapanda bei hata sh. 1 mpaka leo.
Hii biashara ya hisa ina wenyewe.
 
Halafu haziuziki Rostam kawezaje kuuza? Soko la hisa litoe utafanunuzi kwa Nini hisa zingine Kama hizo za Rostam zinauzika na zingine haziuziki kwa Nini? Waandishi wa habari fuatilieni hilo
 
View attachment 1214645

Tanzanian Tycoon Rostam Aziz Sells Last Tranche Of Vodacom Shares For $220 Million

Tajiri Kongwe nchini Tanzania Rostam Aziz, Hatimaye amemalizia Ngwe ya Mwisho ya Mauzo fungu la mwisho la Hisa zake za Vodacom Tanzania kwa kuwauzia Vodacom South Africa.

Kwa Mujibu wa report kutoka Citizen newspaper, Aziz ameuza fungu lake la 588 million (Shea) iliyokuwa imebaki Vodacom Tanzania, ambayo ilikuwa ikisimamiwa na Mirambo Holdings, Moja ya kampuni zake za uwekezaji kwendaVodacom South Africa, kwa dili lililokamilishwa kupitia Dar es Salaam Stock Exchange Jumatano iliyopita.

Shea (Shares) hizo zilithaminishwa kwa takribani dola milioni mbili na ishirini $220 wakati wa mauzo. Msemaji wa Vodacom Tanzania hakutaka kutoa ushirikiano wakati alipoombwa kutoa maoni yoyote juu ya hilo.

Dili hilo limekuja karibu Miezi kumi tangu 'Washikadau' (shareholders) wa Dar es Salaam Stock Exchange-kuorodhesha kupitishwa kwa mauzo ya sehemu ya Mirambo Holdings iliyobaki Vodacom Tanzania

Rostam Aziz (55) ndiye aliyewezesha kuingia kwa Vodacom South Africa nchini Tanzania, awali alikuwa akimili wastani wa asilimia ya 35% fungu ndani ya Vodacom Tanzania.

Mwaka 2014, aliuza asilimia 17.2% ya fungu la Vodacom Tanzania iliyokuwa ikimilikiwa na kampuni yake ya binafsi ya uwekezaji Cavalry Holdings, iliyosajiliwa Jersey Island ikiwa na umiliki wa 17.8% ya hisa.

Rostam Aziz, ni bilionea wa kwanza nchini na bado anaongoza kwa biashara. Mbali na kumiliki hisa zake Vodacom Tanzania, amepata utajiri mkubwa kupitia mikataba ya uwekezaji na ujenzi wa Biashara za Mgodi Caspian Mining, Bandari ya Dar es Salaam, Majengo ya Biashara na Makazi nchini na Mashariki ya kati sambamba na uwekezaji kupitia vyombo vya habari nchini Tanzania (Channel Ten/Magic FM/ DTV/CTN/C2C nk).

Mwezi July Mwaka huu alizindua Biashara ya kiwanda cha Ujazaji gesi, Dar es Salaam (Petroleum Gas-LPG) yenye thamani ya dola za kimarekani $65Millioni.
Yanga hoyeeeee!
 
Exactly kama jumla ya hisa zilizo orodheshwa na kampuni usika let's say ni laki tano ambazo zinakuwa mikononi mwa watu mbali mbali ambao ni ordinary na preferred ukiweze kuwashawishi ukazinunu a zote basi kampuni itakuwa yako. Lkn mara nyingi sheria hairuhusu shares zote kumilikiwa na mutu mmoja maana ikitokea hvyo hyo Haitakuwa tena public company bali italudi kuwa private maana itakuwa inamilikiwa na mutu mmoja.
Naomba wasalimie ndugu hapo Nkasi mutu yangu
 
Halafu haziuziki Rostam kawezaje kuuza? Soko la hisa litoe utafanunuzi kwa Nini hisa zingine Kama hizo za Rostam zinauzika na zingine haziuziki kwa Nini? Waandishi wa habari fuatilieni hilo
haha...mkuu, thamani ya hisa za rostam si umeziona?? hizo unazosema haziuziki ni za shi ngapi kwani??
 
Back
Top Bottom