Hata kama ni dharura ni lazima watu wa procurements wafuate procurement procedures, hivi muende tuu kununua simenti, mabati, nondo etc kama unajenga nyumba yako si mtapigwa au hamuwajui vizuri maafisa manunuzi? Mfano kama hamjakubaliana kupata quotations ili muamue mtanunua kwa bei ipi si mtu ataenda kununua kwenye bei nafuu halafu makaratasi akaongeza cha juu?
Haraka haraka ya nini,kama ni kuchelewa,mtani umeshachelewa.Hizo fedha sio za mama Samia, ni kodi au mkopo kwa wananchi.Kuna mtu kasema acha kupotosha.Fedha ni za Watanzania.na sio zinagawanywa kwa hisani tu.Nadhani huyu mtani anadhani mama katoa kwenye pochi halafu akampa.
Shida sana, hawa wanasiasa ukimwambia atoe kwa maandishi kuamuru hizo fedha zitumike, utasubiri sana.Na ukimwambia mkuu, tunaomba idhini ya matumizi haya kwa maandishi tutumie kama supporting document,huwezi amini anakuwa mkali kuliko huyu mtani.Mara utasikia kwenye majukwaa huyu anakwamisha kazi,mara ananidharau,mara mimi ndiye rais wa mkoa huu nk.
Ok ikumbukwe,na ifahamike kuwa kuna kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za serikali kisheria zilizotungwa na bunge.Ni lazima maafisa ununuzi,wahasibu,wakurugenzi na wengine kuzifuata.Na zikifanyika kama anavyotaka huyu mtani wangu atawaruka hao wataalamu wakati Otto,Prof Asaad atakapohoji.(quere) hutaamini.Procurement prcedures zipo.Kwa nini anataka kupita short cut (Chunguzeni kuna kitu hapo).kuna mtu anatakiwa kupewa hiyo kazi bila kufuata utaratibu.PAC note down.
Hata zabuni hazijatangazwa ili kupata mkandarasi mtaalamu.Huyu mtani wangu anataka apewe billion 11 akanunue cement,mabati,matofali,
nondo nk.amesahau juzi tu mama mwenzake kwenye kamati ya PAC ilivyoibua matumizi mabaya ya fedha za serikali kwenye taasisi za serikali zikiwemo baadhi ya halimashauri.
Mimi nadhani nimshauri mtani wangu awaache wataalamu wafuate taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za serikali.Aache kuwatisha wataalamu.Wao ni wataalamu sio wanasiasa kama yeye, wamesoma na wameajiriwa kisheria,wala hawajateuliwa kwa hisani ya mtu kama yeye.
Ahsante wataalamu, simameni kwenye taaluma zenu.Akiwalazimisha aweke kwa maandishi.Jifunzeni kilichotokea kwa Yule Dc.Kwenye kutoa ushahidi alijitetea kuwa aliagizwa na ngazi za juu kwa mdomo bila document.Badala yake ona kichapo alichopata sasa.Be careful hawa wanasiasa sio watu hawa.Na yeye anataka ajulikane yupo.
Kwa nini asikae vikao vinavyojulika kiutendaji atangaze tenda,apatikane mzabuni halafu tuone kama wataalamu wangekataa kutoa fedha kwa maelekezo kutoka kwake.Wamemkatalia kwa sababu taratibu na kanuni za fedha hazijafuatwa.
Hoja za ukaguzi zikitokea wa kwanza kulaumu wataalamu hasa wahasibu na maafisa ugavi ni yeye.Na wa kujibu hoja hizo ni wahasibu na hao wataalamu wengine.Yeye anakaa mbali.Nina uzefu na hili.
Mara zote kazi za zimamoto kama anavyotaka mtani wangu ndio hapo zinapopigwa fedha za kutosha kisawasawa halafu anayeitwa kufungua anakataa kufungua kwa sababu hazifanani na b.11.
Nchi hii wengi wanafanya hivyo na kuvunja sheria halafu adhabu anabambikiziwa mtaalamu.Tufuate taratibu zilizopo kisheria na tusifanane na yule jaji wa ile kesi ya PGO.