Bilioni 650 za DP World Zamkuna Makala. Zaongeza Ufanisi wa Bandari ya Dar kutoka Makasha 7,000 Hadi Makasha 20,000

Akili huna wewe usiyefuatilia habari za maana. Kesi ya kupinga DPW asipewe uendeshaji kule Mbeya, Mwabukusi na wenzake waliangukia pua ndio SSH akaamuru mchakato wa kumkabidhi hayo magati namna 8-11 uanze mara moja.

..DPW wangekuwa toka mwanzo na malengo ya kuendesha gati # 8 - 11 na mchakato ukawa wa wazi hakuna mtu angepiga kelele.

..tatizo lilikuwa ni IGA ambayo ilipitishwa na bunge na inakiuka sheria ya ulinzi wa rasilimali iliyopitishwa mwaka 2017.

..Na mimi nalazimika kuamini kwamba bila mayowe kupigwa DPW were coming for more than just gati # 8 - 11.

..Utakumbuka kwamba TICTS hakuhitaji IGA ili kuendesha gati za makontena bandarini. ADANI naye hakuhitaji IGA ili kukodishwa gati ktk bandari yetu.

..Sasa kama Ticts na Adani hawakuwa na IGA, kwanini mambo ni tofauti kwa DPW?

..Zaidi, waliopinga IGA wako wengi zaidi ya Adv.Mwabukusi. Wako wasomi wakubwa na wanaoaminika kama Prof.Issa Shivji. Maaskofu ktk umoja wao waliounga, na si kweli kwamba alikuwa Fr.Kitima peke yake. Shura ya Maimamu walisema IGA ina matatizo.

..Wakati mwingine nadhani Watanzania hatuna skills za kupambanisha hoja zinazohusu maslahi ya taifa letu. Tunajadili mambo mazito ya kisheria kana kwamba tunajadili Simba na Yanga. Vilevile hakuna uwazi hivyo kila unakuta watu wanabishania jambo la msingi bila kuwa na taarifa za kutosha.
 
Huyo unayemsifu kama angekuwa na akili timamu angefanya yeye hayo mabadiliko ili 100% zote ziingie kwenye account ya serikali. Na si kukodisha au kugawa
 
Uongo mtupu eti ongezeko kutoka containers 7151 hadi 20151 kwa miezi mitatu? kwanza ni mapemakuona ufanisi kwa kipindi kifupi hivyo vinginevyo kama kuna ufanisi inaonesha tu hata bila uwekezaji huo bandia kungekua na ongezeko. Tatizo ni usimamizi wetu ambao umejaa upigaji na serikali haina nia kuondoa upigaji. Kuwapa wageni kuendesha bandari ni sehemu tu ya upigaji. Bandari wenyewe tumeshawekeza sana hela za umma . Hapo wageni wanakuja kula uwekezaji wa umma kwa kushirikiana na vigogo fisadi wabinafsi wasiokua na uchungu na nchi yao.
 
Urais wa TLS ni wa mwaka mmoja na unaruhusiwa kugombea na kuwa kiongozi kwa vipindi viwili mfululizo tu.

Ukishinda mara mbili mfululizo unakaa pembeni.
Nyie hata sijui mnaishi dunia gani?! Hiyo sheria ilishabadilishwa sasa hivi Rais wa TLS anahudumu kwa miaka mitatu mfululizo.
 
Zakuambiwa changanya na zako.
Aliye kuambia kwamba meli zinakaa outer Anchorage siku tatu Ni Nani wakati sisi kwa macho yetu tunaziona?
Wewe uko usweken huko unasifia kwa kuambiawa kitu usicho kiona?
Mbona ilitumika nguvu kubwa Sana kuhalalisha uwepo wa DP World mpaka kina Slaa wakawekwa ndani? Mpaka mbunge wenu mtarajiwa hapo mbeya bw Mwakubusi akaja kwenye limelight?
 
Zimemkuna wapi, makalioni?au, kichwani?
 
Kusema kwamba IGA ipo kinyume na sheria ya rasilimali ya 2017 ni kulishwa matango pori kwani bandari sio sehemu ya rasilimali, ni uvumi ulianza kipindi kile kile wakati DPW wanataka kupewa tender ya kuendesha bandari.

Huwezi kulinganisha TPA na mbuga za wanyama, huwezi kulinganisha TPA na mlima Kilimanjaro au hifadhi ya Ngorongoro, bandari ni chombo cha kiuchumi tofauti kabisa na hizo rasilimali zinavyoendeshwa. Bandarini kuna meli na makontena yanayotoka nje ya nchi, kuna magari yanayoshushwa kutoka kwenye hayo makontena unaweza vipi kuviiita hivyo vitu rasilimali za Taifa?.

IGA haiathiri ufanisi wowote wa mwekezaji wowote pale bandarini, mimi na wewe tunaweza kuanzisha kampuni ya masuala ya shipping na tukawa na vigezo vya kupewa tender ya kusimamia bandari yoyote ya TZ na hiyo IGA haitakuwa na nguvu ya kisheria ya kutuzuia kufanya lolote, hili ndilo kina Mwabukusi na hao wanasheria wengine waliloshindwa kulitolea ufafanuzi.

Kwamba mkataba mzima una vifungu 21, wao wanaongelea IGA peke yake, vipi kuhusu vifungu vingine vya mkataba mbona hawaviongelei?. Mbina hawaongelei juu ya DPW kuwapa elimu wataalam wa bandari yetu ikiwa ni sehemu ya kifungu kimojawapo kati ya vingi vilivyomo kwenye huo mkataba?.

Hakuna suala la michakato ya tender za bandarini kuwekwa wazi, ni kwa sababu za unyeti wa mikataba na taratibu zake.

Adani kapewa mkataba wa kuendesha magati namba 8-11 umewahi kuona mahali popote pale karatasi yoyote yenye kifungu chochote cha mkataba kati yake na Serikali?. Huwezi kuona kwa sababu mikataba ya kimataifa ni siri ya serikali na mwekezaji ukiiweka wazi huyo mwekezaji ana haki ya kukushtaki.

IGA haina nguvu kwani hakuna la maana kiuchumi linalowekwa ndani yake na ndio maana DPW hakushtaki mahali popote, ule mkataba uliosainiwa mbele ya Samia kule Ikulu Dodoma ukija kuwekwa hadharani na kujadiliwa serikali yetu itashtakiwa na DPW.
 
Zaidi ya malalamiko yenye msingi wa miaka ya nyuma, hakuna cha maana ulichokiandika.
 
Inatia shaka malawi na zambia wasingekimbilia msumbiji!
 
Kodi,kwani ulitaka ipate nini? Tuna capitalize kwenye mafanikio ya DP World.

Wale wengine Adani Ports sijasikia chochote kuhusu wao Toka wamepewa gati za Bandari pia.
Ukitaka kujua tuna jamii ya kijinga Adani ndiye mwenye kumiliki magati yenye faida kuliko DPW lakini sisi akili zetu kwenye IGA ya DPW kuliko kuangalia kipi anachokifanya Adani.
 
Huyu makala ni bogus sema ndio hivo ukishakuwa kwenye mfumo wa CCM
 
Mimi nasubiri taarifa ya CAG kuhusu uwekezaji huo.
 
Kwani Bandari ipo Tanzania pekee? Mkiwa na Huduma zinazokaribiana Kwa ufanisi wateja wakakimbilia kwenye shorter distance na kwako inakuwa second option
Kama wanajua kuwa bandari ni biashara ya mteja kuchagua apeleke wapi mzigo wake wasingekuja na akili za kuipinga DPW kiasi cha Maaskofu kuandika waraka wa kitu wasichokuwa na ufahamu nacho wa kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…