Billnass amzawadi Nandy gari ya ndoto yake, amwandikia ujumbe mzito mumewe

Siwajui kiundani ila nipende kusema tu hio hela hawana hata wakichanga wote wawili 🀣! Ununue LC300 400M kisha ndani ya miezi mitatu ijayo ununue LR ya 400M?

Kwa chanzo gani cha mapato au hio Nandy Festival inalipa kiasi hicho? Waseme tu gari wamepewa wazitangaze ila za tajiri flani wa showroom. Sababu Billnass nae ni dalali wa magari.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Kijana anafugwa halafu leo hii aseme ametoa Defender 110 ya 2023 kama zawadi kwa mkewe. Hilo halikubaliki duniani wala mbinguni! Maisha sio rahisi hivyo
 
Mimi peke yangu humu jf ndio naweza nunua ilo gar
 
Unalipa bei gani? Hawa wasanii ukiniambia wanatumika kama madodoki ya mafisadi ntakuelewa ila usiniambie mziki unalipa sijui blaah blaah.

Wapo wasanii kibao kina Rich Mavoko mbona hawafanyi hizo vurugu za kununua magari nao si wanaimba?
Kama Nandy muziki unamlipa, wanafanya matangazo ya bidhaa kwenye social medias accounts zao, youtube wanalipwa, shows wanalipwa za nje na ndani, siku hizi spotify, boomplay n.k wanalipwa...

Bado wana biashara zao walizoanzisha tokana na muziki, kwa msanii A list kama Nandy anaingiza pesa hizo...
 
Hela ya youtube watakuwa wanaipata ila sio nyingi kiasi cha mtu kuspend million 850 ndani ya miezi 4 😁! Hilo nakataa
Wasanii wenyewe ndo hawa wanashindana namba za kwny youtube. Platforms zinazolipa vzr, wasanii wa Tz hawafanyi vzr kwny hizo platforms(spotify, deezer, apple music, amazon n.k) Pesa ya youtube ni ya kawaida sana.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Kijana anafugwa halafu leo hii aseme ametoa Defender 110 ya 2023 kama zawadi kwa mkewe. Hilo halikubaliki duniani wala mbinguni! Maisha sio rahisi hivyo
Analiona ilo gari kama vits kila mtu anaweza kopa akanunua
 
Punguza uchawa kidogo sema ukweli ty
 
Kwa Nandy sawa ana mianya ya hela toka zama za ruge aliachwa vizuri na rangi ya mtume wakubwa lazma watakuwa wanajipigia ila Bilnass hio hela ya kununua Defender 110 ya 2023 hana. Labda kama kapewa kadi akalipie na mkewe🀣.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…