Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho


Mkuu sisi na ninyi tumefikia conclusions mbili kinzani

Sisi tunao simama na sayansi tumesema HATUJUI kwa hakika binadamu kaumbwaje zaidi ya nadharia za kisayansi

Ninyi mnadai KWA HAKIKA yupo MUNGU aliyetuumba

Kwa muktadha wa hoja zetu nadhani sasa tubadili kidogo hoja ya msingi ya awali kwakuwa sasa wenzetu mnamjua aliyeumba basi tujikite kumjadili aliyeumba ili sisi tusio mjua tumfahamu PASI NA SHAKA

Tuanze na MUNGU ni nani?
Kaumbwa na nani?
Yupo wapi?
Mmejuaje yupo?
Nini role yake kwa maisha yetu?
Nini wajibu wetu kwake?

Haya ni baadhi ya maswali yanayoweza kutoa mwanga kwa tusio mjua Mungu tukamfahamu pia

Karibu
 
Tatizo la watu kama kina Mayu na Infropreneur wanataka wapate majibu Kwa kutumia njia isiyo sahihi na halali.
Usahihi na uhalali wa hizi njia zenu uko wapi?

Zaidi ya mawazo ya kufikirika mliyonayo?

Mkiambiwa mthibitishe uwepo wa huyo Mungu mna anza kuzunguka kwa kusema mara oooh! Mungu huyo ni roho.

Mki ulizwa roho ni nini? Mnazunguka tena kwa kusema mambo hayo ni ya kiroho hayawezi kueleweka kwa Akili za kibinadamu.

Kwanza elezea
Roho ni nini? Na Mungu ni nini?

Huwezi kupata jibu la masuala ya kiroho Kwa kutumia mfumo wa kisayansi au nadharia za Wana falsafa.

Mambo ya kiroho hujadliwa kwa kutumia kanuni za kiroho!!
Kwanza elezea hiyo roho ni nini?

Na ulitambuaje roho hiyo ipo?
 
Huyo mwanaume karogwa sio Bure.
Chosen Rich hateeb10 na Mayu hebu tuje tuijadili hii habari ya mwenzetu infropreneur ambayo nimeitoa mtaa wa pili.

Jee uchawi ni nini na unaweza kuuthibtisha vipi uchawi?

Unaweza kujua chanzo cha uchawi Kwa kutumia zile njia Tano za fahamu?

Kusema mtu karogwa ni Imani ama ni jambo halisia??
 
Don't take serious mkuu.

Hapa natania tu.😄
 
Idadi ya watu duniani inaongezeka kadri muda unavyozidi kwenda, Kwa maana hiyo ilianza na 1 mpaka hapa tulipofikia...Nini unachofahamu kuhusu binadamu huyo wa kwanza kuhusu chanzo chake ?

Chanzo ni Mungu.
 
Kwa hiyo tunakubaliana kwamba Yesu ndio huyo huyo Allah pia, si ndio mkuu!?
 
Umewaza kitoto sasa,ulimwngu mzima ni dunia tu?? Wakati kuna matilioni ya sayari,nyota zote zipo kwnye dunia? Wakati kuna manyota makubwa mara mabilioni ya dunia .fanya tafiti kabla hujaandika ujinga
Kwa hiki ulichoandika, unatuthibitishia vipi uwepo wa hivyo vitu??

Sth like umeandika utoto fulani hivi.
 
Sasa hapo ndipo Ninashidana na hii nadharia ambayo inashadadiwa sana na wapinga uwepo wa Mungu.

Jee Mungu ni nani au ni nini? Jee unaweza kuelezea kuwa Ili Mungu awe Mungu anatakiwa/inatakiwa awe na sifa zipi??
Mungu ni nadharia, na jambo lolote likishakuwa ni nadharia, kila mtu atakuwa na perception tofauti juu ya jambo hilo.
 
Mungu ni nadharia, na jambo lolote likishakuwa ni nadharia, kila mtu atakuwa na perception tofauti juu ya jambo hilo.
Kwa ivo "Perception" ya nani ni sahihi nani anaamua??

Hivi Mungu ni dhana ama ni nadharia!!??
 
Rudi shule kafundishwe mada ya kuitwa "MAFUMBO" kwa mara nyingine tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…