Mayu
JF-Expert Member
- May 11, 2010
- 7,621
- 12,505
Tatizo la watu kama kina Mayu na Infropreneur wanataka wapate majibu Kwa kutumia njia isiyo sahihi na halali.
hateeb10 kajitahidi kuiweka dhana na nadharia kuhusu Mungu na uumbaji Kwa lugha rahisi sana lakini Kila wakati tunarudi kulekule.
Kwa mfano unaweza kuulizwa swali la 2+2=? na wewe ukajibu 2+2=4 na ukawa umetumia njia sahihi kujibu swali hilo.
Lakini ukitumia mfumo huu kujibu swali hilo hilo la 2+2=5-1 unaweza kung'ang'ania kuwa umetoa jibu sahihi Lakini ukweli Wa mambo utakuwa hujatumia mfumo sahihi wa kukokotoa swali la hisabati ulilopewa.
Huwezi kupata jibu la masuala ya kiroho Kwa kutumia mfumo wa kisayansi au nadharia za Wana falsafa.
Mambo ya kiroho hujadliwa kwa kutumia kanuni za kiroho!!
Mkuu sisi na ninyi tumefikia conclusions mbili kinzani
Sisi tunao simama na sayansi tumesema HATUJUI kwa hakika binadamu kaumbwaje zaidi ya nadharia za kisayansi
Ninyi mnadai KWA HAKIKA yupo MUNGU aliyetuumba
Kwa muktadha wa hoja zetu nadhani sasa tubadili kidogo hoja ya msingi ya awali kwakuwa sasa wenzetu mnamjua aliyeumba basi tujikite kumjadili aliyeumba ili sisi tusio mjua tumfahamu PASI NA SHAKA
Tuanze na MUNGU ni nani?
Kaumbwa na nani?
Yupo wapi?
Mmejuaje yupo?
Nini role yake kwa maisha yetu?
Nini wajibu wetu kwake?
Haya ni baadhi ya maswali yanayoweza kutoa mwanga kwa tusio mjua Mungu tukamfahamu pia
Karibu