Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Kwa ivo "Perception" ya nani ni sahihi nani anaamua??

Hivi Mungu ni dhana ama ni nadharia!!??
Nadharia ni mkusanyiko wa hoja mbali mbali zenye ukweli ndani yake bila kuegemea upande fulani (Theists & Atheists)

Sijui umenielewa?
 
personal attack!

Jibu kwa hoja kama unavyojibiwa.
 
Mkuu pole sana lakini binaadamu anapojaribu kujitoa ufahamu na kusahau mapungufu aliyonayo Wala haipendezi, inawezekana kujisahau lakini sio kujizima data kabisa, tusisahau mapungufu yetu ni mengi na makubwa mno kuweza kujipa cheo Cha uungu.
 
Usipojijua mwenyewe huwezi kumjua Mungu.
Umemaliza mkuu, na kujijua mwenyewe ni lazima na akili pia ziwepo ndio maana machizi hawana hukumu mbele ya mungu Kwa sababu hawajitambui
 
Mtachanganyikiwa bureeee...
Kuleni kwa sababu mna midomo
Laleni kwa sababu kuna usiku
Fanyeni kazi kwasababu mna nguvu
Fanyeni matusi kwa sbb mna vya kufanyia
Zaeni kwa sababu mna uzao n njia za kuzalia
Na mengine yote kwa sababu mna utashi...
Mkijiuliza sana hamchelewi kuwa vichaa
 
Kuwa kichaa😂, mbona mambo yako wazi Tu
 
Umemaliza mkuu, na kujijua mwenyewe ni lazima na akili pia ziwepo ndio maana machizi hawana hukumu mbele ya mungu Kwa sababu hawajitambui
Kwa hiyo mungu kawapa baadhi ya watu uchizi ili asiwatambua Mbele Yake ,basi huyu mungu atakuwa nae anauchizi kidogo
 

Mkuu hili ni swali gumu sana ambalo halina jibu moja. Ila nitajaribu kukufafanulia kadri ya upeo wangu.

Kwa sasa kuna nadharia mbili kuu zinazojaribu kuelezea jinsi binadamu alivyo tokea. Nadharia hizi ni ya Evolution na Creation.

Nadharia hizi zote zina mapungufu mengi yenye utata usio kuwa na majibu ya kueleweka.

Kwa mfano kwenye nadharia ya evolution, haielezi mwanzo au chanzo cha kiumbe kinacho evolve na pili mchakato wa evolution hata kama unatokea taratibu mno, na pia kwa nini hamna hatua za evolution sasa hivi zinazo onekana?

Kwenye nadharia ya Creation inaeleza kuwa Mungu aliumba viumbe hai na visivyo hai kwa kutamka, kitu ambacho hakiwezekani! Ni mawazo ya kufikirika. Chanzo cha Mungu mwenyewe hakieleweki kwa nadharia hii.

Ukitaka kuelewa chanzo cha viumbe tupanue wigo wa usakaji wa ukweli huo. Tuseme tutumie nadharia yangu inayoitwa nadharia ya kutazama (Observation theory).

Kwa kutumia nadharia hii, tutazame anga letu (our universe), nikufahamishe kuwa kuna universes Bilioni kadhaa kama unavyo Ona mapovu ya sabuni.

Kwenye universe/anga letu ukiangalia usiku angani utaona kuna galaxy kibao, ukweli ni kwamba kuna galaxies zaidi ya Bilioni na kila galaxy moja ina nyota zaidi ya Bilioni.

Sasa tuje kwenye galaxy yetu. Jua letu ni moja ya nyota Bilioni kwenye galaxy yetu. Jua letu lina mfumo wa sayari 8 na miezi kibao. Lengo letu tutazame composition na mpangilio wa anga unavyojiendesha kwa utimilifu.

Kwa maelezo hayo machache ni dhahiri lazima kuna viumbe vilivyo na uwezo mkubwa kimwili, kiaili, kikawi, kimaarifa kiteknolojia, kiuchumi kwa nyakati tofauti vilifanya hayo yote.

Nafahamu wengi watauliza kwamba hivyo viumbe chanzo chake ni nini? Tukifika hapa tunatumia kanuni inayoitwa: "impossibility of reverse knowledge to the source"

Kwa mfano gari, kiti, computer, simu, nguo, nyumba na kadhalika ni vyombo vinavyoumbwa/undwa na mwanadamu, kimsingi haviwezi kuwa na ufahamu/utambuzi wowote juu ya binadamu ambaye ni mtengenazaji/muumbaji/muundaji wake!

Kwa maana hiyo ukitazama wingi wa nyota angani, fikiria kila nyota ikiwa na mfumo wake wa sayari na mwezi, kama ilivyo kwenye jua letu na kukawepo na sayari moja yenye viumbe hai, unafikiri kutakuwepo na idadi ya viumbe hai kiasi gani kwenye anga letu tu?

Kimsingi viumbe hai, ni vyombo vilivyotengenezwa kwa teknologia ya juu na chanzo chake (super beings) ambao kwa hakika ndio walio husika kuumba/kuunda mfumo wote wa sayari ya dunia na dunia yenyewe.

Lengo la kuu la kuumba viumbe hai ni kutimiza haja ya kuwa na mawasiliano ya uhakika kutoka duniani pasipo kutumia nguvu na gharama kubwa ya kusafiri mara kwa mara kuja duniani.

Kama vile unavyoona tunavyotumia vyombo kama spaceship, satellite na vyombo vya kwenda mars kwa ajili ya utafiti na mawasiliano.

Kwa makini ukitazama malighafi ya kuumba viumbe hai utagundua haitokani au kufanana na malighafi yoyote hapa duniani.

Kwa mfano ukichunguza kwa makini mwili wa wabinadamu utagundua ni muunganiko wa vumbuzi mbali mbali ili kufanikisha lengo tarajiwa sawa na ilivyo kwenye gari au chombo chochote cha mwanadamu.

Tofauti kuu baina ya viumbe hai na vyombo vya mwanadamu, moja ni aina malighafi iliyotumia na pili ni uwezo wa viumbe hai kujizalisha bila gharama na bila kuleta mabadiliko yote ya kuzuia mawasiliano.

Uwezo wa viumbe hai kujizalisha ni teknolojia ya hali juu sana yenye lengo la kupunguza gharama kubwa ya uzalizaji viumbe hai wa mara kwa mara kama ikiwa uzalizaji ungekuwa unafanyiwa kiwandani.

Kujibu swali lako la chanzo cha binadamu. Niseme kwamba binadamu ana chanzo chake. Kwa kuzingatia kanuni niliyo taja hapo juu ni ngumu kuwa na ufahamu au utambuzi wowote juu chanzo chake/muumba wake kama ilivyo ngumu kwa vyombo ambayo ameviunda mwenyewe kupata ufahamu na utambuzi juu yake.

Vivyo hivyo, kanuni hiyo ina apply kwa muumbaji wa muumbaji wa binadamu kuhusu ufahamu na utambuzi juu muumbaji/chanzo chake! Na hivyo hivyo kwenye umbaji/uundaji wowote kwenda nyuma uliopo au ujao!
 
Nilitegemea uchambuzi uli mpaka na wa kina lkn naona ni kama mada chokonozi
 

Gari imeundwa na binadamu lakini haitambui kama imeundwa na binadamu...... kauli hii HAINA MANTIKI mkuu kwasababu gari halijitambui hata kama lipo

Kulinganisha gari na binadamu sio SAHIHI ni mfano MFU

Kama tunadhani binadamu lazima kaumbwa kwasababu hawezi kutokea from nowhere basi hata huyo aliyemuumba binadamu na galaxies kwa ujuzi mkubwa lazima na yeye ana chanzo...... kanuni hii inatengeneza infinity

Shida ya kanuni tunazo tumia kuhalalisha uwepo wa chanzo kisicho na chanzo inakosa MANTIKI
 

Kwa maelezo hayo machache ni dhahiri lazima kuna viumbe vilivyo na uwezo mkubwa kimwili, kiaili, kikawi, kiteknolojia, kiuchumi kwa nyakati tofauti vilifanya hayo yote.
Unathibitishaje viumbe hivyo vipo?

Uthibitisho upi una thibitisha kwamba viumbe hivyo vyenye uwezo mkubwa kimwili, kiakili, kiteknolojia na kiuchumi vilikuwepo duniani kwa nyakati hizo tofauti?
Lakini Binadamu ni Kiumbe mwenye ufahamu na utambuzi anaweza kuhoji chanzo chake ni kipi?

Maana ufahamu, utambuzi na uelewa tunao.

Vitu kama gari, kiti, computer,simu,nguo, nyumba n.k tulivyo viunda sisi wenyewe HAVIWEZI kutuhoji sisi binadamu maana havina ufahamu, utambuzi na uelewa wa kufanya hivyo.

Sisi kama tuliumbwa na hao viumbe unao dai walituumba, Kwa nini tuwe na uwezo wa kuvihoji viumbe hivyo?

Au uwezo huo wa kuvihoji viumbe hivyo, walitupa viumbe haohao?

Kwamba viumbe hivyo waliumba binadamu wenye uwezo wa kuvihoji?

Viumbe hivyo, Vilishindwaje kuumba Binadamu tusio na uwezo wa kuvihoji kama wapo kweli au hawapo?

Kama ni ngumu kufahamu na kutambua chanzo chetu binadamu ni kipi, Sasa utasemaje binadamu tuna chanzo, ilhali huwezi kuthibitisha kwamba chanzo hicho kipo?

Aliyesema kwamba Binadamu tuna chanzo(muumbaji), Yeye alifahamu vipi?

Maana umesema wazi kwamba, Ni ngumu kwa binadamu kufahamu muumbaji wake.
Vivyo hivyo, kanuni hiyo ina apply kwa muumbaji wa muumbaji wa binadamu kuhusu ufahamu na utambuzi juu muumbaji/chanzo chake! Na hivyo hivyo kwenye umbaji/uundaji wowote kwenda nyuma uliopo au ujao!
 

Mkuu una haki ya kuuliza na kuhoji na ndio maana kwenye utangulizi nilisema swali hili ni gumu lisilo kuwa na jibu moja.

Nimejaribu kutoa mawazo yangu kadri ya upeo wangu, mtazamo wangu na kwa ufuhamu wangu. Nategemea nawe katika kuhoji mawazo yangu utoe mawazo yako ili tuweze kupata jawabu.
 
Kama mungu angekuwepo basi Hata hii Post isingekuwepo
 
Mkuu haya maswall unayojiulza bila kuw na majb,
Kwangu mm ni kama Leo umekuja kwenye fikla zang inawezekn vp yaan !? Ni vyema tupate haya majb kw wajuv wa haya mambo!
 
Mkuu haya maswall unayojiulza bila kuw na majb,
Kwangu mm ni kama Leo umekuja kwenye fikla zang inawezekn vp yaan !? Ni vyema tupate haya majb kw wajuv wa haya mambo!
Mkuu mimi naamini kwamba Binadamu hatuna mwanzo wala mwisho.

Pia Dunia haina mwanzo wala mwisho.

Mungu ni mafikirio ya watu tu.
 
Vipi kama kipo ambacho ndicho mwanzo na mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…