Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Duniani sehemu gani??
Kwenye ardhi ya Dunia.
Kwa ramani ya sasa ya dunia huyo binadamu alikuwa yupo nchi gani??
Nchi na ramani ni mipaka ya kibinadamu tu iliyowekwa na binadamu.

Binadamu alikuwepo sehemu zote kwenye ardhi ya Dunia.
Na alikuwa peke yake au alikuwa na nini au na nani!!??

Alikuwepo na viumbe wengine na wanyama pia.
Ilikuwaje kukawa na utofauti kati ya maumbile ya Kike na yale ya Kiume. Hakuna aliyeyabuni maumbile hayo!!??
Mpaka sasa hakuna uthibitisho wa aliyebuni maumbile haya zaidi ya imani tu.

Na hakuna ulazima wa kwamba kuna mbunifu.
 
Mpaka sasa hakuna uthibitisho wa aliyebuni maumbile haya zaidi ya imani t
Ujue natumia nadharia zako kujenga hoja zangu.

Unasema kama kitu hakitambuliki kwa zile njia kuu za fahamu yaani kuonekana, kugusika, kusikika, kunusika na kuwa na ladha basi hicho kitu hakipo. Na kwa kuwa Mungu hana sifa hizo basi hayupo.

Maumbile ya kike na kiume yana sifa hizo zote tano. Sasa nataka uelezee imekuwaje hayafanani muundo wake wala kazi zake. Imekuwaje ni mwanaume anampa mimba mwanamke na siyo kinyume chake.

Jee kuna nguvu iliona umuhimu wa kumpa mwanamke nyonyo ili akizaa mtoto anyonyeshe ama nayo pia imetokea kwa nasibu tu?
 
Tukubali kwamba binadamu wa mwanzo hayupo.

Kila Mwaka inapofanyika sensa huonesha watu huongezeka,
Una uthibitisho wa idadi ya watu kwa miaka bilioni iliyopita kwamba walikuwa wachache?
kwa maana nyingine tunakotoka kulikuwa kuna watu wachache zaidi kuliko sasa.
Una uthibitisho wa sensa yeyote ile ya miaka bilioni iliyopita inayo onyesha kwamba kwa wakati huo dunia ilikuwa na watu wachache?
Jee akili yako haikugutushi kwamba zamani zaidi watu walikuwa wachache zaidi kuliko sasa.
Zamani hizo ulikuwepo ukathibitisha kwamba kuna idadi ndogo ya watu kuliko sasa?

Au kuna uthibitisho wowote ule wa kuonyesha miaka bilioni iliyopita kulikuwa kuna watu wachache

Ilikuwaje dunia na watu wakatokea tu kusikojulikana???
Watu na dunia hawaja tokea mahali popote pale.

Watu na dunia walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo.
 
Ujue natumia nadharia zako kujenga hoja zangu.

Unasema kama kitu hakitambuliki kwa zile njia kuu za fahamu yaani kuonekana, kugusika, kusikika, kunusika na kuwa na ladha basi hicho kitu hakipo. Na kwa kuwa Mungu hana sifa hizo basi hayupo.

Maumbile ya kike na kiume yana sifa hizo zote tano. Sasa nataka uelezee imekuwaje hayafanani muundo wake wala kazi zake. Imekuwaje ni mwanaume anampa mimba mwanamke na siyo kinyume chake.

Jee kuna nguvu iliona umuhimu wa kumpa mwanamke nyonyo ili akizaa mtoto anyonyeshe ama nayo pia imetokea kwa nasibu tu?
Nguvu hiyo ilipewa nguvu na nani?

Je nguvu hiyo ilitokea kwa nasibu tu ikampa mwanamke nyonyo?

Kama nguvu hiyo iliweza kutokea kwa nasibu tu, Hata maumbile ya kike na kiume yalitokea kwa nasibu tu.
 
Nguvu hiyo ilipewa nguvu na nani?

Je nguvu hiyo ilitokea kwa nasibu tu ikampa mwanamke nyonyo?

Kama nguvu hiyo iliweza kutokea kwa nasibu tu, Hata maumbile ya kike na kiume yalitokea kwa nasibu tu.
Unatoka nje ya nadharia zako.

Utofauti wa maumbile unatokana na nini??

Ukikubali kuwa mambo hutokea kwa nasibu nadharia yako inakufa kifo cha kawaida (Natural death).
 
Unatoka nje ya nadharia zako.

Utofauti wa maumbile unatokana na nini??
Sijui unatokana na nini.

Na mpaka sasa hakuna jibu sahihi lenye uthibitisho huu.

Hivyo mpaka sasa jibu lililopo ni kwamba utofauti huu upo tu wenyewe.
Ukikubali kuwa mambo hutokea kwa nasibu nadharia yako inakufa kifo cha kawaida (Natural death).
Sikubali kwamba mambo hutokea kwa bahati.

Ndio maana nakwambia dunia haijatokea popote pale.

Dunia ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo.

Lakini kama nguvu iliyoweka utofauti wa kimaumbile kwa binadamu ilitokea tu, Basi hata utofauti huu wa kimaumbile unaweza kutokea tu.

Si lazima kwamba utofauti huu wa kimaumbile uliwekwa na nguvu fulani.

Na utofauti huu wa kimaumbile ulitokea tu kwa logic ileile ya nguvu kuweza kutokea tu.

Na kama haiwezekani utofauti huu kutokea tu, Na nguvu hiyo unayo dai iliweka utofauti huu wa kimaumbile haiwezi kutokea tu from nothing.
 
Unatoka nje ya nadharia zako.

Utofauti wa maumbile unatokana na nini??

Ukikubali kuwa mambo hutokea kwa nasibu nadharia yako inakufa kifo cha kawaida (Natural death).
Unacho jaribu kufanya niku Exclude nguvu hiyo kwamba haijaumbwa ilitokea tu.

Kama kila kitu lazima kiwe kimeumbwa huwezi ku Exclude nguvu hiyo kwenye uumbaji.

Na nguvu hiyo lazima iwe imeumbwa.

Na kama si lazima kila kitu kiwe kimewekwa na nguvu fulani, Basi hata dunia haijawekwa na nguvu yeyote ile.
 
Infropreneur tudadavue hii hoja kwa umakini wake.

Wewe unaona utofauti wa kimaumbile ya binadamu umejitokeza tu wenyewe. Unaposema upo upo tu unamaanisha nini.
 
Infropreneur tudadavue hii hoja kwa umakini wake.

Wewe unaona utofauti wa kimaumbile ya binadamu umejitokeza tu wenyewe. Unaposema upo upo tu unamaanisha nini.
Kwa nini unadhani utofauti huu umejitokeza?

Je hudhani kwamba utofauti huu unaweza kuwepo tu wenyewe pasipo kutokea au kujitokeza?
 
Kwa nini unadhani utofauti huu umejitokeza?

Je hudhani kwamba utofauti huu unaweza kuwepo tu wenyewe pasipo kutokea au kujitokeza?
Kwa nadharia yako ni kwamba vitu vyote vipo tu kwa kuwa vipo tu.

sasa nataka kujua huu utofauti kati ya mwanamke na mwanaume upo tu bila ya kuwepo kwa kusudio??

Yaani mji wa uzazi uko kwa Mwanamke ila mbegu za uzazi ziko kwa mwanaume, ipo tu bila ya kuwa na chanzo!!??
 
Ndio ipo tu.

Hakuna chanzo.

Utofauti huu unaweza kuwepo tu, pasipo chanzo.

Utofauti ndio mwanzo wenyewe ulivyo Hivyo hivyo.
 
Absolutely yes.

Ukianza kuweka ulazima wa kwamba kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo, Basi hata
"chanzo cha vyanzo" lazima kiwe na chanzo chake,

Ili muundo ule ule wa ulazima huo ufuatwe. Pasiwepo kitu chochote kitakacho kwenda kinyume na ulazima huu kwa kujitokeza chenyewe tu pasipo mwanzo,

Maana kitavuruga muundo mzima wa ulazima huu na kuzua maswali mengi ya kimewezaje kuwepo bila chanzo.
Sio lazima chanzo cha vyanzo lazima kiwe na chanzo.
 
Sijakataa kwamba nadharia yako iko ivo. ithibitishe sasa kwa kutumia njia kuu za fahamu.

Unaposema kuwa "Unaweza kuwepo tu" hapo inaonesha huna uhakika.

Kwa ivo mwanzo wa Mwanaume ndiyo mwanzo pia wa mwanamke!!?
Binadamu ni mwanaume na mwanamke.

Utofauti wa binadamu mwanaume na mwanamke hauna aliye uweka.

Upo kama ulivyo.
 
Na hata dunia si lazima iwe na mwanzo.
Dunia lazima ina mwanzo kwani kuna matter ambazo zina disintergrate continuously. Mfano Uranium 238 half life yake ni 4.5 billion years. Sasa kama dunia ilikuwepo tangu nyuma indefinitely, Uranium yote ingeshabadilika kuwa Lead. Hivyo dunia ina mwanzo ambao si zaidi ya miaka ambayo Uranium ingekuwa imebadilika kuwa Lead.
 
Dunia ina mwanzo upi?

Uranium hiyo ilikuwa nje ya dunia?

Au uranium ipo ndani ya dunia?
 
Nguvu hiyo ilipewa nguvu na nani?

Je nguvu hiyo ilitokea kwa nasibu tu ikampa mwanamke nyonyo?

Kama nguvu hiyo iliweza kutokea kwa nasibu tu, Hata maumbile ya kike na kiume yalitokea kwa nasibu tu.
Kwa hiyo maumbile ya kike yalipokuwa yanatokea, automatically maumbile ya kiume yalikuwa yanatokea kwa nasibu tu, na maumbile ya kiume yakafiti na maumbile ya kike na yakatoa mbegu ambazo zinaungana na yai kupitia maumbile ya kike kupata mtoto. Yote hii ni nasibu tu. Kama unaamini hivyo, hata Boeing yaweza tokea kwa nasibu tu.
 
Back
Top Bottom