Binadamu Kumlaumu Mungu kwa Makosa Yake Mwenyewe.

Kama Mungu aliumba watu wamtumikie yeye peke yake, Kwa nini tena aweke freewill ya kutomtumikia?

Huu si ukichaa?

Yani anaweka freewill ya kutotumikiwa halafu asipotumikiwa anatoa adhabu!

Sasa kulikuwa na haja gani kuweka freewill ya kutotumikiwa?
Kwa nini Mungu aingilie freewill ya mtu, kuchagua kutomtumikia kwa kumpa adhabu?

Je huyo Mungu hajui kwamba watu wametumia freewill ileile kutomtumikia?

Kwa nini atoe adhabu, wakati freewill ya kutotumikiwa aliiweka yeye mwenyewe?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
 
Wewe unaamini Nini? Au Unaamini Nini Kuhusu Chanzo cha Mwanadamu Duniani hapa ! ALitokea Wapi
Kama kila kitu kilichopo kitahitaji kuwa na chanzo, Hata chanzo cha kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo chake kingine.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho exist chenyewe tu pasipo chanzo.

Hivyo kutakuwa na msururu mrefu wa vyanzo vingi visivyokuwa na mwisho.

Ikiwa mifumo tata inahitaji muumbaji, basi muumbaji naye anahitaji muumbaji aliye tata zaidi.

Hilo linapelekea msururu mrefu usio na mwisho wa waumbaji, ambapo kila mmoja anakuwa tata zaidi kuliko aliyemtangulia.

Hii inaitwa, infinite regress of causes.

An infinite regress of causes is an endless chain of events where every cause has its own prior cause going back forever.

There is no first event, no start, and no uncaused beginning.

Sasa nyie watu wa dini na imani, mnatakaga tu dunia iwe na chanzo. Halafu huyo Mungu wenu asiwe na chanzo.

Kama haiwezekani ulimwengu kuwepo wenyewe tu bila chanzo, Hata huyo Mungu wenu haiwezekani awepo tu mwenyewe bila chanzo.
 
Kama Mungu alijua hapendi mabaya yafanyike, kwa nini hakuyazuia tangu mwanzoni?

Yeye si Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele?

Je Mungu hakujua kwamba, mabaya yatakuja kufanyika, ayadhibiti mapema yasije kufanyika?

Au anapenda mabaya na alijua kwamba mabaya yatakuja kufanyika, akaacha mabaya yaje yafanyike?
 
Kuna Swali nimekuuliza

Duniani Kuna Wanadamu ambao hawatendi Dhambi na Wala hawatendi Mabaya Maisha Yao yote. Unawazungumziaje Hao?

Kama Hao wameweza Kuishi maisha Masafi unasemaje Mungu ameruhusu Mabaya. Je Hao Ambao hawatendi Dhambi wameambiwa na Nani wasitende dhambi
 
Mungu Wetu Yeye amesema Hivi

Yeye ni MWANZO na MWISHO elewa ALPHA and OMEGA. Kwahiyo hakuna Kitu kilichokuwepo Bila Yeye Kukiumba yeye ndio Chanzo cha Yote unayoyaona
 
North Korea ni shithole, hauwezi kuwa mfano mzuri kwa mungu wako, anaweza kufanya vizuri zaidi.
Ila Ww mwenyewe umesema DUNIANI.. Kwani Unadhani Watu wa North Korea si Viumbe Wake Mungu? Ila Wapo chini ya Utawala wa Mabavu ambao hawataki hata Kuhubiriwa
 
Ila Ww mwenyewe umesema DUNIANI.. Kwani Unadhani Watu wa North Korea si Viumbe Wake Mungu? Ila Wapo chini ya Utawala wa Mabavu ambao hawataki hata Kuhubiriwa
Hayupo huyo mungu unayemzungumzia.
 
1. Ukizaa mtoto akawa anakutukana kwanini unamuadhibu si Umwache Akutukane tu. Unampiga wa nini na Kumtamkia maneno ya Laana. Unaposema Mungu anaingilia FreeWill yako basi Na Wewe mwanao uliyemzaa mwache usingulie Matusi yake Yavumilie

Unapomzungumzia Mungu. Jiweke Nafasi Hiyo kwako kama Baba Unayeishi na Watoto wako ndani. Umewazaa ila Wakikukosea Unawapa Adhabu, sasa kwanini Unawaadhibu ? Ungewaacha Tu
 
1. Ukizaa mtoto akawa anakutukana kwanini unamuadhibu si Umwache Akutukane tu. Unampiga wa nini na Kumtamkia maneno ya Laana. Unaposema Mungu anaingilia FreeWill yako basi Na Wewe mwanao uliyemzaa mwache usingulie Matusi yake Yavumilie
Ningekuwa na uwezo wa kuumba mtoto ambaye hawezi kunitukana ningefanya hivyo.

Lakini sina uwezo huo, kwa sababu siwezi mambo yote.

Sasa Mungu ambaye mnadai anaweza yote, Alishindwaje kuumba binadamu ambao hawataweza kumkana, kumuasi na kutenda mabaya?
Unapomzungumzia Mungu. Jiweke Nafasi Hiyo kwako kama Baba Unayeishi na Watoto wako ndani. Umewazaa ila Wakikukosea Unawapa Adhabu, sasa kwanini Unawaadhibu ? Ungewaacha Tu
Ningekuwa na uwezo wa kuzaa watoto ambao hawanikosei, ningefanya hivyo.

Lakini siwezi kufanya hivyo, kwa sababu sina uwezo huo na siwezi mambo yote.

Sasa huyo Mungu wenu mnayedai anaweza yote, Kama hapendi binadamu wamkosee, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu wasioweza kumkosea?
 
Atleast upo honest mkuu, kitendo cha kutolea mfano north korea ni ujasiri mkubwa sana
 
Hivi mkuu wewe unassma hakuna mwanzo, au ni ngumu kufahamu mwanzo?
 
Hakuna anayeweza kuthibitisha huyo Mungu yupo.
 
Hivi mkuu wewe unassma hakuna mwanzo, au ni ngumu kufahamu mwanzo?
Ni ngumu kufahamu.

Kwa sababu binadamu hatuwezi kujua tusivyo vijua.

Lakini hata kama kuna mwanzo, bado kutaibuka tena swali, Huo mwanzo na wenyewe ulianzaje?

Lakini kama hakuna mwanzo. There's nothing to ask.
 
Hakuna anayeweza kuthibitisha huyo Mungu yupo.
1. Farao wa Misri alijua Yupo kwa kupigwa mapigo
2. Mfalme Wa Babylon alidhibitisha Yupo kwa Daniel Kushindwa Kuliwa na Simba Wenye Njaa
3. Eliya aliomba Mungu Moto ukashuka mbele ya Watu wasioamini

YOTE KWA YOTE. YESU ALIKUJA NA KUFANYA MIUJIZA MBELE YA WASIOAMINI NA WAKAAMINI KWAMBA MUNGU YUPO.

Huwezi muona kwa Macho maana Siyo kuku, bata , au samaki mwenye Mwili Yeye ni ROHO
 
Ni ngumu kufahamu.

Kwa sababu binadamu hatuwezi kujua tusivyo vijua.

Lakini hata kama kuna mwanzo, bado kutaibuka tena swali, Huo mwanzo na wenyewe ulianzaje?

Lakini kama hakuna mwanzo. There's nothing to ask.
Unapokuwa huwezi Kufahamu jambo unawezaje Kuuliza Wengine Jambo ambalo ww unasema Ni Ngumu Kufahamu?

Kama Wengine wanakuambia Chanzo ni Mungu ila Wewe unakataa ila Ukiulizwa wewe unasema ni Ngumu Kufahamu ina Maana Huna Ukweli Mwingine unaoweza Kupita Ukweli Tulionao Sisi ..ndio maana Unashindwa kufahamu

Kama Una Ukweli Kuzidi Huu ndio Uanze Kubisha...
 
mbona wewe unakataa pia madai ya jamaa kwamba "hakuna chanzo" ? sababu unazotumia wewe kukataa na yeye anatumia kukataa madai yako - mjadala sio rahisi namna hiyo mkuu
 
Mtu akikuambia rais wa Fiji ni Trump unaweza kukataa hata kama humjui rais wa Fiji,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…