Binadamu walifanya Ibada hata kabla ya hizi Dini

Binadamu walifanya Ibada hata kabla ya hizi Dini

Neno "dini" linamaanisha mfumo wa imani na ibada za kiroho au za kimungu ambazo watu wanazifuata. Dini inajumuisha mambo kama imani, maadili, ibada, na utamaduni ambao unaunganishwa na imani ya kimungu. Kwa kifupi, dini ni njia ya kumfikia Mwenyezi Mungu au nguvu za kimungu kwa njia ya imani na ibada.
Unaweza ukawa na dini lakini usiwe hata na chembe ya Imani ya kumfikia Mwenyezi Mungu ujue, ko dini haimati kama ww uko na imani thabiti
 
Umeitowa wapi hiyo maana?

Dini ni neno linalotokana na lugha ya Kiarabu. Kwa neno moja la Kiswahili, tafsiri yake inamaanisha "njia" .
 
Umeitowa wapi hiyo maana?

Dini ni neno linalotokana na lugha ya Kiarabu. Kwa neno moja la Kiswahili, tafsiri yake inamaanisha "njia" .
Umeuliza "nini maana ya neno dini" au umeuliza "asili ya neno dini"?
Ni maswali mawili tofauti na unapaswa kujua juu ya huo utofauti wake

Hata hivyo neno "njia" kwa lugha ya Kiarabu ni "sabeel" au "tariqah". Katika muktadha wa dini, neno "njia" linaweza kutafsiriwa kama "tariqa" au "tarika", ambalo linamaanisha njia au mfumo wa kufuata katika imani fulani.
Kwa hiyo bado hilo neno njia haimaanishi njia ya kupita kwa miguu au baiskeli, inamaanisha njia ya kufuata imani fulani
 
Soma historia uone watu waliishi vipi zamani. Kuna jamii ziliishi kwa kuamini katika kutoa binadam wenzao kafara Amerika ya kusini. Na hata Afrika tu kuna jamii zilikua na mila za ajabu sana za kuumiza binadam wenzao kabla ya dini
Hayo mambo ya kuua hata sasa yapo.

Al Shabaab, boko haram. al Qaeda na wengine wengi wameangamiza binadamu wenzao wengi sana bila hatia kwa sababu hiyo hiyo ya mambo ya dini.
 
Hayo mambo ya kuua hata sasa yapo.

Al Shabaab, boko haram. al Qaeda na wengine wengi wameangamiza binadamu wenzao wengi sana bila hatia kwa sababu hiyo hiyo ya mambo ya dini.
Naam na ndio maana nikasema mahali kua dini inaharibiwa sifa na watu wanao iongoza
 
Mwanzilishi wa Dini ya ukristo na uisalam ni mtu mmoja tena ni kwa lengo la utawala na biashara, hakuna cha ziada kuhusu uisalam na ukristo.

Maandiko na dini ni vitu viwili tofauti.
Tupe maana ya neno dini linatoka kabila gani
 
Dini ni njia.

Njia ya kwenda wapi?

Qur'an ina jibu la hilo...

Qur'an inasema Inna Dini Indi Allah Al Islam.

Hakika dini (njia) kwa Mwenyezi Mungu ni Uislam.

Sasa wewe jiulize, Mwenyezi Mungu yupo toka lini?

Naam, Qur'an unaielewa? Umeshachukuwa nia ya kuidoma uuelewe ujunbe uliomo japo kidogo? Au unataka kubishana kuhusu usiyoyajuwa?
Hicho kitabu cha Quran si kimeandkwa juzi karne ya 7 ? Kitabu cha juzi hapo kinathibitisha nini wakati hakikuwapo kabla ya hapo?

Unathibitisha vipi uwepo wa uislam toka mwanzo wa ulimwengu kwa kutumia kitabu kilichoandikwa juzi hapo miaka ya 600's?

Nipe Uthibitisho NJE ya Hicho kitabu cha karne ya 7 kuwa Uislam ulikuwepo kabla ya Mohamad.... Toa Uthibitisho WOWOTE ulionao... I'm here waiting for you.
 
Dini yako ni ipi? tuongelee unachokijuwa. maana dini yangu umeielewa kuhusu hicho ulichokisoma lakini hutaki kukubali.
Dini yako ya Uislam ilianza karne ya 7. Haikuwahi kuwepo kabla ya hapo.

Huu ni ukweli mchungu ambao you have to swallow it.

Hakuna maandishi yoyote YA KABLA YA MOHAMAD yanayothibitisha uwepo wa Uislam. HAYAPO.

Narudia tena, HAYAPO. Kama yapo YAWEKE HAPA.
 
Uislamu kama dini ya Kiislamu, ilianzishwa na Mtume Muhammad (SAW) huko Makkah na Madina karne ya 7 AD. Hivyo, haiwezekani kusema kwamba Uislamu uliwepo kabla ya Mtume Muhammad (SAW).

Hata hivyo, inajulikana kwamba mafundisho ya Uislamu yanategemea mafundisho ya Mitume wengine wa Mwenyezi Mungu, ambao walikuja kabla ya Mtume Muhammad (SAW). Kwa mfano, Uislamu unakubali na kuamini kwamba Mitume wote wa Mwenyezi Mungu, kuanzia Adamu, Nuhu, Ibrahimu, Musa, Isa, na wengineo, walikuja na kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu wao.

Kwa hivyo, ingawa Uislamu kama dini ilianzishwa na Mtume Muhammad (SAW), mafundisho yake yanategemea mafundisho ya Mitume wengine wa Mwenyezi Mungu ambao walitangulia kabla yake.
Kuamini manabii waliopita (ambao walizungumzwa na Tanakh ya wayahudi na Biblia ya Wakristo) hakuufanyi kuwa ulikuwepo kabla.

Point ni kuwa UISLAM ulianzishwa karne ya 7 na kabla ya hapo haukuwahi kuwepo popote pale.
 
Mungu ulimjuaje bila kupitia dini?kwa sababu babu zetu awakumjua
Walimjua vzr tu. Sema mliaminishwa kuwa walikuwa hawamjui na mkaamini. Mnazani zile mvua walizoomba zikaja zikitokana na shetani???. Plus madawa ya kujitibu unazani hizo AKILI waliipata kwa shetani. Tulimjua Mungu kabla Hao watu weupe hawajafika huku. Mbaya walivyokuja wakatuachanisha na njia ambazo zilikuwa rahisi kumfikia now tuko kama matahira
 
Kuamini manabii waliopita (ambao walizungumzwa na Tanakh ya wayahudi na Biblia ya Wakristo) hakuufanyi kuwa ulikuwepo kabla.

Point ni kuwa UISLAM ulianzishwa karne ya 7 na kabla ya hapo haukuwahi kuwepo popote pale.
Ndio nilichosema hapo. Uislamu haukuwepo kabla ya karne ya 7, Ulianza kuwepo karne ya 7 mara tu alipozaliwa mtume Muhammad (SAW)
Mtu anayesema uislamu uliwepo kabla ya hapo anataka kuleta ushabiki usio na tija tu
 
Umeitowa wapi hiyo maana?

Dini ni neno linalotokana na lugha ya Kiarabu. Kwa neno moja la Kiswahili, tafsiri yake inamaanisha "njia" .
Dini a.k.a Religion ina definition yake na inapatikana kwenye dictionary kwa sababu dictionary/kamusi ndio inayotupa tafsiri ya maneno.

Definition ya Dini/Religion sio njia.

Hiyo definition ya "Dini ni njia" ni definition ya msikitini. Lakini Definition ya Lugha ipo kwenye kamusi /dictionary na haisemi hicho unachosema
 
Unaweza ukawa na dini lakini usiwe hata na chembe ya Imani ya kumfikia Mwenyezi Mungu ujue, ko dini haimati kama ww uko na imani thabiti
Ni kweli kabisa kwamba mtu anaweza kuwa na dini lakini bado asiwe na imani thabiti au hata asiwe na imani kabisa. Dini inaweza kuwa sehemu ya kitambulisho cha mtu, lakini kile kinachomfanya mtu kuwa muumini wa kweli ni imani yake binafsi na uhusiano wake na Mwenyezi Mungu. Imani ya mtu inaweza kuathiriwa na mambo mbalimbali kama vile uzoefu wa maisha, mazingira ya kijamii, na hata elimu. Kwa hiyo, kuwa na dini haiwezi kuhakikisha kwamba mtu ana imani thabiti au ya kweli kwa Mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom