Mkuu ni kweli; lakini kwa wakati tulio nao, watu wanajaribu kuhoji ili kupata ufahamu juu mambo fulani fulani; leo huko Arabuni wa mama/wasichana hawaoni mantiki ya uvaaji wa hijabu; hawaoni kwa nini kutovaa hijabu ni dhambi, wakati Uingereza ilikuwa kuwa Waziri Mkuu ni sharti sio tu kuwa mkristo, bali uwe Mwa-anglican lakini leo hata mwarabu ana kuwa kiongonzi wao. Hivyo Mkuu, haya mambo yana badilika kutokana na wakati. Biblia inasema unapo toa sadaka hata mkono mwingine usijue!! ikiwa maana kwamba utoaji wa sadaka uwe siri yako na sio wa kujulikana na mtu mwingine. Leo inatolewa hadi na simu. Hivyo inabidi tuvumiliane tu; ni suala la muda.