Binafsi mtu anayenipa kadi ya mchango wa sherehe namwona kichwani hamnazo

Binafsi mtu anayenipa kadi ya mchango wa sherehe namwona kichwani hamnazo

Hi gentlemen!

Wakuu hivi mnalichukuliaje suala la kadi za michango ya sherehe kama hharusi na send-off?

Binafsi mtu anayenipa kadi ya mchango wa sherehe namwona kichwani hamnazo, amekosa akili kichwani.
Tubadilike, tuache kupenda mambo makuu, tufanye sherehe za kipato chetu.

Tusaidiane kwenye mambo ya elimu, biashara , ajira na afya sio mambo ya kuchangiana mtu akafanye nanilii na mwenzi wake.
Uko sahihi 100%.
 
Pamoja sana

Binafsi nilikataa kuchangiwa sendoff niliwashinda wapinzani wa katazo langu ambao ni ndugu na jamaa waliokua wanang'ang'ania ati nichangiwe sababu wao wamechangia

Unataka kuoa au kuolewa weka mipango yako sawa kadri ya uwezo wako sio kadri ya mifuko ya wengine
Sherehe hujachangia nani aje raha ya sherehe uchangie,

Mimi mwenyewe sipendi kwenda kwenye sherehe ambazo sijachangia
 
Tafuta pesa ili ufanye sherehe kubwa unayoitaka,na sio kusubiri hela za wanaume ili ukaolee.
Kuna matajiri Wana hela na still wanachangisha kwanin ili watu wawe comfortable

hivi mwanaume unavaa unapendeza unaenda kwenye sherehe unakula na kunywa huku hujachangia hata mia unajisikiaje

Mimi siwez nenda kwenye sherehe ambayo sijachangia ni bora nisiende sitakua huru
 
Sisi watanzania tumezoea kusaidiana kwenye shida na raha km huna unasema tu sasa makasiriko na kuona watu hawana akili inatoka wapi ....au ww mkimbizi nn umetoka kwenye jamii ya watu poli huko wana rohoo mbaya km shetani.
 
Kwahiyo kuomba mchango wa harusi ndo kukosa akili.

Wewe na akili zako mpaka saivi umeisaidia nini jamii inayokuzunguka tu

Si kila jambo duniani hapa lazima ukubariane nalo wewe na likiwa tofauti ulione la kijinga..!
 
Mimi nadhani "kuchangisha watu" ni umasikini mkubwa zaidi ya "kukataa kuchanga".

Tutafute hela ili tusichangishe watu kwenye mambo madogo madogo kama harusi.
Watu wajifunze kujitegemea/kusimamia mambo yao.Nitawachangia wasiojiweza na wenye nia thabiti ya ndoa.Ujanjaujuanja haufai.Kitonga kipigwe marufuku.
 
Watu wajifunze kujitegemea/kusimamia mambo yao.Nitawachangia wasiojiweza na wenye nia thabiti ya ndoa.Ujanjaujuanja haufai.Kitonga kipigwe marufuku.
Kama mtu unaweza kunywa bia za elfu 10, au 20, au hata 50 kwa mwezi kwanin nisichangie harusi

Kama unaweza mhonga mchepuko au mwanamke kwanin nisichangie life is too short ukipata nafasi na uwezo enjoy

Kwa sis Wanaume unaweza ukawa unalipia kingamuz lakin hata usipate mda hata wa kuangalia sababu unaondoka asubuhi unarudi usiku Sasa kwanin usichangie harusi
 
Hi gentlemen!

Wakuu hivi mnalichukuliaje suala la kadi za michango ya sherehe kama hharusi na send-off?

Binafsi mtu anayenipa kadi ya mchango wa sherehe namwona kichwani hamnazo, amekosa akili kichwani.
Tubadilike, tuache kupenda mambo makuu, tufanye sherehe za kipato chetu.

Tusaidiane kwenye mambo ya elimu, biashara , ajira na afya sio mambo ya kuchangiana mtu akafanye nanilii na mwenzi wake.
Hatamimi ndio falsafa yangu.
 
Bora hata hiyo kidoogo! inayonishangaza zaidi na sitakaa nichange ni ile mtu anafikisha kwa mfano miaka 5, 10 15... ya ndoa halafu anachangisha watu afanye sherehe! ujinga kabisa, wewe ndiye unayesherehekea, gharamia kila kitu ili uite watu uje ufurahi nao kwa kutimiza hiyo the so called yako! sio watu wakuchangie, alaaa! halafu unaletewa na zawadi wakati mwingine unakasirika kwa nini flani hajakuletea zawadi huo ni ung'ong'olo in "masikiopopotz voice"
 
+1
Binafsi nilifanya harusi ya kimya kimya sikutaka kusumbua watu na haikunigharimu kabisa ni zike za mafungu siku ya mkesha wa pasaka.

Wakija na kadi mkononi wanaonijua huwa nawauliza swali moja tu , unaikumbuka harusi yangu ilivyofana? story zinaishia hapo, nimewahi kuchangia harusi chache sana moja ni wa bizz mate wangu ambaye hajui history yangu

Bora nichangie mgonjwa
Hapo sawa, hata Mimi nashauri watu wafanye sherehe kulingana na uwezo walio nao.
 
Tatizo kuna maeneo kama kanda ya kaskazini ukiandaa sherehe ukaalika watu bila wao kuwa wamechanga hawaji, wanaona umewaona ni masikini hivyo umewaita ili uwalishe bure ( dharau) ndio maana hata matajiri huchangisha
 
Africa ni wachawi sana!! Hatusaidiani kwenye mambo ya msingi bali tunabebana kwenye masuala ya kipumbavu! Ndio maana wazungu wanatubagua sometimes kwa sababu mambo mengi tunayoyafanya ni ya kipumbavu na si kimaendeleo,
 
"Usiache ambachao kwa msala upitao" binafsi natoa sana sema siwez kuhudhuria wala Mimi binafsi kuchangisha mtu....ukiniletea kadi means umeniheshimu na kuona kwamba ninao uwezo basi sina shaka kuchangia ila sitoweza kuhudhuria binafsi ...nitashiriki jambo lifanikiwe tu maana kila mtu na imani yake nilishawahi kushiriki harusi ya jamaa mpaka hatua ya kupamba ukumbi ila mda wa sherehe nilisepa nikarudia nae asubuhi kutoa mapambo na kuondoa vitu kama viti..
 
Back
Top Bottom